Ndagullachrles
JF-Expert Member
- Jun 20, 2023
- 256
- 259
Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijajulikana umeripotiwa kuzuka tena kwa mara ya pili ndani ya mwezi huu wa septemba.
Moto wa kwanza uliripotiwa kuzuka September 3 katika eneo la Kikererwa wilayani Rombo lakini ulidhibitiwa ndani ya siku chache na vikosi vya uzimaji moto kutoka jeshi la uhifadhi ,jeshi la zimamoto na uokoaji ,wananchi na wadau wa utalii .
Taarifa ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa)iliyotolewa leo September 28,2026 kutoka kitengo Cha mawasiliano inaeleza kuwa moto huu wa pili umezuka eneo la Sangarini -Kamwanga kuelekea eneo la Shira ndani ya Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro mkoani kilimanjaro.
"Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa),linautaarifu umma moto umetokea katika eneo la Sangarini -Kamwanga kuelekea Shira ndani ya Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro "
"Juhudi za kuudhibiti moto huo zinaendelea ambapo Tanapa imepeleka timu za uzimaji moto ya jeshi la uhifadhi ,vikosi vya jeshi la zimamoto,wananchi pamoja na wadau wa utalii "
"Tanapa inauhakikishia umma kuwa moto huo utadhibitiwa na kwamba usalama wa wafanyakazi,watalii na wadau wa utalii ni kipaumbele cha kwanza "
"Aidha shughuli za utalii katika hifadhi ya Taifa Kilimanjaro zinaendelea kama kawaida "
Imehitimisha Taarifa ya Tanapa kupitia kwa Catherine Mbena ,Kamishna msaidizi wa uhifadhi kitengo Cha mawasiliano Tanapa Leo septemba 28,2026