Mourinho Hataki Kulea Vigonjwa

seansenior

Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
10
Reaction score
17
Baada ya mechi ya Jana kupoteza dhidi ya Brighton Mo akawachana wachezaji wake live,alisema baadhi ya wachezaji hawaumii na matokeo kama yale pia aliwaambia waandishi kuwa kwa sasa watakuwa wamepata jibu kwanini kila siku LUKAKU anamuanzisha

Amesema wachezaji wengine hawajitumi na ndio maana anawalisha mbao hayo ameyasema baada ya akina rashford na martial kuboronga Jana

Kwangu naona Mo kuongea maneno kama haya tena hadharani yana faida sana kwa wachezaji husika hii inawasaidia kukua na kujitambua pia kujifunza nini wanatakiwa kufanya kwenye wakati sahihi

Wenger amefail kuwafanya makinda wake kama hivi kwenye miaka ya karibuni na ndio wanamuangusha na kumtoa machozi

Labda kwenye kitu atakuja kujuta Wenger ni kuwaamini hawa akina Iwobi,Big Up kwa Mo kwani kauli kama zile ni nyenzo muhimu kwa mchezaji aliyebweteka
 
Morihno naye achukue likizo kama gardiola-aangalie mpira unavyokwenda aje na mbinu mpya!....
 
Lukaku kaanza game 30+ za ligi tena dakika 90 zote, lakini ana magoli 16 tu, na hayo magoli 16 asilimia 60 ametengenezewa na hawa Martial & Rashford.

Hawa vijana huwa wanapata muda mchache wa kuingia uwanjani lakini kila mmoja ana magoli karibia 7/8.

Huwezi kumpa nafasi ya kuanza kijana uliyemkalisha benchi mechi 5 mfululizo ukategemea atafanya cha ziada.

Martial & Rashford wamemzidi mbali sana huyo Lukaku. Wangekuwa chini ya kocha kama Guardiola au Wenger au Fergie au Klopp ambao wanajali vijana, sasa hivi wangekuwa mbali sana kimpira.

Mourinho amewarudisha nyuma mno.

Martial, Shaw na hata Rashford wachukue maamuzi magumu ya kutafuta maisha kwingine kama walivyofanya akina De Bruyne, Salah, nk Mourinho huwa hawaamini vijana.
 
Mkuuu umenena npo na ww kabisa,Josee anatumia rasilimali alizo nazo vibaya ndoo maana simkubali mm
 
Mkuuu umenena npo na ww kabisa,Josee anatumia rasilimali alizo nazo vibaya ndoo maana simkubali mm
Anataka ready made players. Hawezi kutengeneza vijana.

Academy ya Man U ina wachezaji wazuri sana. Kuna dogo mmoja kiungo mshambuliaji anaitwa Tahith Chong, badala ya kwenda kununua wazee kama akina Sanchez kwa pesa nyingi na kulipwa mshahara mkubwa ilipaswa kupandishwa kwa hawa vijana timu ya kwanza.
 
Shida ni kwamba hata hao ready made players anaowachukua hawatumiwi ipasavyo!
 
Mourihno hana uwezo wa kuwaamini na kukuza vipaji vya vijana.
Kwanza mfumo wake wa ku paki bus si DNA ya Man U. Wamtimue mapema
 
Mpira sio kufunga tu, Lukaku bullies opposition defense.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…