Moja ya tatizo kubwa linaloikabili tasnia yetu ni uwepo wa watu wasio sahihi kwenye tasnia...kuanzia Waigizaji mpaka Wasmbazaji mpaka wenye dhamana na Wizara ya sanaa.
Miaka ya tisini Watanzania walifanya mapokezi mazuri kwa sanaa yetu ya uigizaji, haswa baada ya ITV kuonyesha kuwa Watanzania wanalo la kufanya pia, ila kwa bahati mbaya mapokezi hayo yakaangukia kwenye mikono isiyo sahihi.
Na kama ilivyo udhaifu wa Mtanzania tamaa ya pesa huwekwa mbele kwenye kila jambo, kama wanafanya wengi wa viongozi wetu na watendaji wa Serikali, tuli/tunashuhudia jinsi ambavyo Wasanii wenyewe kuingia tamaa na kutamani kuhodhi kila kitu kinachohusu uandaaji wa muvi bila kujali weledi, na aliyekuja kushindilia jeneza kwenye hilo ni Msambazaji/Wasambazaji.
Wasambazaji walishikana mikono na Wasanii,na hii ni kwa kuwa tu usambazaji ulihitaji mtaji mkubwa ambao wasanii hawakuwa nao otherwise wasanii wangekaba kote, athari hizi ndizo zilizoendelea mpaka leo hii, na Wasanii waliotangulia ndio wa kulaumiwa pakubwa kwa jinsi walivyoshindwa kutumia vizuri MAPOKEZI ya Watanzania kwao na kutanguliza tamaa.
Tofauti na Msambazaji, Wasanii walipaswa kukaa chini na kutumia akili badala ya kuichukulia filamu kama jambo rahisi tu, leo hii tasnia ikipotea Msambazaji atabadili biashara na kumuacha Msanii anag'aa macho. Wasanii na Wasambazaji "walichangamkia tenda" hawakujali Filamu inahitaji nini kuwa Filamu, vigezo pekee walivyoshinikiza Wasambazaji ni UMAARUFU na sio sanaa, unatengeneza nini halikuwa la maana kwao, Msanii anapatana na Msambazaji, hivyo anaburundaburunda ilimradi Filamu ikamilike, then inakimbizwa sokoni bila kujali Washabiki wao.
Filamu ni team work, hivi kweli umpe JB au RAY milioni thelathini aandae muvi utegemee aumize kichwa kuandaa team ? atakachofanya ni kukusanya jamaa/rafiki zake na kuburundaburunda tu, na mfumo huu ulipelekea baada ya muda kila Msanii kutamani kuwa PRODUCER.
Nchi zote zenye akili timamu wamewekeza kwenye PRODUCERS na sio Wasanii haohao kujigeuza PRODUCERS (hapa nazungumziaa Producers kwa weledi sio Financiers), ni Producer aliyekaa darasani pekee ndiye anaweza kujua umuhimu wa SCREENWRITERS, CINEMATOGRAPHER, DIRECTOR, EDITOR n.k., ni Producer pekee ndiye ana/angeweza kumshauri Msambazaji kuwa haiwezekani kuandaa filamu ndani ya mwezi mmoja, au kukataa mambo ya pati one na two, au kutafuta Screen plays zenye ubora badala ya Msanii kujiandikia tu chochote na kuita Screenplay n.k.
Kwa hiyo kina JB, Ray, Richi, Cloudi ni wa kubebesha lawama kwa ujinga wao, na inahitaji nguvu kubwa sasa ili kufufua tena imani ya Watanzania, na kama bado kuna wanaodhani kuwa Tasnia ya Filamu haijayumba watakuwa wanazidanganya nafsi zao, Washabiki wengi wamehamia kwenye kazi za Kiharamia za kina Rufufu na wenzake, sina utafiti rasmi lakini nimeshuhudia hivyo pakubwa.