Movie Mpya ya KANUMBA Kuzinduliwa LOVE AnD POWER

Movie Mpya ya KANUMBA Kuzinduliwa LOVE AnD POWER

CompaQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2012
Posts
281
Reaction score
134
FILAMU ya aliyekuwa nguli wa
tasnia hiyo hapa nchini, marehemu
Steven Kanumba, inayokwenda
kwa jina la ‘Love and Power’
inatarajiwa kuzinduliwa rasmi
Aprili 7, mwaka huu.
Filamu hiyo, ambayo wengi
wanasema marehemu Kanumba
alijitabiria kifo chake, itazinduliwa
kwenye viwanja vya Leaders,
Kinondoni jijini Dar es Salaam, huku
ikienda sambamba na
kumbukumbu ya mwaka mmoja
tangu kufariki dunia kwake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
jana, mdogo wa marehemu
Kanumba, ambaye pia ni kiongozi
wa ofisi yake ya ‘Kanumba The
Great’ iliyopo Sinza, Seth Bosco,
alisema zaidi ya waigizaji 10
kutoka Ghana wanatarajiwa
kuwepo siku hiyo.
Alisema mbali na waigizaji hao wa
Ghana, pia rafiki wa marehemu,
ambaye ni muigizaji maarufu
barani Afrika, Mnigeria Ramsey
Noah, pia anatarajiwa kuwepo siku
hiyo ya uzinduzi.
“Ramsey tulimpigia simu na
tukamtaarifu na akasema kuhusu
uwepo wake siku hiyo, atatujulisha
kabla kama anakuja au la,
kutokana na kuwa na majukumu
mengi ya kikazi,” alisema Bosco.
Akizungumzia ratiba ya siku hiyo,
alisema itaanzia nyumbani kwa
marehemu, baada ya hapo
wataelekea makaburini na baadaye
Leaders kwa ajili ya uzinduzi huo.
Alisema wapenzi na mashabiki wa
filamu za Kanumba wanatakiwa
kufika asubuhi nyumbani kwa
marehemu kwa ajili ya ibada
itakayoanza saa nne asubuhi na
kwisha saa tano.
Alisema mara baada ya ibada hiyo,
ndugu, jamaa, marafiki, waigizaji
pamoja na mashabiki wake
watakula chakula cha pamoja kisha
kuelekea makaburini.
Aliongeza kuwa bendi ya muziki
wa dansi ya Twanga Pepeta, ndiyo
itahusika siku hiyo kwa upande wa
burudani, kisha uzinduzi rasmi
utafanyika huku nakala za filamu
hiyo zikiuzwa papo hapo.
Marehemu Kanumba alifikwa na
mauti Aprili 7, mwaka jana
nyumbani kwake Sinza Vatican,
huku kifo chake kikihusishwa na
msanii wa filamu, Elizabeth Michael
‘Lulu’.
 
Nimeona tu kakipande ka hiyo muvi. Cha kushangaza zaidi hata sharo milionea naye yumo kwenye hiyo muvi
 
Back
Top Bottom