Movie ya Hard Target

Movie ya Hard Target

Kitambo sana hii muvi enzi hizo pale kimara mwisho ilipokuwa CCM zamani tumeliwa sana tags 30 zetu pale [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ha ha ha mkuu,,,bado unakumbuka ile ya pindo la chupi?
Yule mtoto inteneti sikukubali mzigo uende bure mkuu,,,nilimalizana nae mkuu,,,
Halafu ktk mambo ya movie kuna movie zng za zamani lazima niwe nazo mkuu,,
Mfano hizo za damme ninazo kama 7 hivi..
Hard target,
AWOL
Maximum risk
Blood sports
Cyborg
Double impact
Na za Anod ninazo kama 7 hivi..
Terminator 1/2/3
Commando
Predator
Araser
Na ipo moja jina limenitoka ya 1999 inazungumzia mambo ya new millennium,,
Kuna binti mmoja anazaliwa 1976 halafu pajani kuna alama 666 ,,analelewa mission,, kwa kulindwa na pandre fulani bila yeye kujuwa,,inapita miaka 23 shetani anamtaka amtoe kafara,,wakati anord anamlinda yule binti ili ifike mwaka 2000.new millennium ili maisha yaendelee,,
Bonge moja la movie,,la anord mkuu...
Sometimes naweka kuangalia ili kunipa kumbukumbu za zamani...
Picha kama. deadly pray
War bus
The hard way
First blood 1/2/
Missing in action
Delter force
Na nyingi tu ,,,zipo home library mkuu,,,
Now hakuna .movie za kibabe..
Hiyo nadhani ni end of days.
 
Van damme hakamatiki kirahisi..ni former Force Recon marine...vita ilikuwa inamjua van damme

Hahahaha,dah hako ka verse nimekaelewa kweli kwa nakshi zake.....eti vita ilikua inamjua van damme.
 
Movie naielewaga sana hii inanikumbushaga utotoni.😀

🙌Unajua sana kusimulia.
 
Ha ha ha mkuu,,,bado unakumbuka ile ya pindo la chupi?
Yule mtoto inteneti sikukubali mzigo uende bure mkuu,,,nilimalizana nae mkuu,,,
Halafu ktk mambo ya movie kuna movie zng za zamani lazima niwe nazo mkuu,,
Mfano hizo za damme ninazo kama 7 hivi..
Hard target,
AWOL
Maximum risk
Blood sports
Cyborg
Double impact
Na za Anod ninazo kama 7 hivi..
Terminator 1/2/3
Commando
Predator
Araser
Na ipo moja jina limenitoka ya 1999 inazungumzia mambo ya new millennium,,
Kuna binti mmoja anazaliwa 1976 halafu pajani kuna alama 666 ,,analelewa mission,, kwa kulindwa na pandre fulani bila yeye kujuwa,,inapita miaka 23 shetani anamtaka amtoe kafara,,wakati anord anamlinda yule binti ili ifike mwaka 2000.new millennium ili maisha yaendelee,,
Bonge moja la movie,,la anord mkuu...
Sometimes naweka kuangalia ili kunipa kumbukumbu za zamani...
Picha kama. deadly pray
War bus
The hard way
First blood 1/2/
Missing in action
Delter force
Na nyingi tu ,,,zipo home library mkuu,,,
Now hakuna .movie za kibabe..
End of days
 
Image may contain: 1 person, motorcycle and outdoor




..Alikuwa mtaani..ndani ya orleans..hakuijua kula yake kama maskini wengine wa pale...akayakubali hayo..akayaishi maisha yake..

..Douglass binder..pamoja na hali yake ya kukosa mahitaji muhimu..hakuwahi kumuibia mtu..na aliwasaidia wenzie waliohitaji maisha kama yake..

..Hadi ilipokuja siku ya leo ngumu kwake..siku aliyopewa mkanda wenye dola elfu kumi..aufunge kiunoni..na akimbie kadri ya uwezo wake..

..Akifanikiwa kufika upande wa pili wa mji..basi pesa ile ni yake...

..Haikuwa hiyari..ilikuwa ni lazima..

..Ni mchezo wa kishenzi unaochezwa na washenzi tu..wenye pesa walikuwa wanachezea kamari maisha ya watu..

..Ukijiona unafaa kukimbia..ulikuwa unakosea..ilikuwa ni hunting..

..ili kuipata hiyo pesa inabidi uwindwe kwa kila aina ya silaha ngumu..yenye kutoa uhai wa watu..

..Douglass binder akavaa mkanda kiunoni akaanza safari..

..Ni hivo tu..alikimbia mwanzo..akashindwa mwisho..kwenye daraja la mbao..katikati ya mto..binder alipigwa mshale wa umbali mrefu na safari yake ikaishia hapo..

... Van Cleef..kiongozi wa wawindaji akamfumba macho kwa kiatu..akachukua pesa zao wakaondoka...

..Kitabu cha maisha ya binder kikafungwa rasmi..

...Natashaa..mtoto wa douglass binder..alirudi kutoka masomoni akiamini atamkuta babaake..kila alipofika aliambiwa hawakumuona..

...shida alizopata kwa siku nzima kumtafuta mzee wake..zilimpeleka mpaka kwenye mgahawa ndani ya eneo dogo la hermagodo..

..Natasha hakujua maisha ya watu wa eneo lile..alitoa pesa akahudumiwa akatoka nje..

...Ni mtu mmoja tu ndo alijua kuwa binti yule anafanya makosa kuonesha pesa nyingi hadharani..

..ndani ya eneo lile wahuni wanaosubiri kudhuru watu ni wengi kuliko maduka ya bidhaa..

..mtu yule akatangulia nje..ili yule binti akitoka aweze kumsaidia..kama wakitaka kumpora..na alivowaza ndo ilivyotokea..

..Natasha alipotoka nje akakutana na asichokijua...wakati wahuni wakitaka kuchukua mkoba wake wenye pesa..akaja mtu mwingine asiemjua pia..

...Ni jean claude van damme..fundi wa martial arts..bingwa wa mateke ya uzani wa juu duniani...

..Vann damme aliwahesabu wabaya wake kwa macho..akafunua koti mguu wake wa kulia...

..Mguu mmoja wa van damme ulibaki chini..ule mmoja ukasafiri bila kutua chini kwenye vichwa vya watu watatu..amazing..

..Msichana yule hakuamini kinachoendelea..ndani ya dakika mbili..alizubaa asijue kinachotokea...

..Inawezekana vipi binadam akawa mwepesi kiasi kile!..muda alioamaliza kuwaza van damme alikuwa kasha weka watu watano chini...natasha akamuomba vann damme amsaidie kumtafuta babaake..

..Ni hapo kizaa zaa kilipoanza...fisi anapewa bucha alinde..

...Alimuahidi pesa nyingi na van damme alikuwa muhuni tu wa mtaani..akaahidi kumsaidia..

...Ni katika kutafuta kwake ukweli wa kilichomtokea babake natashaa..vann damme alijikuta anasakwa yeye..

..Wale wawindaji walipoona damme anakaribia kuujua ukweli wa kilichotokea..wakaamua kumuangamiza yeye na natashaaa..

..Walikosea..

...Huyu wa sasa wala hahitaji kupewa mkanda wa pesa afunge kiunoni..walipoamini itakuwa ni kazi rahisi kama wanavyowafanya wengine siku zote..

..Walikosea tena kwa mara ya pili..

..Van damme hakamatiki kirahisi..ni former Force Recon marine...vita ilikuwa inamjua van damme..

..Akamwambia natasha niamini...upo kwenye mikono ya mwanajeshi..

..Natasha akavua begi akaweka bega lake kwenye kifua cha van damme akamkabidhi maisha yake...

..Akawaonesha nyayo za alipoelekea..akaamini watamfuata..

..Ni kweli walimfata...na walimkuta van damme akiwa kashauvaa ule uaname wake wa kipindi kirefu..

..Jeshi la van cleef likaandaa silaha zote za moto na za jadi..

..Van damme akafunga kitambaa mkononi akawakaribisha kwenye uwanja wake wa nyumbani...

...Ni flying kick master...skills za mateke yenye heshima ya medali ilikuwa inapatikana kwa van damme tu..

..Van cleef alipokuwa anaona watu wake wanapungua aliamua kumuita van damme kwa jina..

..Akamuuliza kwani we ni nani!...

..Muda ambao ye hamjui van damme jina..

..Ndo muda ambao van damme anavua shati anabaki na singlendi..

...Maadui wanataka amani..wakati van damme ndo anaanza vita...

...Leo waliingia sipo...

...#Hata sijui nawaza nini leo#
Hii movie ni 1 of the best yan haichoshi kabisaa!....Orlando Orlando Orlando leaving without saying goodbye[emoji41]
 
Back
Top Bottom