Movies nne kali za kucheki wiki hii

Movies nne kali za kucheki wiki hii

SteveMollel

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
8,797
Reaction score
25,177
1. TELL NO ONE.

d8f1d7081efd8285b1236ffa8f4fffbf(1).png


Ni miaka nane sasa imepita tangu dokta Alex alipompoteza mkewe, bi. Margot, kwa kuuawa kifo cha kikatili na kisha mwili wake ukatupwa karibu na makazi yao.

Kwa kipindi chote hiko mpaka sasa, dokta amekuwa akiumia na hajapata kutulia kamwe. Bado anaomboleza msiba wa mpenzi wake.

Hivyo kwaajili ya kujipa ahueni ya akili, anaamua kujikita kwenye kazi yake kwa nguvu ili asikumbuke mambo haya ya nyuma. Na pia urafiki mpya anaoutengeneza na Helen walau unamsaidia kumwepusha na upweke wa dunia.

Lakini katika haya, linakuja kuibuka jambo jipya.

Palepale alipotupiwa bi. Margot baada ya kifo chake miaka nane ilopita, imepatikana miili mipya ya binadamu wawili.

aea9823fcb6b669f3df0f961f3f2f8d8.png


Jambo hili linafufua kesi upya na vidole vyote vya polisi vinamnyooshea Dr Alex kama mtuhumiwa namba moja wa mauaji haya.

Ushahidi ndo' unasema hivyo.

Kama haitoshi, siku hii hii, Dr. Alex anapokea barua pepe yenye video inayomwonyesha mke wake, bi. Margot, akiwa mahali fulani, yupo hai, mzima wa afya!

Video hiyo imeambatana na ujumbe mfupi sana unaosema; "Tell No One." Usimwambie mtu, kisha hamna kingine kilichoandikwa.

Sasa Dr Alex, akiwa anahemewa na polisi mgongoni mwake, anaanza kuhaha kuutafuta ukweli wa mambo haya yaliyojifunga kabla muda haujamtupa mkono.

28bd201435050798f4417420e61df9f1.png


Anahangaika kujua ni nani anayemchezea mchezo huu?

Nani muuaji?

Na kweli mke wake aliyekuwa akiamini amekufa muda wote huo, yuko hai?

Kwea kwenye msako huu wa nguvu.

2. GOTHIKA.

-6021544557470138146_120.jpg


Katika hospitali hii ya wagonjwa wa akili, Dr Miranda anafanya kazi pamoja na mumewe Dr Douglas ambaye ndiye mkuu wa kitengo hiki alichomo.

Usiku mmoja wa mvua kubwa, Dr Miranda akiwa kwenye gari anaelekea zake nyumbani, anapata ajali akijaribu kumkwepa binti mmoja barabarani.

Katika tukio hili anapoteza fahamu na anapokuja kuamka anajikuta katika hospitali ileile anapofanya kazi, hospitali ya wagonjwa wa akili, ila muda huu yeye akiwa mgonjwa, si tena daktari.

d1d1276104c11f3e0bd702dd737f6e74.png


Akiwa haelewi ni nini kinaendelea hapa na amechanganyikiwa, anashangaa hakumbuki chochote kile baada ya ajali ile.

Lakini cha kumshangaza zaidi, anakuja kupata habari ya mumewe, yaani Dr Douglas, ya kwamba ameuawa kikatili na muuaji si mwingine bali ni yeye mwenyewe.

Amemuua muda gani? Hakumbuki! Achilia mbali amemuulia kitu gani.

Sasa Miranda akiwa hana kumbukumbu, tena yuko ndani ya selo za wagonjwa wa akili, anaanza kujitafuta yeye ni nani na nini kilitokea akaishia hapa.

-6021544557470138147_120.jpg


Lakini akiwa anafanya hivi, anabaini mbali na wagonjwa na madaktari katika eneo hili, pia kuna vitu vingine visivyoonekana.

Vitu hivi alikuwa akivisikia kwenye maneno ya wagonjwa kipindi anawatibu akadhani ni maradhi tu yanawasumbua, si unajua tena machizi? Kumbe ni kweli vitu vipo.

Na mbaya zaidi vinaonekana kwa wagonjwa peke yake.

Sasa itakuaje na mkasa huu? Tegua kitendawili hiki ndani.

3. BELOW ZERO (BAJOCERO)

72df17192dab98d362dc3d24855683ef.png


Siku yake ya kwanza kabisa kwenye kituo kipya cha kazi, Afisa Martin anapewa kazi ya kusafirisha wafungwa sita hatari kuwapeleka gereza jingine la mbali.

9c77efcaa7c8508e0ed0988595a3314a.png


Katika safari hii, anaambatana na afisa Montesino ndani ya basi na huko nje, mbele yao, wanatanguliwa na gari dogo la polisi lenye maafisa wawili ndani yake.

Safari inaenda vema.

Lakini wanapofika kwenye barabara yenye ukungu wa baridi kali, nyuzi joto ikiwa chini ya sifuri, hapo ndo' matata yanapoanzia.

Mbele hapaonekani.

Wanakanyaga waya wa miba ulotegwa barabarani, matairi yanapasuka na kupelekea safari kusimamia hapa.

d9c28da0bb98e74fdfe564f869c9a93b.png


Afisa Montesino anashuka kuangaza. Wenzao walokuwa wametangulia kwenye gari la mbele, wote wamekufa.

Afisa Martin anapoona kimya, naye anashuka kutazama. Anamkuta mwenzake Montesino amelala chini anamwaga damu.

Kitambo kidogo, anakumbana na bwana asiyemjua ambaye ndo ameitengeneza ajali hii. Bwana huyu amebebelea vitu viwili pamoja naye; silaha mkononi na kisasi kifuani.

Anamwaga njugu bila kujali.

Anachotaka yeye ni mfungwa mmoja alokuwamo ndani ya basi hilo. Huyo ana biashara naye ambayo anataka kuimaliza leo hii.

Apatiwe mtu huyo la sivyo hamna atakayetoka hai.

c568fb090e8525be5658d115c669106b.png


Hapa ndo' afisa Martin anapojikuta katika kazi asiyoitarajia. Moja, kuwalinda wafungwa hatari ndani ya basi na pili, kupambana na mtu hatari aliye nje ya basi.

Na wakati huo hali ya hewa ni katili mno, 'heater' imekata ndani ya basi, baridi isiyo ya kawaida inachapa kisawasawa.

Hii ndo' tunasema kazini kuna kazi.

Tazama mzigo huo.

4. THE MAN FROM NOWHERE.

1d4316fd07be81c43b10956fbf0243ba.png


"Maji yalotulia ndo' yenye kina kirefu."

Bwana Tae ni muuza duka mwenye maisha ya kimya sana. Hana marafiki wala watu wa karibu mbali na binti mmoja mdogo anayeishi jirani yake.

Binti huyo anaishi na mama yake, teja wa madawa ya kulevya, ambaye anafanya kazi kwenye klabu ya usiku.

Mara kadhaa mama huyu angekuja na wanaume tofauti wa kulala nao hapa nyumbani, binti yake akampisha kwa kwenda kukaa na mshkaji Tae mpaka atakapomaliza mambo yake.

2bb25a826a4d9fd2d28d8c5da817e2e7.png


Sasa siku moja mama huyo anaingiwa na tamaa, anaiba kiasi kikubwa cha madawa yaliyokuwa yanauzwa kule kazini kwake. Anayatia kwenye mkoba wa kamera kisha anaenda kumpatia Tae amtunzie kama bondi hapo dukani kwake.

Tae anaupokea mkoba bila kujua kinachoendelea.

Haipiti muda, wahuni wanamkamata huyu mama na kumshurutisha aseme mali yao iko wapi. Inabainika yapo kwa bwana Tae, muuza duka.

a64f61e48a62d335daf290e765f84dfa.png


Sasa shida inakuja hapa ...

Wahuni hawataki madawa peke yake, wanamteka mpaka mtoto wa mdaiwa wao.

Mtoto ambaye bwana Tae alishajipatia jukumu binafsi la kumlinda na kumsaidia kwa njia yoyote ile.

Kwa huyo mama nyie fanyeni mtakavyo, ila kwa huyu mtoto mmeuvuka mpaka.

Mwanaume anaingia uwanjani kuwajuza wahuni rangi yake halisi.

Anafanya mambo yanayowaacha watu na butwaa wakijiuliza huyu mwana ni nani hasa?

52bc722111a160ef0498077655e9ebea.png


Na nini kilimkumba akawa pale dukani kana kwamba mtu wa kawaida?
 
Movies zipo kwenye telegram channel, search UZI MKALI utanipata.

Lakini pia kuna channel ya VIP ambayo kuna;

🌟 Movies zote zilizotolewa maelezo.

🌟 Maelezo ya movie yoyote unayoitaka wewe.

🌟 Kutumiwa movie yoyote unayo-request.

Ada yake ni alfu 2 tu.
 
Mkuu SteveMollel hio a man from no where naipata wapi?
Kaka, nimeziweka movies zote kwenye channel zangu za telegram. Channels ziko mbili, ya kawaida ambayo natuma movies kadhaa na pia channel ya VIP ambayo natuma movies zote na maelezo yake.

Ingia telegram, search uzi mkali, utanipata
 
Movies zipo kwenye telegram channel, search UZI MKALI utanipata.

Lakini pia kuna channel ya VIP ambayo kuna;

🌟 Movies zote zilizotolewa maelezo.

🌟 Maelezo ya movie yoyote unayoitaka wewe.

🌟 Kutumiwa movie yoyote unayo-request.

Ada yake ni alfu 2 tu.
Pamoja Steve Ake good angalau upate ya bundle
 
Movies zipo kwenye telegram channel, search UZI MKALI utanipata.

Lakini pia kuna channel ya VIP ambayo kuna;

🌟 Movies zote zilizotolewa maelezo.

🌟 Maelezo ya movie yoyote unayoitaka wewe.

🌟 Kutumiwa movie yoyote unayo-request.

Ada yake ni alfu 2 tu.
Hy buku mbili n kwa muda gn
 
Back
Top Bottom