SteveMollel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 8,797
- 25,177
1. VACANCY.
Baada ya kumpoteza mtoto wao wa kiume, familia ya David na Amy haijapata kukaa sawa tena. Wamepoteza furaha yao na wanatazamia kuachana hivi karibuni.
Wakiwa safarini, ndani ya gari lao, wakati huu wa usiku, David anaacha njia kubwa na kufuata shortcut ili wapate kuwahi huko wanakoenda.
Lakini haichukui muda, katika njia hii, David anamwona mnyama mdogo mbele yake. Anajaribu kumkwepa na hapo ndo' gari inaharibika na safari hii inaishia hapa.
Sasa hawana namna, wanatafuta hoteli ya bei rahisi iliyopo karibu nao ili wajilaze kuuvusha usiku huu kisha asubuhi wajue nini cha kufanya.
Bahati nzuri wanaipata, na kwenye hoteli hii chakavu, kuna runinga ya kuwaburudisha. Sio kinyonge. Wanatazama filamu inayorushwa, na punde David anabaini kuna jambo fulani halipo sawa.
Filamu hii ya mauaji mbona kama anaijua?
Ebu ngoja ... anaitazama tena. Ndio. Kuna kitu anakijua humu.
Filamu hii imechukuliwa kwenye chumba hiki hiki walichokuwemo wao, na watu hawa mbona kama ali ...
Anatazama vema, kuna kamera humu ndani, zinawachukua na kuwanakili kila wanachokifanya.
Si muda mrefu anabaini jambo ya kuwa humu ndani ni 'setting' ya mauaji.
Hapa wageni wanaingia na kisha wanauawa wakirekodiwa 'live' kwaajili ya maonyesho ya wageni watakaofuatia.
Wanatazama milango, yote imeshafungwa. Kupiga simu ya msaada, nayo hamna kitu!
Sasa wanajikuta wakiungana kujiokoa na wauaji wanaomiliki hoteli hii ambayo kuingia ni gharama ya pesa ila kutoka ni gharama ya uhai.
Ndoa yako ilokuwa inayumba, inabidi isahau yalopita, ili wapate kutoka hai hapa.
Ni nani wauaji na wanataka nini?
Na je, watatoboa kuuvuka usiku huu mrefu?
Jipe raha.
2. THE CALL.
We unasema kazi yako ina stress kisa bosi wako Muhindi, ushawahi kuwafikiria wahudumu wa namba za dharura?
Wanatoka nyumbani kwenda kupambana na simu za watu wanaobakwa, wanaotaka kuuawa, wanaotekwa, wanaovamiwa.
Kila unapoweka simu sikioni, basi ni tatizo.
Yani kila simu na mkasa wake.
Mkasa mmoja wao ni huu anaokutana nao opareta wa 911, jina lake Jordan.
Siku hii akiwa kazini kama kawaida yake, anapokea simu ya mtoto Lea. Mtoto anapiga simu akiwa anatetemeka wa hofu, anamwambia kuna mtu ameingia ndani kwao na anataka kumuua.
Jordan anajaribu kumtuliza na kumshauri akajifiche juu, kidogo simu inakata. Jordan akiwa hana uhakika na usalama wa Lea, anapiga simu tena aongee naye.
Simu kuita inakuwa makosa makubwa.
Mlio wake unamshtua muuaji na kumsaidia kufahamu alipojificha mtoto Lea.
Kwa kutumia simu, Jordan anamsihi muuaji asifanye alichopanga kufanya lakini anachelewa.
Muuaji anamwambia;
"Tayari ishaisha."
Kisha anakata simu.
Kesho yake mapema, kwenye runinga, Jordan anaona habari ya kifo cha mtoto Lea.
Roho inamuuma sana kwa kutomsaidia binti huyu.
Sasa anaona inatosha, hataki tena kupokea simu za wahanga, yeye atabakia kama mkufunzi wa wafanyakazi wapya katika kitengo hiki cha dharura.
Miezi sita baadae, akiwa kazini kama mkufunzi, anakutana na mkasa mwingine wa mtoto mwingine.
Siku hiyo inapigwa simu anapokea mhudumu mwanafunzi. Anayepiga simu ni binti Casey ambaye ametekwa na mtu asiyemjua kisha akafungiwa kwenye buti la gari.
Anapiga simu kuomba msaada haraka. Anaogopa sana.
Ubaya simu aliyotumia ni 'disposable phone', hii huwezi kui-track. Sasa hapa utashi wa mhudumu unahitajika. Tena mhudumu mzoefu ili kumnusuru na kifo.
Hapa ndo' Jordan anakabidhiwa tena simu ili amuokoe mhanga.
Sasa simu hii ndo' kisanga chenyewe.
Jordan anaongea na mhanga akimpa maelekezo nini afanye kujiokoa, lakini kadiri muda unavyozidi kwenda, hali inazidi kuwa ngumu, hatari inazidi kuongezeka.
Simu hii ni simu ya kifo na Jordan anahaha sana kurekebisha makosa yake ya awali.
Sasa ataweza kumwokoa binti huyu kwa kutumia sauti yake tu?
Tazama kigongo hiki.
3. THE MIST.
Baada ya kimbunga kikali kuchapa kitongoji cha Bridgton, mji wa Maine, maisha yanabadilika kabisa.
Mbali na madhara mengine, kimbunga hiki kimeleta janga kubwa ambalo hamna anayelijua vema.
Kwenye majira ya asubuhi, David na mkewe wakiwa wanatazama mti uloangukia nyumba yao sababu ya kimbunga kile, wanagundua kuna ukungu mkubwa unasogelea ziwani.
Baadae David akiwa pamoja na mwanae, wanafunga safari kwenda kununua mahitaji yao ya nyumbani.
Wakiwa ndani ya supermarket, wanashangaa kuona magari ya polisi huko nje yakiwa yanakatiza kwa kasi sana.
Mara anaingia mtu mmoja humu ndani.
Mtu huyu ana woga sana.
Anasema kwa hofu ya kwamba huko nje kuna hatari ... kule kwenye ukungu mkubwa kuna hatari.
Kabla hajaeleweka hatari gani, king'ora cha tahadhari kinalia kwanguvu huko nje kuwaonya raia popote pale walipo.
Sasa meneja wa supermarket anafunga lango la duka, na watu wanabakia humu ndani wakati ukungu ukiendelea kusambaa huko nje ...
Na ukiwa unasambaa, watu pia wanakufa wakimezwa na viumbe vilivyomo ndani ya ukungu huu wa ajabu.
Sasa David na wenzake wanajikuta katika mtihani mkubwa. Mkewe yuko nyumbani. Wao wamefungiwa madukani na nje kuna hatari isiyo na mfano.
Ni baadae ndo inakuja kugundulika, janga hili limesababishwa na kufeli kwa jaribio la jeshi liitwalo 'Project Arrowhead'.
Jaribio hilo limefungua malango kwa kiumbe cha hatari kisichoeleweka nguvu wala udhaifu wake.
Hivyo mji wa Maine, kufumba na kufumbua, unageuka kuwa ulingo, kila mmoja akihaha kupambania uhai wake kabla ukungu huu haujawameza wote.
Tazama chombo hiyo.
4. THE GIRL ON THE TRAIN.
Rachel ameshaachana na mumewe na sasa kila mtu ana maisha yake. Bwana ameshaoa na hivi sasa ana mtoto huku Rachel akiwa bado single, mpweke na mlevi.
Mbaya zaidi, Rachel akiwa ndani ya treni, kila siku iendayo kwa Mungu kwenda jiji la New York, anakatiza njia iliyo karibu na makazi yake ya zamani alokuwa anaishi na mwanaume huyu waloachana.
Hivyo apende asipende, atapaona mahali hapa na tena siku nyingine atamwona ex wake pamoja na familia yake; mkewe mpya na mtoto wao wakiishi kwa furaha.
Just imagine.
Kwasababu hii, Rachel anaamua kupuuza eneo hili na kuanza kuzingatia zaidi majirani zake, na hapo ndo anapoiona familia ya mwanamke Megan na mumewe Scott.
Familia ambayo Rachel anaamini ni familia 'perfect', yenye mapenzi ya dhati.
Basi anaitazama kwa macho ya wivu.
Lakini siku moja, akiwa katika treni kama kawaida yake, anashuhudia kitu asichokitarajia.
Anamwona Megan akimbusu mwanaume mwingine na hapo anabaini kumbe familia hii siyo kama vile alivyokuwa anaiwaza.
Swala hili linamkwaza.
Baadae anapiga zake vyombo na kuzima. Anapokuja kuamka ana 'hangover' ya maana, majeraha mwilini na hakumbuki nini kilitokea jana yake.
Mara kwenye TV anaona habari. Yule mwanamke Megan amepotea na inahofiwa amekufa.
Sasa hapa ndo' Rachel anashangaa. Kwanza kilitokea nini jana yake mpaka akaamka na majeraha?
Na kitu gani kimemtokea yule Megan aliyemwona mzima akiwa anamsaliti mumewe?
Basi anatoa taarifa kwa polisi juu ya kile anachokijua kumhusu Megan. Lakini ajabu polisi wanaanza kumshuku mwanamke huyu kuwa huenda ni yeye ndo amehusika na tukio.
Kwanini?
Na ukweli wa mambo ni upi?
Cheki mzigo huo, THE GIRL ON THE TRAIN.