Preta, Kama nitakuwa nimewaelewa watoa huduma, watakuwa wamesema moyo ''umekuwa mkubwa'' kwa lugha ya kitaalam wanasema Heart enlargement hasa wanapotumia vipimo vya kuonyesha moyo. Hii ina maana kuwa moyo ''haujavimba'' bali umeongezeka size. Sababu ni nyingi, lakini kwa ufupi ni kuwa inawezekana mahitaji ya mwili[kwa damu] yameongezeka na hivyo kulazimisha moyo kufanya kazi ya ziada, au performance ya moyo haitoshelezi mahitaji ya mwili kwa sababu kadhaa, hali hii inaitwa compensatory mechanism.Kwahiyo kuongezeka size sio tatizo la awali bali ni dalili za kuwepo kwa tatizo mahali fulani. Sababu za tatizo zikitafutiwa ufumbuzi moyo utarudi katika hali yake ya kawaida, na kwa hiyo matibabu hayalengi moyo bali sababu zinazopelekea moyo kufanya hicho kinachoitwa ''compensatory mechanism''.
Pamoja na maelezo haya, wataalam waliokaribu na mgonjwa wanaweza kutoa sababu halisi kutokana na picha au vipimo. Ninachotaka kukuambia hapa ni kuwa kuvimba kwa moyo[ mimi ningesema kuongezeka ukubwa] ni hatua za moyo wenyewe inazochukua kukabiliana na tatizo fulani linaloathiri utendajikazi wa moyo. Kwa vile bibi yupo KCMC nina hakika kuwa wataalamu watamshughulikia vizuri na usiwe na hofu, tumuombe mola matibabu yampe bibi unafuu na arejee hali yake.
[kwa wasomaji: Unapomuona mbeba lumbesa ana kifua kimegwanyika, au bega limejaa hatusemi amevimba kifua au bega,tunasema amejaa au ameongezeka/ ametuna kifua au bega Enlarged chest/ shoulder muscles. Lakini ukijikwaa kidole, au ukawa na kidonda mguu ukavimba, au akawa umeumia kwa kitu mkono ukavimba, au ukawa umeumwa na nyuki uso ukavimba, hapa tunatumia neno kuvimba Inflammation hatusemi enlargement]
Ahsante