Moyo unanilazimisha kusema!

Moyo unanilazimisha kusema!

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Wewe ni kama hewa mwanana inayopatia mapafu yangu furaha iliyonjema!.. kila neno lako nalikumbuka na isitoshe hata lile cheko lako tamu nalikumbuka pia!.

Nahisi Kama nina deni kwako haswa pale picha yako ikinijia usoni ni kama vile inaniambia "Ninayo Siri,Njoo uifunue!".

Labda nilikuuzi kwa ukomamanga wangu! Hope you know it,lkn sidhani kwa kiwango hicho unachofikiri!. Kitu usichokijua ni kuwa mwenzako nimekolea zaidi namaanisha vipimo vya penzi langu kwako vimeimalika zaidi!

Bado nafasi ya upendeleo ipo juu yako hata lile gurudumu tuliokuwa tukilisukuma hivi sasa limekuwa jepesi zaidi ila linanishinda maana umeniachia pekee na umebaki ukinitazama!.

Wewe ni fahari kwangu maana umeonyesha tamanio lako kwangu!,japo unajitia ukaidi lkn nakuhakikishia grass lazima ipasuke!... Sikutishi bali nakuvuta kwasababu ulianza wewe kunivuta hivyo ninayo haja ya kung'ang'ania mvuto wako,maana ni muda sahihi na ni mtu sahihi pia..

Nisitie chumvi nyingi ikakulevya ukaja zimia nikakukosa haja wa moyo wangu!.. yamenitoka hayo machache Ila yatakuwa mazito ukizembea.

Ni mimi komamanga wako.
 
Inategemea na hali fikra na moyo na mawazo na maisha kwa ujumla wake. Niliwahi pokea sms ya aina hii toka kwa mwanamke ambaye tuliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi kirefu kiasi lakini penzi likaja kufa

Nilimjibu tu kifupi "Too late".
 
Inategemea na hali fikra na moyo na mawazo na maisha kwa ujumla wake. Niliwahi pokea sms ya aina hii toka kwa mwanamke ambaye tuliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi kirefu kiasi lakini penzi likaja kufa

Nilimjibu tu kifupi "Too late".
Hii si hivyo mkuu!
 
Hayo maneno unamuambia jiwe au nani maana maccm akili zenu mnazijua wenyewe
Subiri 28 ukapige kura kila mtu aangaike na linalomuhusu easy like that.
 
Back
Top Bottom