Moyo wa nguruwe sasa yathibitika unaweza kuokoa maisha ya mwanadamu

Moyo wa nguruwe sasa yathibitika unaweza kuokoa maisha ya mwanadamu

Ehud

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2008
Posts
2,685
Reaction score
338
Wataalam nchini marekani kwa mara nyingine tena wamethibitisha umuhimu wa nguruwe kwa maisha ya mwanadamu pale majaribio yao ya moyo wa nguruwe waliomuwekea nyani kuonesha pasi na wasi kuwa unaweza kumsaidia nyani kuishi tena. Mafanikio hayo yanatafsiriwa kuwa ni hatua muhimu katika kusaidia kuokoa maisha ya wanadamu ambao watakuwa wakihitaji kuwekewa moyo baada ya mioyo yao kuwa na matatizo.

Hayo yalitangazwa na jopo la madaktari katika kituo cha USA cha National Heart, Lung and Blood Institute huko Bethesda, Maryland wakiiongozwa na Dr. Muhammad Mohuiddin.

Haya sasa wale wasiompenda mnyama muhimu kwa maisha ya mwanadamu kazi kwenu....muoneni Dr wa ukweli mwenye jina lake hapo anavyofanya kazi yake bila kinyongo:roll:

p01yptkq.jpg

Soma zaidi hapa: BBC - Future - Would you accept a pig?s heart?
 
sijui ni mimi nakosea?? ila nguruwe kama mammal ana mfumo kama wa binadamu na nyani na tofauti iko lkn ni ndogo sana na hii hasa ipo kwenye mfumo wa akili na sauti. na hapa tunaanza kutofautiana kutoka kwenye genus
 
sijui ni mimi nakosea?? ila nguruwe kama mammal ana mfumo kama wa binadamu na nyani na tofauti iko lkn ni ndogo sana na hii hasa ipo kwenye mfumo wa akili na sauti. na hapa tunaanza kutofautiana kutoka kwenye genus

Sasa mwalimu, genes si tofauti? Na moyo si utakuwa na tudamu damu twa kitimoto, sijui magroup nayo yakoje.
 
hapo sasaa utakubali kufaa ama kupona kwa kuwekewa moyo wa kitimoto?
 
Sasa mwalimu, genes si tofauti? Na moyo si utakuwa na tudamu damu twa kitimoto, sijui magroup nayo yakoje.

yeah lkn kuna study moja niliwah kuiona imefanywa na mdada mmoja Dr Makame kwenye mambo ya genomics, ilionyesha baadhi ya nguruwe wana blood groups AB AND B, na wengine A NA O, ila sasa Rh1 antibodies haikuwa na reaction wakati wa kutest.....

so utofauti upo sana tu lkn si kwenye shape ya moyo wenyewe hapana so wako ijnterested na moyo as moyo na asio damu na ni rahisi sana kuondoa damu yote ya nguruwe ndani ya moyo wake ukiwa nje ya nguruwe
 
Kwani huyo atakayewekewa moyo wa Kitimoto atakuwa amekula ? Si amewekewa tu ndani ya mwili wake?

Kama kula tu ni haramu
Je kuwekewa ndo itakuwa halal I?
 
Sisi tutakufa tu pesa ya kwenda kutibiwa Marekani ipo wapiiii yaan huyu mnyama mnajitahid kumsafishaaaa
 
Huo moyo wangemwekea ustadhi sheh Ilunga angepona kabisa
 
Siyo moyo tu, hata nyuzi za kushonea wakati wa operesheni zinatengenezwa kutokana na utumbo wa nguruwe. Nyuzi hizo hazitolewi bali hubadilika kuwa nyama kidonda kikipona.
 
Qur'an: 2

10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. ***

2_11.gif
11. Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. ***

2_12.gif
12. Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui.
 
Kama kula tu ni haramu
Je kuwekewa ndo itakuwa halal I?
Watu tutaanza kukimbiana hapa, Nilifundishwa kwenye biology kuwa Nguruwe na mwanadamu wana sifa zinazofanana, Mfano nguruwe anakula majani (Herbivorous) , Anakula Nyama (carnivorous) na pia anakula matunda (frugvorus) kwa hiyo mnyama anayekula aina zote za vyakula anaitwa omnivorous, katika kundi hili yupo binadamu na nguruwe pekee. Kwa hiyo nadhani kutakuwa na mambo mengi tu yanayofanana.....
 
Back
Top Bottom