SoC02 Moyo wako; Siri ya mafanikio yako

SoC02 Moyo wako; Siri ya mafanikio yako

Stories of Change - 2022 Competition

Fannjosh

Member
Joined
May 28, 2016
Posts
35
Reaction score
46
Ni ukweli usiopingika kwamba kila mtu anatamani kufanikiwa katika maisha. Wapo wanaotamani kufanikiwa kifedha, kisiasa, kielimu, kijamii na hata kiafya.

Moja kati ya siri kubwa za mafanikio ni kusikiliza kile moyo wako unachohitaji. Wengi wamejuta kwenye maisha kwa kufanya mambo ambayo yalikuwa ni kinyume na sauti za mioyo yao.

Utakiri kwamba, kuna wakati uliponea chupu chupu dhidi ya hatari fulani, na kikubwa ni kwasababu ulisikiliza sauti ya moyo wako.

Mabilionea wengi wamefanikiwa si kwasababu walikuwa na connection za watu ila ni kwasababu walifanyia kazi ndoto za mioyo yao.

USHAHURI
  • Kuna wakati unajaribu kutafuta ajira kwenye taasisi kubwa ili upate pesa lakini kila unapojaribu unakwama, hiyo ni kwasababu Mungu anahitaji ufanyie kazi malengo yako yaliyo ndani ya moyo wako. Sikiliza moyo wako na anza kufanyia kazi ndoto zako.
  • Kuna wakati unafanya biashara lakini inakufa, sikiliza moyo wako, anza kufanyia kazi malengo yako.
  • Kuna wakati unatafuta kazi maeneo tofauti tofauti lakini unafukuzwa unarudi mtaani bila hata sababu, sikiliza moyo wako, fanyia kazi ndoto zako.
  • Usiulize kwa watu kuhusu biashara inayolipa kwa wakati huo, sikiliza moyo wako, fanyia kazi ndoto zako.

MUHIMU: Sikiliza moyo wako, anza sasahivi kufanyia kazi malengo ya moyo wako. Acha kupoteza muda kwenye mambo unayohisi yatakupa mafanikio, badala yake jikite zaidi katika ndoto za moyo wako. Inaweza ikawa ngumu kuanza, ndugu na marafiki wasikuelewe ukabaki mwenyewe, lakini kikubwa, fanyia kazi ndoto zako.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom