moyo wangu una huzuni kiasi cha kufa

Ohhhh real sad
Tunamuombea sana na tunaamini Mwenyezi Mungu atakuwa nae kumpa uponyaji
Mpe pole sana sana
 
Pole sana Smile.....
usijali mama atapona.....
Tunamuombea na nina hakika Mwenyezi Mungu atasikia sala zetu......
 
Ok unajua nilikuwa sijaona hayo maandishi mengine siunajua hv vimeo vingine baba!
Mpe pole sana bana,
Hakika mungu wetu ni mwema natamsaidia atapona haraka iwezekanavo!!!!
 
Pole sana jamani,lakini usisahau Mungu wetu ni mponyaji hivyo tuzidi kumuomba na kumuamini,usipoteze imani,hakuna neno gumu kwa Mungu,
 
Pole Smiley!
Mwenyenzi Mungu amjalie uzima na afya njema.
 
Pole smile kwa wakati huu mgumu kwako kaza moyo mungu atamjalia apone
 
Tunakuomba ewe Baba Mwenyezi unyooshe mkono wako umponye huyo Mama anayeumwa apate kupona na kuwa mzima kabisa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti unayeishi na kutawala milele na milele pokea uzima Mama sasa katika jina la Yesu Kristo, nguvu zote za wachawi, wanga, mapepo, majini nazivunja na kuziamuru zitoke na kurudi zilikotoka kwa jina la Yesu Kristo, asante Yesu kwa kuwa hakuna linaloshindikana kwako, ni katika jina la Yesu Kristo ninaomba na kushukuru, Amen.
 
Pole sana dada.Tuko pamoja katika kumtakia nafuu na afya njema.Mungu jaalia.
 
Very sad. Mwenyezi mungu amjaaliye apate nafuu haraka. Maradhi ampe paka mweusi. AMIN.
 
ubarikiwe mpendwa
 
Pole sana Smile, Mungu ni mwema, mama atapona. Huu ni muda wako wa kumuombea sana, usiruhusu kukata tamaa. I promise to pray for her.
 
asanteni jamani hadi nimechoka
 
pole mkuu,usilalamike sana,kuwa na imani mungu atamponyesha..sema amen.
 
Pole sana smile, usife moyo, amini Mungu ni mwema na yuko upande wako. Kuugua sio kufa hivyo amini kuwa mama atapona! Tunamwombea apone upesi!
 
..pole sana mkuu!..get well soon our dearest mom!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…