Moyo wangu unavuja damu

Moyo wangu unavuja damu

Kanashimi

Member
Joined
Apr 10, 2024
Posts
10
Reaction score
27
Habari zenu wana Jamii Forum… Natumaini sote tumesherehekea Eid vizuri wale Eid iliyokuwa mbaya kama mimi nawapa pole tupo pamoja Mimi ni member wa muda mrefu ila imebidi nije na ID mpya kutokana na haya yanayonisibu….. Nitajaribu kuelezea kwa ufupi sana kadri nitakavyojaaliwa…

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 31 ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto wa3 wote tukiwa ni wa kike kwa bahati mbaya wazazi wangu walitengana miaka mingi sana iliyopita sisi tukiwa wadogo… Kwa miaka yote hiyo tumekuwa tukilelewa na mama ambaye yeye ndiyo sababu ya mimi kuandika uzi huu

Mama yangu amekuwa akitulea kwa mapenzi makubwa mno na alipambana kuhakikisha sote tumesoma vizuri na kupata mahitaji ya msingi Alhamdulilah.

Baada ya kumaliza degree yangu ya kwanza Mungu alinisaidia nikapata kazi nzuri na nashukuru nimeweza kuisupport familia yangu kwa kipindi chote hiki

Miaka kadhaa nyuma nilianza kuona mabadiliko kwa mamangu na kwa kuwa ni mtu ambaye nampenda sana hata kitu kidogo tu kikiwa hakipo sawa nakuwa wakwanza kugundua tofauti na ndugu zangu.

Mama yangu ni mwanamke mrembo sana ambaye ni mchanganyiko wa Mtanzania na Mgiriki hivyo ni mtu aliyekuwa na muonekano wa kuvutia sana nakumbuka katika miaka yangu yote ya kusoma akiwa anakuja shule marafiki na walimu walikuwa wanabisha kuwa ni mama yangu na wengi walidhani ni dada yangu wa kwanza kutokana na muonekano na namna anavyojipenda.

Tuendelee mama alianza kubadilika na taratibu urembo wake ukaanza kupotea akawa hana raha, afya ikaanza kuyumba na kuna muda inakaa sawa nikawa naongea nae kumuuliza ana shida gani tofauti na Pressure inayomsumbua lakini akawa anadai yupo sawa basi siku zinazidi kwenda… 2021 akawa anashambuliwa na maradhi mara kwa mara anaenda hospital anakuwa poa kusema kweli nilianza kuwa na hofu kubwa juu yake… lakini siku zikawa zinakimbia

Moyoni mwangu kuna sauti ilikuwa inaniambia kuna kitu kikubwa hakipo sawa nilichokuwa nafanya kila nikisali nilikuwa namuomba Mungu amrejeshee furaha mama yangu

To cut a story short mwaka huu mwanzoni mwa mwezi wa tatu nilisafiri kwa majukumu ya kikazi na nikiwa huko wadogo zangu walinipigia wakanambia mama amepata typhoid kali sana na yupo kwenye dawa ila nisiwe na hofu… ila niliporudi Mungu wangu mama yangu alikuwa ameisha nyie nilipomuona sikuweza kuzuia machozi yangu nikawauliza wadogo zangu imekuwaje hii hali wakanambia amekuwa mvivu wa kula.

Ikabidi siku iliyofuata nimpeleke hospital mimi na last born wetu nilivyofika nikaingia kwa doctor na dozi alizopewa za Typhod nikaomba amfanyie mama vipimo vyote ili nijue shida nini… majibu yakatoka doctor akanambia nani anaishi nae nikamwambia ni mimi na ndugu zangu akanihoji maswali kadhaa na mwishowe akaniambia MAMA YAKO NI HIV POSITIVE kwa mujibu wa vipimo. Naomba nikiri sijawahi kusikia maumivu kama niliyosikia ile siku niliona kama dunia imenielemea nyie mama yangu kipenzi changu

Nilisali pale Mungu anipe uvumilivu nisionyeshe mabadiliko yoyote kwa mama na ndugu yangu maana walikuwa nje na Doctor alinishauri nisimwambie yeyote hata ndugu zangu ila nimkazanie ale kisha nitafute hospital ya wilaya aanze CLINIC…. nilipotoka wote wakaniuliza umeambiwaje kwa ujasiri nikajibu ni Typhod inabidi umalize dozi

Nikiri hakuna siku nililia kama ile maana tuliporudi home niliwaaga wadogo zangu nikatoka mara moja nikatafuta mahali nikalia sana ndugu zangu naomba niwaambie nimekata tamaa nawaza nitaanzaje kumwambia mama hali yake moyo wangu umejaa maumivu makali sana.

Niliwashawishi wadogo zangu wasafiri for eid ili mimi nibaki na mgonjwa niongee nae wameondoka tangu jana lakini mpaka ninavyoandika hapa sijaweza kumwambia chochote…. kila nikikaa ni machozi tu yanatoka na ameanza kunotice ananiuliza mbona huna raha.

Ndugu zangu wana jamii forum naombeni mchango wa mawazo hili jambo ni zito nashindwa kulibeba na nimeona nikiandika huku huwenda nitakuwa nimetua mzigo natanguliza shukran.
 
Habari zenu wana Jamii Forum… Natumaini sote tumesherehekea Eid vizuri wale Eid iliyokuwa mbaya kama mimi nawapa pole tupo pamoja Mimi ni member wa muda mrefu ila imebidi nije na ID mpya kutokana na haya yanayonisibu….. Nitajaribu kuelezea kwa ufupi sana kadri nitakavyojaaliwa…

Ndugu zangu wana jamii forum naombeni mchango wa mawazo hili jambo ni zito nashindwa kulibeba na nimeona nikiandika huku huwenda nitakuwa nimetua mzigo natanguliza shukran.
Umejipa kazi sio yako,
Aende hospital na huko hospital watampima na wataongea nae na kumjulisha majibu na kumuanzishia dawa
 
Pole sana dada yangu, pole kwako na mama na ndugu zako.
Ila mbona Hiv sio shida kubwa nyakati zetu kiasi cha kufanya iwe hivyo ulivyo eleza.
Sijaona sehemu umesema mmeenda kupima mara ya pili na ya tatu.

Lakini pia hilo swala la taarifa halikupasi wewe bali daktari na wataalamu husika.

Daw za kutuliza makali zipo na maisha yanaendelea kama kawaida, ingekua miaka ile ya 90 kuja 2000 hapo walao, lakini leo Hiv imekua kawaida mnoo.
 
Habari zenu wana Jamii Forum… Natumaini sote tumesherehekea Eid vizuri wale Eid iliyokuwa mbaya kama mimi nawapa pole tupo pamoja Mimi ni member wa muda mrefu ila imebidi nije na ID mpya kutokana na haya yanayonisibu….. ona nikiandika huku huwenda nitakuwa nimetua mzigo natanguliza shukran.
Pole, jikaze umwambie, wewe ni mtoto wa kwanza na sifa ya watoto wa kwanza ni ujasiri na upendo.
Ukishindwa mualike huyo daktari nyumbani alafu atasema na mama akiwa nyumbani na atakua Sawa.
 
Usimwambie wewe mama tatizo lake kwa jinsi navyojua asili ya akili ama ubongo wetu. Uko Kama radi na sijui umesema anayo presha.

Pole sana my dear hii Ni asili usipingane nayo utaumia wewe zaidi. Ikubali na elewa kwa kila kitu lipo under the control of universe. Accept it maisha haya tunapita sema tu Raha za dunia ni za muda Tu. Kikubwa aambiwe na watalaamu Ila sio wewe.

Hao ndugu zako wasijue ama na wao wanajua Ila hawataki kukuambia pia. Komaa ivyo ivyo angalia usimwambie rafiki yako wa karibu naye atamwambia mwenzake wa karibu na chain itaendelea
 
Wazazi wengi wenye HIV huwa hawapendi watoto wao wajue mapema huwa wanatunza siri had mambo yakienda vibaya, sasa kuwa makini hizo taarifa dokta ndo alitakiwa amueleze mama yako taarifa ukimpa wewe moja kwa moja huenda akaumia mara mbili japo sidhani kama kweli mama yako hajui kama ana Hiv
 
Ndugu zangu wana jamii forum naombeni mchango wa mawazo hili jambo ni zito nashindwa kulibeba na nimeona nikiandika huku huwenda nitakuwa nimetua mzigo natanguliza shukran.
Pole sana dada.
Allah atawapa nguvu na ujasiri wa kulikabili hili.

Mimi kwa umri ni kaka yako, kwa miaka 5 zaidi. Najitolea, kuwa mfariji wako na unitambulishe kwa mama kama rafiki yako wa muda tu nilikua mkoani nikiishi huko.
Tuongee na mama pole pole na kwa kipawa nilichojaaliwa na Allah tutafanikisha kumueleza mama hali yake. Nna imani ataipokea. Ntakuja na daktari, tutashauri kitu na hali ataipokea mwenyewe. We jifanye hujui kitu.
After all, maisha lazima yaendelee, no matter what. Ni jaribu tu hili. Litapita.
Karibu.
 
Umejipa kazi sio yako,
Aende hospital na huko hospital watampima na wataongea nae na kumjulisha majibu na kumuanzishia dawa
Unaweza kuwa sahihi ila kutokana na hali aliyokuwa nayo Doctor alinambia akikaa sawa niweza kumwambia maana mm ndo naishi nae na mama hana mtu mwingine wa karibu ila mimi na wadogo zangu… ni miaka mingi sijawahi kumuona japo na rafiki
 
Pole sana dada yangu, pole kwako na mama na ndugu zako.
Ila mbona Hiv sio shida kubwa nyakati zetu kiasi cha kufanya iwe hivyo ulivyo eleza.
Sijaona sehemu umesema mmeenda kupima mara ya pili na ya tatu.

Lakini pia hilo swala la taarifa halikupasi wewe bali daktari na wataalamu husika.

Daw za kutuliza makali zipo na maisha yanaendelea kama kawaida, ingekua miaka ile ya 90 kuja 2000 hapo walao, lakini leo Hiv imekua kawaida mnoo.
Asante sana ndugu barikiwa
 
Ukimwi sio mwisho wa maisha dear, msaidie mama aishi vizuri, mtie moyo usimuoneshe kuumia ye ataumia zaidi mpe moyo aone ni kawaida kikubwa azingatie dose ale vizuri


mtunzie siri yake pia
Asante kwa ushauri nitafanya hivyo nitajitahidi sana nimejiahidi sitawaambia hata hao wadogo zangu
 
Back
Top Bottom