Moyo wangu unavuja damu

Kanashimi I assure you, HIV is No longer an issue to worry to that extent.
Nimehudumia wateja wa HIV for about 8 yrs now.

Ninachokijua akilini mwako umejawa simanzi zito ukiwaza kwamba unaenda kumpoteza mama hivi karibuni. Lakini nakuhakikishia haotokuwa hivyo unavyowaza endapo mama ataanza Clinic haraka na kutumia dawa kwa ufuasi mzuri kabla hajaendelea kuadvance kwenye AIDS.

Kuna ndugu zetu hapo juu wamejitolea kukusaidia katika hili, jaribu kuwapa nafasi na ikitokea unahitaji msaada zaidi nitaku Link na Nurse mmoja ambaye ni Mmama wa 53 yrs ameishi na HIV for over 15 yrs na yuko Healthy kuzidi hata wasio na HIV atamsaidia kwa mambo kadhaa freely na vile ni Mmama mwenzie itafit zaidi.
 



Pole Sana.

Magonjwa Kama UKIMWI ni ugonjwa ambao unaweza kuishi nao na maisha yakaenda vizuri tu.

unapokuwa unamuuguza mgonjwa haijalishi yupo hatua gani Ila hakikisha unakuwa optimistic -yaani make sure mgonjwa asi-notice sura ya uzuni kwako wewe unayeuguza ,then hakikisha unongea maneno ya USHINDI 24/7 mbele ya mgonjwa.


Mama yako mpatie matibabu ktk haya maeneo.

@ psychological (therapy)
@ Huduma bora za Afya ya mwili
@ spiritual - mfanye awe connected with divine power.

tatizo lolote linaweza kuwa kubwa au Dogo kutokana na vile umelitafsiri.

so hilo sio tatizo .

Jitahidi -ufanye gratitude -penda kumshukuru MUNGU kwa kila jambo linalotokea ktk maisha yako.

Nakuombea na naimani mama atakuwa bora Sana.🙏🏽⭐🌙
 
Dada chukuliwa easy tu.. mtu akiwa positive sio mwisho wa maisha yake mi nimezaa watoto wawili na mwanamke ambaye yuko positive japo tumetengana ila watoto wote wapo negative na mimi pia nipo negai na afya ya huyo bi shosti ipo njema na fresh kabisa... Kuzingatia dawa na vyakula tu atakaa na afya njema na ataishi hadi wajukuu wafike vyuo au waolewe na kuoa
 
Ukiusoma kwa makini uzi wako ni kama mama yako anaijua hali yake, isipokuwa ni ama ameamua kuishi hivyo hivyo bila kutumia ARV...

Ongea na daktari aliyekupa habari za hali ya mama yako, afanye kama anamuita kutaka kujua maendeleo yake, then akiwa huko amchane hali yake ya afya...
 
Unachokisema kinaweza kuwa sahihi niliwaza hivyo pia naona anahisi tutaumia sana esp mimi pengine aliamuua akae zake kimya.
 
Karne ya 21 unaanzaje kuuona ukimwi ni ugonjwa wa ajabu hadi unakaa unalialia.hayo ni mawazo ya miaka ya 90.In short hilo sio tatizo bali wewe ndo unalifanya tatizo kwa kuendekeza hisia uchwara badala ya akili na huko shule ni dhahiri hukwenda kupata elimu bali ulikwenda kusomea kazi. Mgonjwa ukimpeleka hospitali na akafata utaratibu wa kidakitari anaendelea na maisha kama kawaida na mwili wake unarudi.
 
Pole sana ndugu na pia hongera kwa kupata ujasiri wa kushare,

Kwa hali aliyonayo mama yako haitakiwi kukutoa kwenye mstari ukizingatia sasa hivi kuna dawa akitumia kwa ufasaha (good adeherence) atakuwa vizuri tu ndani ya muda mfupi na hakuna gharama zozote katika clinic zote (CTC) za HIV, na kuna privacy ni yeye tu kumuweka wazi ili ajue hali aanze dawa.

Jitahidi umuambie mapema na ikiwezekana nenda nae kwa counselor kama wewe unawasiwasi ili aweze kumhandle vzuri for pre and post counseling.
 
Mmmmmh aiseee...
Takbir....
 
Kanashimi

Sijui ni kwa Nini Daktari alikueleza wewe hizo habari badala ya mama.

Ninavyojua utaratibu mgonjwa ndio anatakiwa kuwa mtu wa kwanza kujua afya yake isipokuwa kama ana hali mbaya sana.
Yeye ndio ataamua kuwajulisha wengine.

Kwa kuwa imeshatokea mimi Nakushauri, usimwambie.
Mchukue mpeleke hospitali, Mueleze Mtoa huduma, amupime then ikithibitika anao yeye ndio amueleze.

DR Mambo Jambo unasemaje.
 
Nika zani cancer kumbe ukimwi..ondoa shaka na mzingatie ushauri wa madaktari ataishi mda mrefu pasipo gharama.
 
mdada nazani hiyo kazi ya kushauri siyo yako ila wewe ni muhudumiaji kulingana na maelekezo ya dokta sasa chakufanya nenda hospitali ongea na mtoa ushauri nasaa/psychologist ambae atakaeweza kumshauria atumie dawa na pili akukutanishe wewe na mama yako ili ajaribu kuweka jambo hilo huwenda mama yako anahofu juu yenu kuwa mkijua hana pa kuweka uso wake ila kama dokta akifanya inshu ya kuwaonganisha wewe na mama yko kwamba mama yako ajue kwamba kuna mwanawe mkubwa anajua siri yake ila anaitunza atakuwa hana hofu na atakuwa katika hali normal.

usimwambie chochote na jikaze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…