Mozambique na Zambia wataka kuuza dhahabu yao Kenya

Mozambique na Zambia wataka kuuza dhahabu yao Kenya

REDEEMER.

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2015
Posts
8,925
Reaction score
14,890
EFDDqRdXoAA_36J.jpeg
EE-eYQhX4AULwsP.jpeg
EE-eaebXsAA9UAz.jpeg
EFJ5f6nWwAAV-ib.jpeg
EFJ5f18XYAAFJsL.jpeg
#1
MAFANIKIO ya haraka ya Soko Kuu la Kimataifa la Dhahabu Geita ambalo ni la mfano katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, yamezivutia nchi za nje ambazo tayari zimeomba kulitumia soko hilo kuuza dhahabu yake. Hali hiyo imetajwa kuchangiwa na nidhamu ya Watanzania katika kusimamia ununuzi na uuzaji dhahabu na hivyo kuziba mianya ya wizi na utapeli katika biashara ya dhahabu.

“Serikali inastahili kuungwa mkono kwa kuanzisha soko la uhakika wa dhahabu. Hakika limeleta matokeo chanya... ni jambo la kujivunia, ndiyo maana nchi kama Msumbiji na Zambia zimeomba kuja kuuza dhahabu yake hapa Geita” alisema Waziri wa Nishati, Dotto Biteko (pichani) mwishoni mwa wiki wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mjini hapa.

Kwa mujibu wa Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Bukombe mkoani Geita, kabla ya kufunguliwa kwa masoko ya madini nchini, makusanyo ya dhahabu yalikuwa kilo 101 kwa mwezi, lakini baada ya masoko kufunguliwa makusanyo yameongezeka na kufikia kilo 1,974.

Na kutokana na imani ya wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, Biteko alisema watu waruhusiwe kuleta madini katika masoko rasmi ya ndani. Alisisitiza kuwa, wasibughudhiwe kama inavyoripotiwa katika baadhi ya maeneo kwa wachimbaji wadogo kusumbuliwa wakitakiwa kuonesha vitalu vyao. “Kama wanaleta madini katika masoko yetu rasmi, msiwasumbue hata chembe.

Na hata kama inatoka nje acha iingie sokoni kwa sababu ni sisi ndio ndio tutakaonufaika. Lakini kama wanatorosha madini kwenda kuuza nje, hao wabanwe...,” alisema. Wataka Benki Kuu Awali, Mbunge wa Geita Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu alielezea kufurahishwa na mafanikio ya haraka ya soko hilo, akisema siku si nyingi, Geita itahitaji kuwa na Kituo cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na kuimarika kwa mzunguko wa fedha. “Tunaishukuru serikali kwa kuelekeza nguvu katika sekta hii ya madini. Sisi wa Geita tumeanza kuona thamani ya madini yetu... Mji wetu huu una matumizi makubwa sana ya pesa kutokana na ongezeko la mauzo ya dhahabu.

Nadhani wakati umefika tupatiwe Kituo cha Benki Kuu. “Jana (juzi) tukiwa Chato, watu wa benki wale wanunuzi wa pamba walisema kuna tatizo la pesa. Mimi nalijua kwa muda mrefu, benki hizi nyingi zinapoagiza kutoka Mwanza (Tawi la Benki Kuu ya Tanzania) inachukua zaidi ya siku mbili kupata pesa. Tunaomba tupate kituo cha Benki Kuu kama ilivyo Shinyanga (Kahama) ili kurahisisha matumizi ya pesa katika mji huu. “Lakini pia kutokana na kustawi kwa mji huu, tumewasilisha mezani kwako ombi la kuwa Manispaa,” alisema.



Takwimu zinaonesha kuwa, kipindi cha kuanzia Machi, mwaka huu hadi Septemba 7, mwaka huu, jumla ya kilo 1,573 zenye thamani ya takribani Sh bilioni 145.46 zilizalishwa na kuuzwa katika soko la Madini Mkoani Geita. Kupitia mauzo hayo, Serikali ilikusanya Sh bilioni 10.18. Hii ina maana kwamba, soko la mkoa wa Geita ndilo linaloongoza katika uzalishaji wa madini ya dhahabu na kuchangia wastani wa asilimia 43.1 ya dhahabu yote iliyouzwa kwenye masoko ya nchini.

Aidha, kuimarika kwa hali ya soko la dhahabu kunatoa taswira kwamba, mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa nao unakwenda kuimarika, kama lilivyo lengo la serikali la kutaka kuona ifikapo mwaka 2015, sekta hiyo iwe inachangia asilimia 10 katika pato la taifa. Mchango wa sekta ya madini kwa sasa ni asilimia 5.1 kwa takwimu za hadi mwaka 2018, ikilinganishwa na asilimia 4.4 mwaka 2017. Aidha, makusanyo ya maduhuli kwa mwaka 2018/2019 yalifikia Sh bilioni 335.18 ikilinganishwa na Sh bilioni 301.29 kwa mwaka 2017/2018. Kati ya Julai na Agosti, 2019 tayari kiasi cha Sh bilioni 74.43 zimekusanywa sawa na asilimia 15.82 ya lengo la kukusanya Sh bilioni 470.35 kwa mwaka 2019/2020.

mwaka 2017 kwa mwaka mzima dhahabu uliyopatikana kutoka kwa wachimbaji wadogo ilikuwa kilo 1,000, mwaka 2018 ikapanda hadi kilo 1,400 lakini sasa, ndani ya miezi minane tayari kilo 1,900 zimepatikana,” alisema Mkuu huyo wa mkoa anayesisitiza kuwa, dhahabu inakuja kuikomboa Geita na nchi kiuchumi kutokana na ukweli kwamba, asilimia 70 ya dhahabu yote nchini inapatikana Geita. Kwa mujibu wa Gabriel, kilo moja ya dhahabu katika soko la dunia kwa sasa ni wastani wa Sh milioni 100.
 
Jamaa zetu walipiga dhahabu ya mfalme, wote wapigaji wakurugenzi wa chama tawala na upinzani, Kenya ni failed state ndo maana vita za wenyewe haziishi sababu vigogo wao wana bulk money za kutunishiana misuli
 
Dhahabu inataka kuuzwa Kenya, ila maelezo ya ndani ni mauzo yanafanyika Tanzania Geita...

Mleta mada haupo serious...


Cc: mahondaw
 
Dhahabu inataka kuuzwa Kenya, ila maelezo ya ndani ni mauzo yanafanyika Tanzania Geita...

Mleta mada haupo serious...


Cc: mahondaw
We mgeni kwenye ili jukwaa rudi kwenye majukwaa uliyo zoea sisi wazoefu tunasema ajakosea ndiyo maana unaona wakenya wenyewe wapo kimya
 
Back
Top Bottom