Mpaka Kieleweke Si Mbowe

Mpaka Kieleweke Si Mbowe

Status
Not open for further replies.
2006, 11:29 PM
Freeman A. Mbowe
user_offline.gif

Freeman A. Mbowe has no status.
Junior Member
Join Date: Sat Dec 2006
Posts: 2
Rep Power: 0
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_pos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif
reputation_highpos.gif

Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Credits: 309

icon1.gif
The Only Thing We Have To Fear ...
Salaam Wana Jambo.

Kwanza kabisa naomba niwapongeze wale walioanzisha forum hii kama sehemu ya matumizi ya uhuru wao binafsi. Aidha, niwapongeze kwani forum hii ni sehemu ya harakati muhimu ya kujadili mustakabali wa nchi yetu.

Nimesoma maoni, pongezi, malalamiko, hofu, ushauri na mambo mengine kadhaa katika forum hii. Nimejadiliwa mara kadhaa katika hoja tofauti. Nawapongeza wote waliochangia mada zilizonihusu hata kama wamenipinga au kuzusha. Nitoe pongezi zaidi kwa wale walioonyesha kuipenda nchi yetu na kuitakia mema kwa mijadala mbalimbali.

Leo naandika kwenye forum hii kwa mara ya kwanza. Siyo kusudio langu kujibu hoja zinazonihusu moja kwa moja. Aidha, siyo nia yangu kuingia kwenye malumbano ya aina yeyote na wachangiaji. Naheshimu sana uhuru na mawazo ya wote hata kama kwa makusudi au bahati mbaya yanapotosha. Binadamu tunatofautiana katika fikra, uelewa na malengo.

Siasa na uongozi wa Taifa letu vina mahusiano ya moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku.Tanzania ni nchi yetu sote. Hatuna sababu ya kufanya masihara na siasa wala viongozi wetu wote. Walio madarakani na wale wenye nia hiyo.

Mara nyingi, binadamu ni wepesi wa kulaumu na kuhukumu. Tunapenda kadhalika, kudai haki pengine bila kutafakari kwa kina tumetekeleza wajibu wetu kwa kiasi gani.

Tupende tusipende, Tanzania ina kilio. Wote tusipojiuliza na kutekeleza wajibu wetu, kila mtu na nafasi yake kukabiliana na msiba huu, kamwe kilio hakitaisha. Muda wetu wa kuishi maisha haya ni mfupi sana na kila mmoja wetu anastahili kujiuliza amechangia nini katika wajibu wa kumaliza msiba huu?

Naamini, tatizo kubwa la kwanza la kukabiliana nalo nchini mwetu ni WOGA na HOFU. Naamini Wana Jambo forum wengi ni watu wenye uelewa wa kutosha. Kwa nchi yetu iliyo hoi kielimu na hata kiuwezo, hawa ni watu wa "kutumainiwa" na familia zao na hivyo nchi yao kwani familia ni sehemu ya nchi. Napenda kuamini ni sehemu ya "cream" ya Taifa letu nanyi kwa kutoa mawazo yenu, mmekuwa sehemu ya harakati.

Nasikitika, wengi wa wana forum wanatumia majina yasiyo ya kweli. Sina hakika kama siyo ishara ya woga! Na kama wasomi, waelewa, wenye upeo wanakuwa hivyo, Watanzania wa kawaida wategemewe wawe vipi? "Authenticity" ya tunayoyaandika inafifishwa na hali hii?

CHANGAMOTO: KWA KUFICHA MAJINA YETU UJASIRI WETU WA KUHOJI, KULAUMU NA KUHUKUMU UNAPINGANA NA DHAMIRA YA HARAKATI? HARAKATI NA WOGA VINAENDANA? WOGA UNAWEZA KUOKOA TAIFA?

By concealing our identity, are we truly living to our motto which says "Where we dare talk openly?"

"The only thing we have to fear is fear itself" - President Franklin Delano Roosevelt, Washington DC, 4th March 1953

Nawashukuru na naomba kutoa hoja!!

Freeman Mbowe
 
Huyo hapo juu ni MBOWE...Yuko hapa jf kama ilivyo kwa wengine!
Slaa yuko hapa so as Zitto...Swali...Kwanini MBOWE kuna watu wanaozungumza kwa niaba yake tuu!
 
Pamoja na kuwa kauli mbiu ya hamasa ya Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke ilibuniwa na Mwenyekiti Mbowe wakati wa kampeni, nataka kukanusha hapa kwamba mtu anayejiita Mpaka Kieleweke hapa Si Mbowe. Pamekuwa na jitahida sana za kumhusisha mwenyekiti wetu na Majina mawili hapa mtandanaoni, wakati Chinga alianzisha uzushi kwamba Mbowe ni Philimom Michael, Bwana FMES yeye ameanzisha Mpaka Kieleweke ni Mbowe. Nimekuwa nikifuatilia mienendo na michango ya watu hawa wawili na napenda niweke wazi kwamba hakuna Mbowe kati ya watu hao wawili.

Philemon Michaeil ni mwanahabari ambaye mpaka sasa yuko Dar es salaam.

Mpaka Kieleweke ni kada wa CHADEMA anayezunguka kati ya Dar es salaam na Dodoma.

Hata wakati ambapo mwenyekiti Mbowe akiwa nje ya nchi hawa mabwana wawili wameendelea kutoa michango yao kutoka Dar es salaam. Mathalani kwa sasa Mwenyekiti Mbowe yuko kikazi mashariki ya kati lakini bado mpaka kieleweke anaandikia michango yako toka Dodoma.

Kwa mchambuzi yoyote wa michango ya watu humu atagundua kuwa michango ya Mpaka Kieleweke haiendani kabisa na maoni na misimamo ya Bwana Mbowe katika masuala mbalimbali na kwa ujumla bwana Philemon Michael hana undani wa masuala ya kisiasa hususani yale yanayoihusu CHADEMA.

Nawakatia kheri

Asha

Asha
Ni muongo
Kwa maana mpaka kieleweke alisha sema yeye si Mbowe na akaongeza kua yeye anaishi nchi zilizo endelea na ndio maana ana access ya mtandao na ndio maana hadi muda huo alikua ana peruzi mtandao.

Sasa haya madai ya kwamba anafanya Dar es salaam DODOMA ni uongo mkubwa kwani TZ si nchi iliyoendelea na ni nchi masikini duniani.
 
Huyo hapo juu ni MBOWE...Yuko hapa jf kama ilivyo kwa wengine!
Slaa yuko hapa so as Zitto...Swali...Kwanini MBOWE kuna watu wanaozungumza kwa niaba yake tuu!

He is too godly that some can't even see his blunders.
 
Asha
Ni muongo
Kwa maana mpaka kieleweke alisha sema yeye si Mbowe na akaongeza kua yeye anaishi nchi zilizo endelea na ndio maana ana access ya mtandao na ndio maana hadi muda huo alikua ana peruzi mtandao.

Sasa haya madai ya kwamba anafanya Dar es salaam DODOMA ni uongo mkubwa kwani TZ si nci iliyoendelea na ni nchi masikini duniani.

Kwa hiyo Mpaka Kieleweke aliyeko nje ya nchi kwenye hizo nchi zilizoendelea ndio kamwambia Da Asha kuwa yeye awaambie wana jf kuwa yuko Dar-Dodoma?
Duh!
 
Mushi1,'
Jasusi ni mimi, na si mwingine. Ila imeshabainika kuwa nina undugu na marehemu Ballali, hilo siwezi kulikwepa. Lakini bottom line ni kwamba tupo hapa kukata issues. Period. Tuachane na personalities, ingawa mara moja moja haziwezi kuepukikwa.

Ok Kwa hiyo unataka tuelewe kuwa wewe si Ballali bali ndugu yake Ballali....Ok sawa nakubali kwa sasa...Then...Tatizo liko HAPA...Kwamba Ballali ana IMMUNITY hapa JF licha ya kwamba yeye hata si member!
Sasa wewe uliyepewa IMMUNITY YA KUTUKANA NA KUTETEWA...Then unakuja unasema ingawa mara moja haiwezi kuepekukikwa...Mimi naona ni bora uweke ID ako wazi na isiwe mara moja tu kuhusu personalities...Iwe MARA ZOTE!
 
Kwa hiyo Mpaka Kieleweke aliyeko nje ya nchi kwenye hizo nchi zilizoendelea ndio kamwambia Da Asha kuwa yeye awaambie wana jf kuwa yuko Dar-Dodoma?
Duh!

Ndio
Hapo unajua mtu ukisema uongo lazima uu comand kwenye memory ili uwe unaurudia uongo huo huo.Ukijichanganya kidogo tu kwisha kazi
 
Asha
Ni muongo
Kwa maana mpaka kieleweke alisha sema yeye si Mbowe na akaongeza kua yeye anaishi nchi zilizo endelea na ndio maana ana access ya mtandao na ndio maana hadi muda huo alikua ana peruzi mtandao.

Sasa haya madai ya kwamba anafanya Dar es salaam DODOMA ni uongo mkubwa kwani TZ si nchi iliyoendelea na ni nchi masikini duniani.

hizi reasoning nyingine za ajabu... kama mtu hataki kujulikana aliko pia kinakushangaza kitu gani? Kuna vitu ambavyo "Mpaka Kieleweke" amekuwa akiviweka hapa au ana access navyo hapo nyumbani na amekuwa akiviweka hapa na kwa usalama wake yeye mwenyewe au sources zake hataki kuthibitisha wapi aliko au yeye ni nani.

Miye naona JF inakabiliwa na tishio la identity yake. Tunataka kuwatisha watu ambao ni kiungo kikubwa kati ya JF na ndani ya serikali. Tunapojaribu kutaka kuwafahamu watu walioko nyuma ya majina haya tunahatarisha the very spirit that created this forum. If we can not protect the sacrosanct idea of anonymity tunatengeneza the very recipe for the demise of this forum.

I beseech each one of you, humbly I do; tuache haya ya majina, ni mlango ambao hatutaki kuupita. Wakati wengine tunaweza tusipate matatizo sana lakini wengine imani ya watu na habari tunazotoa is based on this trust that people have in us kutupa information n.k

Yawezekana kuna faida fulani fulani ya kulaziimisha kumjua fulani, ila hasara yake ni kubwa kweli.

A friendly observation and petition.
 
MKJJ mimi naona hapa solution ni MATUSI NA KWENDA PERSONAL NA HARASSMENTS VIISHE!
IWE NI HOJA KWA HOJA!
Vipi tena kuhusu ule usemi wako wa Wakiishiwa na hoja....
 
Huyo hapo juu ni MBOWE...Yuko hapa jf kama ilivyo kwa wengine!
Slaa yuko hapa so as Zitto...Swali...Kwanini MBOWE kuna watu wanaozungumza kwa niaba yake tuu!

mbowe no coward mbowe si mpambanaji wa kweli, ndio maana akakimbia uwanja wa mapambano ati toka kujiunga katuma post mbili tena akaja na maneno yale yale ya kilaghai kama yeye anaweza nondo tungekuwa nae na kujibu kila nondo

mie nnaamini yupo kwa jina jengine japo alionesha kuwa yeye shujaaa atatumia jina lake, wapi ....

mbowe huna lolote zaidi ya kukitumia chadema kwa maslahi yako binafsi
 
MKJJ mimi naona hapa solution ni MATUSI NA KWENDA PERSONAL NA HARASSMENTS VIISHE!
IWE NI HOJA KWA HOJA!
Vipi tena kuhusu ule usemi wako wa Wakiishiwa na hoja....

solution hiyo wengine tunaishi kwayo, tunakebehiwa, tunaitwa majina, na kufanywa kila aina ya kituko guess what... hatubadili principle, hoja hujibiwa kwa hoja, period. Kumuita mtu mnafiki, mpumbavu, n.k ni kujaribu kulazimisha hoja na mtu kujifanya anajua sana matusi. Wengine tumetukanwa hadi matusi ya nguoni lakini kitu kimoja hatufanyi ni kurudisha matusi kwa matusi; si kwa sababu hatuyajui ni kwa sababu we'll not stoop that low..

Uchaguzi ni wako, unaweza kuendelea na mtindo wako au ukaamua kuraise up and meet the standard that most people adhere to hapa. Lolote utakalochagua you better be able to stand by it kwani watakuja watu kukusukuma sana and test your patience. Ukihimili watakuheshimu.
 
...Tunapojaribu kutaka kuwafahamu watu walioko nyuma ya majina haya tunahatarisha the very spirit that created this forum. If we can not protect the sacrosanct idea of anonymity tunatengeneza the very recipe for the demise of this forum.

Yawezekana kuna faida fulani fulani ya kulaziimisha kumjua fulani, ila hasara yake ni kubwa kweli.

A friendly observation and petition.

Na ndio maana nilishituka kusikia kuna pati/mkutano wa JF Columbus!

Na ndio maana I cringe nikiona message hapa zinasema "binti fulani nitakuja/tukutane Detroit unipikie Ugali."

Ya kujuana tuyaache kwenye PM.

A friendly observation and petition.
 
Ni vyema.

Ila hata ile thread yako ya UKABILA nilihimili.

Sasa mimi nachoongelea hapa tofauti.

Ni kwamba mimi sijali pressure..Nina himili kwasana tu!

Kwani nilishasema i didn't choose politics!

Nitapimwa kwa mchango wangu hapa jf na niko hapa kupambana na kwa hoja yeyote ile kwani mimi ni HONEST!

Na nilisharudia kauli yangu kama ulivyowahi kuniambia before..Kwamba kama wewe unajuwa hili...Na wengine wanajuwa lile.

Kama nyumba tunayojenga ni moja...Kugombea Fito hakuna maana!

Mimi sina sababu za kisiasa hapa...Mimi ni kama mwananchi wa kawaida..Mwananchi ambaye nime take my time na ku understand the whole issue na hata MOVIE NAWEZA DIRECT!

TENA YA KIMAFIOSO KAMA ZA WEST!

Kuna jamaa yangu bongo na yeye ana mawazo kama hayo na muda si mrefu kutatengenezwa MOVIE LOTE LA HAYA MASAHIBU!

Ikija kwenye issue ya ufisadi hapa jf..Kutokana na midataz iliyokwisha wekwa hapa na mimi kuipitia karibia yote pamoja na other sources of information...THE WHOLE SAGA NI KAMA ONE PAGE IN MY BRAIN!
 
Mzee...hapana yale yalikuwa ni ya KLH News.. na mashabiki wake, siyo JF nasikitika umejaribu kuiweka hivyo. Na hakukuwa mkutano nasikitika pia umechukulia hivyo. Sijaelewa kwanini?
 
Ni vyema.

Ila hata ile thread yako ya UKABILA nilihimili.

Sasa mimi nachoongelea hapa tofauti.

Ni kwamba mimi sijali pressure..Nina himili kwasana tu!

Kwani nilishasema i didn't choose politics!

Nitapimwa kwa mchango wangu hapa jf na niko hapa kupambana na kwa hoja yeyote ile kwani mimi ni HONEST!

Na nilisharudia kauli yangu kama ulivyowahi kuniambia before..Kwamba kama wewe unajuwa hili...Na wengine wanajuwa lile.

Kama nyumba tunayojenga ni moja...Kugombea Fito hakuna maana!

Mimi sina sababu za kisiasa hapa...Mimi ni kama mwananchi wa kawaida..Mwananchi ambaye nime take my time na ku understand the whole issue na hata MOVIE NAWEZA DIRECT!

TENA YA KIMAFIOSO KAMA ZA WEST!

Kuna jamaa yangu bongo na yeye ana mawazo kama hayo na muda si mrefu kutatengenezwa MOVIE LOTE LA HAYA MASAHIBU!

Ikija kwenye issue ya ufisadi hapa jf..Kutokana na midataz iliyokwisha wekwa hapa na mimi kuipitia karibia yote pamoja na other sources of information...THE WHOLE SAGA NI KAMA ONE PAGE IN MY BRAIN!

Jmushi... I'm sorry to disappoint you.. everything I write or written by other people is not about you.. some are general observations kwa ujumla tu. You can do whatever you have been doing, there is only one sun in our solar system.
 
One SUN shining on THE PEOPLE and ONE GOD WHO BLESSED THEM PROTECTS THEM AS WELL!

Talking about dissapointment?

That you had me banned simply by calling jk mafia?

Expressed and extended the apology to the whole forum.

Ok then..Pointi hapa ni watu waachiwe wakate issue na hoja ipingwe kwa hoja!

Na kama kuna URONGO..Pia upingwe kwa UKWELI.
 
ok carry on friend.
 
Mambo mengine jamani hayastahili kujadiliwa kwenye ukumbi wa heshima kama huu; kama ni hivyo basi tujadili na hili hapa.

Kichuguu ni Lowassa, tangu amefukuzwa uwaziri mkuu amekuwa kimya sana siku hiz huku akijitokeza mara moja moja tu.

Haya mjadala open.
 
Asha unasema eti mimi nimeanzisha kuwa Mpaka Kieleweke ni Mbowe? Vipi ukitoa ushaidi mkuu ili nikubali kukosolewa,

Ninasubiri ushahidi wa mimi FMES, kuanzisha kuwa Mpaka Kieleweke ni Mbowe, ukiuonyesha mkuu nitakubali kosa, ila kama huna ushahidi naomba useme wazi kuwa huna na ningewaomba Mods wakushughulikie kwenye hili iwapo huna ushahidi na ukiwa nao naomba Mods pia wanishughulikie ipasavyo, maana si unajua mimi ni jina moja hapa na siku zote huwa niko responsible na kila ninalosema, sijawahi kukimbia kivuli changu au maneno yangu!

Otherwise, sisi wote hapa ni watu wazima kama Mpaka Kieleweke sio Mbowe, hivi ni kweli wewe Asha ndiye uliyepaswa kumuongelea? Yaani yule mtu mzima hawezi kusema mwenyewe? Halafu mbona ni wengi hapa JF waliowahi kusingiziwa majina na mimi nikiwa mmoja wapo mbona hukujitokeza kutetea, WHy huyu Mpaka Kieleweke?

Mkuu hivi kweli nia na madhumuni yako on this topic hasa ilikuwa ni nini, kutuambia au kutotuambia? Maana mkuu sio siri kuwa nimeshitushwa mpaka kwenye mifupa knowing aliyeko nyuma ya hili jina la Asha, lakini nasubiri ushahidi mkuu! Ili baadaye nikuonyeshe jinsi Chinga alivyoitwa godoro la muungwana, jinsi Chinga alivyoitwa kifaa cha muungwana, aliponitumia huu ujumbe niliwamuambia kuwa mezea tu kuna siku yatageuka haya!

Ama kweli, mkuki kwa kondoo!

Kuhamanika kwako ni ishara kwamba ujumbe umefika. Msumari unachoma kote kote kwa kweli

Hebu kumbuka mjadala wa Chacha Wangwe kusimamishwa! Ni wewe uliyeanza kusema unajua nani yuko nyuma ya jina la Mpaka Kieleweke. Halafu wenzio wakadakia kusema ni Mbowe. Wala hukukanusha badala yake ukatoa hitimisho kwa kumwambia kwamba njia aliyotumia kueleza ukweli kuhusu Chacha si nzuri na ukamwambia anyamaze au atafute wengine waseme kwa niaba. Baada ya hapo wengi zaidi wakadakia huu uzushi ikiwemo Jmushi. Hakuna aliyekemea hali hii. Leo hapa nashangaa kila mmoja amekuwa mkemeaji! Hamkuyaona wakati huo? Au mmeona sasa yatavuka mipaka?

Double standard! Wakati bwana mmoja humu alianza uzushi wake kwamba mimi ni Kitila Mkumbo wengi mlikuwa mkitazama tu mpaka pale ilibothibitika kwamba bwana yule alikuwa mwongo na mzandiki. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa hali hii ni muhimu ikakemewa mapema. Nimeamua kuonyesha mfano tu.

Halafu unaanza tabia yako ya kunitisha kuwa unajijua kuliko ninavyojijua, unamjua Asha wewe? Hebu sema hizo pumba zako hapa,mod mruhusuni huyu Bwana amwage hizo pumba zake hapa ili pumba zijulikane pamoja na kuwa rules zetu zinakataza kusema hebu mruhusuni japo kidogo maana amezidi kile siku 'nakujua asha nakujua asha' unatadhani alileta posa kwetu!

Kama nimekukura sana hamishia vitisho na matusi yako kwenye http://ashawazenj.blogspot.com. Hapa ni ukumbi wa wastaarabu bwana, nawaheshimu sana hapa. Nikianza kufungulia mipasho hapatashikika!

Asha

BTW: Kichunguu, umenirejesha kwenye furaha eti wewe ni Lowassa! Baada ya kutoka ofisi ya Waziri Mkuu access ya mtandao wa bure imepungua nini?
 
Kama mtu hujitetei mwenyewe wala kukanusha huo ni uamuzi lakini kila mtu anajitetea mwenyewe. Hata hivyo suala la kanuni ni lazima wote tulitetee. Mpaka Kieleweke alikuwa na uwezo wa kupuuzia hoja hizo au kusema mara moja kuwa yeye si fulani. Tatizo ni kuwa nani ataamini unless ajisema yeye ni nani? ndio maana kwangu mimi binafsi sioni sababu ya kwanini watu wanatafutana na kusema wanafahamiana na kujuana n.k Kama unataka kumjua mtu badilishana naye namba, zungumzeni, fahamianeni, lakini haya ya kushukiana na kuhisiana wala hatuendi mbali.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom