Mpaka Kieleweke Si Mbowe

Mpaka Kieleweke Si Mbowe

Status
Not open for further replies.
FIKRA ushahidi wa haya umetoa wapi..weka japo source....kupunguza spceculations..
 
Ila ukiunganisha dots unaweza kushtuka kwamba nani ni nani hasa kama upo hapa kwa ajili hiyo, mfano kwa hayo maneno yako mama hapo juu nimehisi wewe ndiye MZEE MWANAKIJIJI

Tehe tehe ndugu yangu Jongomero yaani humu ndani unaweza ukahisi watu wengi sana!!! tehe tehe!!!
Kataishu tu mzee kuna watu wana hoja zinafanana humu kama mikate ya Azam
 
Haya bwana mi sina mengi yangu macho ila kama mtafutano ndo huo sisi wageni tulokuja na ishu zetu tunaremain low profile
 
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA

CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA – MBOWE na CHADEMA – WANGWE.

Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi. Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).

Kwa tafakuri pana kila Mtanzania alitarajia kwamba kabla ya kumsimamisha Makamu Mwenyekiti, CHACHA WANGWE, Mwenyekiti wa chama hicho alitakiwa kujibu tuhuma moja baada ya ingine ili kujisafisha yeye mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA.

Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-

Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu. Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.

Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani. Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama. Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama. Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?

Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro). Ikumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.

Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?

Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?

Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?

Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.

Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.

Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.

Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.

Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.

Katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti uliopita, CHACHA WANGWE hakuwa chaguo la Mwenyekiti MBOWE, lakini aliweza kushinda. Kutokana na kitendo cha CHACHA WANGWE kutangaza kwa mara ingine kugombea Uenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi wa Disemba 2008 amezidi kujenga maadui kutoka Makao Makuu ya chama hicho. Hofu ya MBOWE inatokana na ukweli kwamba, hivi sasa WANGWE anaungwa mkono na matawi mengi ya CHADEMA nchini kutokana na msiamamo wake wa kutenda haki na kusimamia ukweli daima.

Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha. Kwa sababu hiyo, WANGWE anadai kwamba hakuelezwa siri alizovujisha hatua ambayo inakidhi matakwa ya kisheria kwamba MBOWE amemhukumu WANGWE bila hatia. Hatua hii ina lengo la kukwaza ustawi wa demokrasia na utawala bora katika vyama vya siasa.

Katika hili la kuvujisha siri WANGWE anajitetea kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa basi mtu aliyetakiwa kuwajibika ni DR SLAA ambaye mke wake ni diwani wa kuchaguliwa wa CCM wakati mkewe CHACHA WANGWE ni mwanachama mwaminifu wa CHADEMA. Kitendo cha DR SLAA kuwa na mke mkereketwa wa CCM yamkini Nyaraka za siri za CHADEMA zinaweza kuangukia kirahisi kwa mkewe na hatimae CCM na pia wageni wa CHADEMA wanaofika nyumbani kwa DR SLAA ambako kuna tawi la CCM kwa maana ya mkewe DR SLAA ambaye anawajibika kuwakirimu wageni na hivyo kusikia mazungumzo yao. WANGWE anataka kujua ni nani kati yake na DR SLAA anaeweza kuvujisha siri za CHADEMA?

Aidha, imeonekana kwamba, kutokana na nafasi yake ya Ubunge WANGWE na wabunge wengine wa upinzani wanaweza kujipatia marafiki kutoka chama tawala CCM kama ambavyo Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na marafiki kutoka vyama vya upinzani. Urafiki huu unaweza kuwa wa binafsi/kawaida kuliko mambo ya siasa kwa sababu ya uzalendo, hivyo tofauti ya itikadi siyo uadui bali ni suala la kusimamia ukweli kama ambavyo ZITTO KABWE alivyojumuika na wabunge wa CCM katika kamati ya madini ya Bomani.

Pia WANGWE anadai, kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa mbona MBOWE amewahi kuonekana akiwa katika mazungumzo na Rais JAKAYA KIKWETE hata kufikia kumkumbatia mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Halikadhalika MBOWE ameonekana katika mazungumzo na viongozi wengine wa CCM, vivyo hivyo wana CHADEMA wengine?

Kwa ujumla kashfa hizi zinakuja wakati bado baadhi ya Watanzania wanahoji uadilifu wa FREEMAN MBOWE. Kashfa ya kukopa na kushindwa kulipa deni la NSSF kwa muda stahiki ilitia mashaka ya uadilifu wa MBOWE kwa taifa lake. Hakika bila kujibu hoja nzito za WANGWE, Mwenyekiti MBOWE asitarajie kupata kura za Watanzania wenye fikra mbadala katika uchaguzi ujao ndani ya chama chake na asijisumbue kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Natoa mwito kwa MBOWE kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari kujibu tuhuma moja baada ya nyingine. Vinginevyo MBOWE atakuwa ameingia katika kundi la Wenyeviti wa vyama vya siasa wanaoua demokrasia nchini.

Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee. Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA? Kamati hiyo ilibaini ubaguzi wa kikabila na kidini katika CHADEMA lakini haikuwekwa wazi kwa Watanzania na wala haijafanyiwa kazi. Je tuwaelewe vipi viongozi hao wa CHADEMA? Ufisadi ni ule unaofanywa na viongozi wa serikali ya CCM tu? Je sio kweli kwamba Hisani siku zote inapasa kuanzia nyumbani???

Nafikiri Fikira M, ameweka mada nzuri sana. Ingefurahisha kama wana Chadema wangejitokeza kuipiga mawe, lakini sioni yeyote. Hata MMJJ amehamia kwenye vichekesho.
 
Naona Kubwa JINGA umeanza kuonyesha rangi zako halisi! Maswali yote hayo mbona tayari yameshajibiwa humu?

Au ndio staili yenu ya kupost kwenye thread nyingi suala moja ili kuwapoteza watu maboya?

Mods; unganisheni thread zote za Mbowe, Chacha Wangwe na CHADEMA, mpaka sasa zimefikika zaidi ya 7! Unganisheni tupate mtiririko wa hoja

Asha
 
Ila ukiunganisha dots unaweza kushtuka kwamba nani ni nani hasa kama upo hapa kwa ajili hiyo, mfano kwa hayo maneno yako mama hapo juu nimehisi wewe ndiye MZEE MWANAKIJIJI

Hivi unajuwa watu hawajuwi mambo ya forensic science!

Hawajuwi pia kuna sayansi ya maandishi!

Wewe unapo type hapa ni sawa na unavyoongea tu!

Na ukifanya tofauti utakuwa kituko tuu!

Speech zinaeleweka iwe ni audio,video(kwa wale wasiosikia sign languaje) halafu kuna "Hand writing analysis" ambayo typing inaweza inangukia humo!

Acha nifupishe kwa kusema hili..Kwamba ndani ya mbongo zetu picha hujijenga kutokana na maandishi ambayo huwa translated na kujenga picha ndani ya ubongo ambapo kwetu sisi wanadamu ambao tuna asili ya uchunguzi basi una fanya "BINARY" Search ama hata saa nyingine top down serach depending on the memory stored in your brain..Be it speech, audio,video an or even writen materials.

Kwa kifupi ni kwamba kuna watu wenye kuweza kwatambuwa watu kutokana na speech ama maandishi yao.
 
Haya bwana mi sina mengi yangu macho ila kama mtafutano ndo huo sisi wageni tulokuja na ishu zetu tunaremain low profile

Wageni kama hawa ambao ni watanzania wa kawaida wanashindwa kutoa michango yao kwasababu kuna some sort of a CYCLE OF MANIAC.
 
Naona Kubwa JINGA umeanza kuonyesha rangi zako halisi! Maswali yote hayo mbona tayari yameshajibiwa humu?

Au ndio staili yenu ya kupost kwenye thread nyingi suala moja ili kuwapoteza watu maboya?

Mods; unganisheni thread zote za Mbowe, Chacha Wangwe na CHADEMA, mpaka sasa zimefikika zaidi ya 7! Unganisheni tupate mtiririko wa hoja

Asha

Yamejibiwa wapi tusipopaona? Tuunganishe napo ili tuone maelezo yake. Kwa mfano kuhusiana na madereva na wabunge.
 
Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?

Huu ni uongo wa hali ya juu.

Nataja madereva wa CHADEMA.
1.Juma waziri- kutoka nachingwea.
2.Pella Ngunagwa-huyu sijui katoka wapi ila ni kusini.
3.Waziri Simba -Mkwere bagamoyo.
4.Baraka Daud -Tanga.
5.Olvary Karia -mchagga.kibosho
6.Kalikisha -Kigoma.

sasa hao wachagga wako wapi? ama mtu aje na kusema nimepotosha ama kusema uongo aweke majina yake na huyo Chacha atawapeleka pabaya fanyeni kwanza kazi ya kuhakiki maneno yake kwani mtajikuta mnajiaibisha ukweli ukiwekwa hadharani kama huu, huyu jamaa ni muongo mradi afikie lengo lake ,nendeni mkamuulize kama hawa sio madereva na ndio wapo na walikotoka.
 
Madereva wamefanya nini? Hao wazandiki wanasema CHADEMA imejaa madereva wachagga wakati ukweli ni kwamba kuna dereva mmoja tu mchagga kati ya madereva watano wa CHADEMA makao makuu. Kati ya hao watano watu wa pwani ni wawili, mbona hao hiyo taarifa ya Mziray na Ballile haisemi kwamba CHADEMA ni chama cha waswahili

Soma hiyo taarifa ya Mziray na Ballile inasema kwamba wabunge watano wa viti maalum wa CHADEMA wanatoka Kilimanjaro kati ya Wabunge Sita. We si tulijadili kwa kirefu hili suala hapa mimi na wewe? Hukumbuki ulivyoshindwa kujustify kwa mfano kuwa Maulidah Anna Komu anatako Kilimanjaro?Unakumbuka nilikupa ushahidi kuwa ni mzanzibar wa kuzaliwa, aliondoka akaolewa Kilimanjaro lakini akarejea Zanzibar na kuwa na makazi ya kudumu kuanzia miaka ya 90. Zaidi ya miaka 10 kabla ya uchaguzi? Si unakumbuka pia tulikueleza vigezo vya uteuzi hapa na kwamba kama kuna mapungufu yalikuwepo yalishatafakariwwa na hatimaye Katiba ya chama ikabaidilishwa mwaka 2006 na mjadala wa suala hili ukafungwa na mkutano mkuu Agosti 13 mwaka 2006?

Sasa unaposema huelewi wewe ambae tulibishana hapa mpaka kikaeleweka nikueleweje? Ndio maana nimesema umeanza tena kuonyesha rangi yako halisi ya ukada wa kifisadi.

Au unataka nimwite tena Mwafrika wa Kike? Maana nakumbuka alivyokuweka sawa wakati ule kwa kuanika vile ulivyo!

Asha
 
MJJ,
Revered by wanaCHADEMA is an understatement, he is godly to them. Lakini eti he is the most targeted, that is a joke. How about JK, Lowassa, RA, Pinda, Chenge etc.?? This is a proMbowe Forum and not the other way round.

Once again, it depends where you stand! Nikikuuliza utafute mada inayomsifia Mbowe hapa au yenye kumtetea utapata kazi sana, lakini nikikuambia utafute inayomkandia na kumuumbua kulinganisha na zile za JK, Lowassa, RA na Chenge.. utashangaa..

Hata kwenye suala la substance utashangaa kuwa wakati hao wengine wanaangaliwa kutoka na nafasi zao za kazi, ni mara chache if any ambapo mtu ameventure kwenye personal life zao to the same extent ambavyo Mbowe anafanyiwa.

Sasa, kwa wengine hilo ni sawa kwa sababu wanaongoza na kitu kingine (chuki) na si kwa sababu wanakuwa fair.

Kwangu bado narudi kule kule, and the same principle Mbowe, Kikwete, Pinda, Chenge are all fair game inapokuja kwenye utumishi wao kwa umma (ndani ya vyama vyao, na serikali) lakini kwenye masuala binafsi (amelala wapi, amekula wapi, amesoma kitabu gani n.k) ni nje ya mjadala unless mambo hayo yanahusiana nafedha za umma au nafasi zao. Kwa wengine that standard inawahusu wengine wote isipokuwa Mbowe tu.

And guess what, sihofu kumtetea mtu yeyote yule anayeonewa pasipo sababu ya msingi na wiki ijayo nitamtetea mtu mmoja ambaye sidhani kama kuna mtu anaona anastahili kutetewa.

Haki ni haki usichague wa kumpatia!
 
Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?

Huu ni uongo wa hali ya juu.

Nataja madereva wa CHADEMA.
1.Juma waziri- kutoka nachingwea.
2.Pella Ngunagwa-huyu sijui katoka wapi ila ni kusini.
3.Waziri Simba -Mkwere bagamoyo.
4.Baraka Daud -Tanga.
5.Olvary Karia -mchagga.kibosho
6.Kalikisha -Kigoma.

sasa hao wachagga wako wapi? ama mtu aje na kusema nimepotosha ama kusema uongo aweke majina yake na huyo Chacha atawapeleka pabaya fanyeni kwanza kazi ya kuhakiki maneno yake kwani mtajikuta mnajiaibisha ukweli ukiwekwa hadharani kama huu, huyu jamaa ni muongo mradi afikie lengo lake ,nendeni mkamuulize kama hawa sio madereva na ndio wapo na walikotoka.

Hawa ndio madereva Kubwa jinga una jingine?
 
Samahani wakuu,

Dada Asha inaelekea una muda mwingi wa kupiga bla bla.

Nadhani umesahahu kuwa ni sheria hapa kuwa huruhusiwi kumtaja jina mtu wala kazi yake. Na kwa kujaribu kutoa hints za Mpaka kieleweke na mwenzie; umevunja sheria hiyo.

Ningekuwa Moderator au admin ningekufungia angalau kwa wiki ukome tabia hii. Bahati mbaya sina madaraka.

Naomba tuache kukurupuka.

FairPlayer
 
Nilifunga mjadala kati yangu na FMES lakini si wewe, umejileta tena.

Ndio maana huna madaraka kwa kuwa unapenda sana kukurupuka.

Sasa Mbona kuhupendekeza walisema kwamba Mpaka Kieweleke na Philemoni Michael ni Mbowe hukusema wafungiwe?

Halafu unajiita Fair Player huku kila wakati ukiandika michango yako unamalizia na kidumu chama cha mapinduzi!

You can't be neutral and at the same time have side.

Na wewe inaonyesha una muda sana wa kusoma bla bla bla!

Asha
 
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA

Once again... wangeanza kwa kututafsiria wanaposema "Ukabila" wanamaanisha nini kwa sababu kaw muda wote ambao nimekuwa nikisoma jambo hili wanazungumzia kana kwamba tunakubaliana maana ya ukabila ni nini. Naamini kwa kuwasoma vizuri kwao ukabila si hisia za kabila moja kujitukuza dhidi ya mengine, au kujiona bora na wanastahili zaidi kuliko makabila mengine bali kwao ukabila is simply idadi. It has nothing to do with vitendo vya kabila fulani dhidi ya makabila mengine.

CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA – MBOWE na CHADEMA – WANGWE.

Huyo aliyeigawa katika makundi hayo ndiye mwenye lengo la kuonesha kugawanyika? Kwanini isiwe CHADEMA - KATIBA na CHADEMA - MALALAMISHI; Kwanini isiwe CHADEMA - UMOJA na CHADEMA - UTENGANO? n.K NI wazi jibu ni kuwa watu na watu ndio wanajitengenezea agenda.

Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi.

Malalamiko ya wanachama wa Chadema au mwanachama mmoja. Hadi hivi sasa sijasikia mwanachama mwingine wa Chadema aliyetoa tuhuma au madai hayo ukiondoa mtu mmoja. Basi hao wengine wajitokeze na wenyewe angalau wampe nguvu huyo mwanachama mmoja. Hao "wanachama" wako wapi?

Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).

Well, it went back to the two! Hakuna makundi as far as one can see; kuna mtu anayejidhania kundi na kuna chama ambacho kina uongozi ambao uko msimamo mmoja. Halafu Wangwe hakuwa Makamu Mwenyekiti alichaguliwa Kukaimu tu.

Kwa tafakuri pana kila Mtanzania alitarajia kwamba kabla ya kumsimamisha Makamu Mwenyekiti, CHACHA WANGWE, Mwenyekiti wa chama hicho alitakiwa kujibu tuhuma moja baada ya ingine ili kujisafisha yeye mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA.

Hili ni wazo zuri, lakini unapotakiwa kujibu tuhuma basi utoe ushahidi wa tuhuma hizo kusema namtuhumu fulani hivi halafu uoneshe msingi wa tuhuma hizo ni kejeli. Tunaposema kwa mfano kuna matumizi mabaya ya fedha katika serikali hatusemi hewan, tunachukua ripoti ya Mkaguzi Mkuu na kuiweka hadharani na kusema ripoti hii inasema hivi, namba ni hizi, na authority ya hiyo namba ni hizi. Tuhuma za Wangwe zina msingi huo?

Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-

hebu tuziangalie tuhuma hizo na kama zina "msingi"

Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu.

Vyama vya kisiasa vinatakiwa kutoa ripoti ya matumizi ya fedha za ruzuku kwa Msajili wa vyama vya siasa nchini. Chadema ni mojawapo ya vyama hivyo vya siasa. Katika mwaka wa fedha ulioisha Juni 30, 2007 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali ilionesha kuwa kuna zaidi ya Shilingi Bilioni 13 ambazo vyama vya kisiasa havikutokea maelezo jinsi gani walizitumia. Bilioni hizi 13 zinahusisha fedha siyo za Chadema tu bali CCM, CUF, TLP n.k

Kwa hiyo, Chacha ana hoja hapa na yeye angeweza kutumia ripoti ya mkaguzi mkuu kama msingi wake wa kuhoji matumizi ya ruzuku inayoenda kwenye chama chake.

Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.

Chacha amekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama chake na ameushika umakamu. Inaonekana yeye ameona vitu ambavyo watu wengi hawajahi kuviona. Kama yeye ana msingi wa madai basi aseme na kujenga hoja kuwa Chama kilipokea kiasi fulani cha ruzuku, vitabuni imeoneshwa hivi, na matumizi yake yameoneshwa vile na haiingii akilini.

Kama kweli alikuwa ananita ya kutatuta ukweli suala la ruzuku haliendi mbali, angeenda kwa Msajili wa vyama vya siasa, angefungua kesi, n.k ili kuweza kupata taarifa hizo. Akienda kwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa na kuuliza kuhusu Chadema kama kinatoa ripoti ya matumizi ya ruzuku kama inavyotakiwa na kama angeweza kuona ripoti hiyo. Hiyo ndiyo njia rahisi ya kuonesha jinsi ruzuku inavyotumika. Yawezekana Wangwe hajui ilipo ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa na majukumu yake?

Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani.

Mwanzoni ilikuwa ni "Mbowe" sasa wameamua kuongeza na "Dr. Slaa" na muda si mrefu watamuongeza na "Zitto" na wakiona haviendi wataongeza "Kamati Kuu nzima" n.k Swali ambalo Wangwe angelijibu kwanza kabla ya kuendelea na kauli yake ni lini, wapi, na kwa amri gani ambayo Dr. Slaa na Mbowe walifanya "kitendo" cha kuzuia ruzuku isifike mikoani. Hapa kwa kumsaidia anaweza akatoa barua, email, mazungumzo, kikao, au ushahidi wowote kuwa kuna agizo au uamuzi kama huo uliochukuliwa na watu hao wawili bila kumhusisha yeye kama Kaimu Makamu Mwenyekiti.

Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama.

Sasa hili la kufungua matawi ya chama halihusiani na fedha moja kwa moja, kwani matawi mangapi ya vyama vingine yanayofunguliwa na fedha toka makao makuu? Ni hoja ya kilaghai kutaka kufanya watu waamini kuwa bila fedha toka Makao Makuu matawi hayafunguliwi. Kosa kubwa la Chadema hadi hivi ni kuwa wameshindwa kuwatia moyo mashabiki wao mikoani na wilani kujianzishia matawi yao wao wenyewe. Matawi yanayoanzishwa kwa misingi ya kupewa fedha mikoani yatakufa fedha hizo zikikoma!

Nadharia hii ya Wangwe siyo tu haina msingi lakini is impractical. Matawi yanaanzishwa na mashabiki, na kwa kadiri yanavyoongezeka hadi pale yanapofikia ngazi fulani ndivyo pesa ya kuendeshea inapoanza kutolewa. Hata CCM na mabilioni yake ya fedha haitoi ruzuku kwenye matawi yake, vinginevyo wangefilisika!

Zaidi ya yote hili wazo kuwa matazi yanaanzishwa kutoka juu halina msingi, matawi ya vyama huanza kuanzia kweny shina ambako wananchi wenyewe wanaamua kuanzisha tawi la chama chao. kwa wale wanakumbuka watakumbuka jinsi gani vyama vya NCCR na CCM vilivyokuwa vinashindana kufungua matawi na hata kule Zanzibar mashindano ya CUF na CCM. NI mara ngapi fedha toka makao makuu zimetumika kufungua matawi vijijini au mitaani? Kwanini Chadema itakiwe kutumia fedha kidogo ya ruzuku kufungua matawi vijijini?

Hoja ya Wangwe ingekuwa ya msingi kama angesema uongozi wa makao makuu haujahamisha wanachama kufungua matawi sehemu mbalimbali nchini na hivyo kukosa wanachama wengi zaidi na mapato yanayotokana na mauzo ya kadi na michango ya wanachama. That is a more valid argument than saying Makao Makuu haijatuma fedha za kuanzisha matawi! this is ab absurdo

Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama.

Hii nayo ni hoja dhaifu. Kama Kamati Kuu au ile ya uchaguzi (whatever final authority is ) waliacha Mbowe atumie helikopta kufanya kampeni hilo ni kosa lao wao wenyewe. Wangwe mwenyewe ni sehemu ya Kamati hiyo. Njia pekee ya kumbebesha lawama Mbowe ni kuonesha kuwa viongozi wengine wote walikataa na walipiga kura ya kukataa lakini Mbowe AKAWALAZIMISHA aidha kwa ahadi au vitisho. Na kama waliogopa kumsimamia (akiwemo Wangwe) basi Mbowe ana ubavu mkubwa sana na hao wengine hawana ubavu wa kumpinga. Hilo linasema zaidi kuhusu wao kuliko yeye.

Hata hivyo, kama maamuzi yalichukuliwa kwa pamoja na uamuzi wa kutumia helikopta ulipitishwa kwa pamoja basi hapa ndio collective responsibility inapokuja. Hivyo Mbowe, Wangwe, Zitto, Slaa na wengine waliopitisha uamuzi huo wanawajibika moja kwa moja kwa kuwaacha "wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama." Ina maana kile anachomtuhumu Mbowe, na yeye anahusika.

Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?

kama wote walihusika na mchakato wa kuruhusu hiyo chopa, the answer is simple uongozi mzima wa Chadema akiwemo Chacha Wangwe.

Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro).
I

There it is! "Mbowe ni Mchagga wa Kilimanjaro"! Sitaki kujua wachagga wengine wanatoka wapi. Hili la Wabunge wote "kutoka mkoa wa Kilimanjaro" limeshajibiwa mara nyingi sana kiasi kwamba hata sitojaribu kuelezea. Tukumbuke tu kuwa kwa Wangwe madai ya ukabila kwake ni idadi. Period. Kuna Ukabila pale penye idadi ya watu wengi wa kabila moja mahali fulani. Ukifiria sana msimamo huu utashangaa ni sehemu ngapi tanzania kuna ukabila!

kumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.

Mbowe ndiye aliyefanya maamuzi haya? Au ndiye mwenye kubebeshwa lawama hizo. Kwanini asiseme chombo au watu waliotoa uamuzi huu ili tuweze kuona msingi wake. Maana huyu Mbowe inawezekana ana nguvu kubwa sana kiasi watu kama kina Mbowe wanashindwa kumhoji humo humo ndani.

Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?

Hili ni suala la ajira, lakini well bado tatizo ni "Wachagga wa Kilimanjaro" na kama mtu haoni sumu ya ukabila na chuki dhidi ya Wachagga wa "kilimanjaro" sijui iwekwe vipi ili ionekane.

lakini kama nilivyosema hapo juu kuwa kwa Wangwe Ukabilla ni idadi anaonesha namba. Basi si wangetoa na majina ya hao wakurugenzi ili tuweze kuamua kuona ukweli (validit) wa hoja yake? Hao wakurugenzi ni kina nani na je ni kweli ni Wachagga, na kweli wanatoka "Kilimanjaro"?

Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?

Once again tatizo siyo ajira ya watanzania bali walioajiriwa ni "wachagga" wa kutoka Kilimanjaro. Hata hivyo hili ni rahisi kwani tunayo majina ya madereva wa makao makuu.

1.Juma waziri- kutoka nachingwea.
2.Pella Ngunagwa-huyu sijui katoka wapi ila ni kusini.
3.Waziri Simba -Mkwere bagamoyo.
4.Baraka Daud -Tanga.
5.Olvary Karia -mchagga.kibosho
6.Kalikisha -Kigoma.

Sasa njia pekee ya dai hili kuwa na nguvu ni kwa Wangwe kutoa majina yake ya madereva wa makao makuu na kuonesha kuwa ni "Wachagga wa Kilimanjaro". Haitoshi tu kusema bali angalau aoneshe chembe ya ushahidi wa madai kama haya kuwa "Madereva wote".

Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?

Hili ni swali zuri lakini lina ufundi. Je kuna wanachama ambao waliamua kukikopesha fedha chama fedha ambazo wanatarajia kulipwa? Kama wapo wanachama hao na ni kweli waliingia makubaliano na chama, wakatia sahihi na masharti yapo na wakatoa fedha hizo, swali kwanini wasilipwe? Jambo pekee ambalo Wangwe anaweza kulionesha ni kusema kuwa hakuna makubaliano yoyote ya kukikopesha chama na hivyo malipo wanayojilipa hayana msingi wa kisheria.

In that case kinachofanyika ni wizi na Wangwe ana haki ya kwenda mahakamani siyo kulalamika. Kwa mpambanaji kama yeye anajua wapi pa kukimbilia.

Kuhusu wanachama wengine, swali ni hilo hilo je na wao waliingia mkataba wa kukikopesha chama na hadi sasa hawalipwi? Ni kina nani hao na waliingia mkataba huo lini na kwa makubaliano gani?

Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.

kwa mara nyingine tena, anampa nguvu kubwa sana Mbowe. Wanachama wa Chadema Dar wako wapi kutoa malalamiko haya? Kama kuna mtu anataka kuanzisha tawi dar kwanini wasianzishe? Je ni kweli Mbowe ndiye aliyevunja tawi hilo? Hapa tunahitaji habari zaidi maana mtu mwenye nguvu ya kuvunja tawi zima na viongozi wenzie kama kina Wangwe wakawa wanamuangalia basi wamempa nguvu za kidikteta; aidha wanahitaji kubadili Katiba au kumuondoa madarakani!

Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA.

Hapa inabidi atuoneshe angalau hiyo Katiba inasema nini kuhusu Wakurugenzi wa Chama. Kwa kuisoma kwangu kwa haraka inasema kuwa Kamati Kuu itakuwa ina jukumu la kuwateua "Wakurugenzi wa Idara Kuu za Chama Makao Makuu"

Sasa kama kweli Mbowe ndiye aliyewateua wakurungezi hao (note a fine difference from what the constitution says and what Wangwe alleges) basi tatizo bado liko kwenye uongozi mzima wa Chadema kwa kumuacha Mbowe avunje Katiba na badala ya kumshtaki au kujenga hoja ya kuondolewa madarakani kwa kuvunja Katiba mtu anaamua kulalamika pembeni. Kumbuka hapo juu tayari ameshadai kuwa wakurunzi wanne ni "Wachagga wa Kilimanjaro".

Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.

Nimeangalia kwenye Katiba iliyoko kwenye tovuti yao na sijaona kipengele hicho ambacho kinasema Katibu Mkuu anatakiwa kuwajibikwa kwa Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti. Kipengele hicho kinasema hivi:

7.7.3 Viongozi Wakuu wa Ngazi ya Taifa watakuwa wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa taifa
(b) Makamu Mwenyekiti Bara
(c) Makamu Mwenyekiti Zanzibar
(d) Katibu Mkuu
(e) Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
(f) Naibu Katibu Mkuu (Bara)

yawezekana Katiba iliongezwa kipengele kidogo cha (iii). Mwenye nacho naomba akiweke na kusema kinasemaje.

Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.

I give up on this one! Tuambie basi hao wengine nao wa makabila gani?

Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo.

Inadaiwa na nani, na yeye au na mtu mwingine.?

Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.

very vague.. taja majina au nafasi yoyote au viongozi ambao hawakufika kwa sababu walifichwa habari hizo. Kwa mujibu wa kanuni za Chadema, sasa basi angalau taja hizo kanuni ziko wapi. Kwa mujibu wa hiyo Katiba mahali pekee ambapo suala la siku 21 lipo ni hapa:

Mapendekezo ya marekebisho ya Katiba yatafikishwa kwa kamati za Wilaya sio chini ya siku 30 kabla ya tarehe ya Mkutano Mkuu unaohusika kujadili mabadiliko. Kamati za Wilaya zitatakiwa kurejesha maoni yake katika siku 21 tangu tarehe ya mapendekezo kutumwa.

Hivyo suala la siku 21 halihusiani na vikao vya kawaida bali suala la kubadilisha Katiba.

Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.

Ingekuwa kwenye mpira wa basketball hapa ndipo ile horn ya kumiss basket inapolia.. ng'eeee!

Katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti uliopita, CHACHA WANGWE hakuwa chaguo la Mwenyekiti MBOWE, lakini aliweza kushinda.

Wow! sasa si ndio uzuri wa demokrasia? Kwani hadi Mwenyekiti akukubali ndio uona uhalali wa wewe kuwepo. As long as umeshinda fair and square si Mbowe wala Slaa ambao wanaweza kufanya lolote nje ya taratibu za kikazi.

Kutokana na kitendo cha CHACHA WANGWE kutangaza kwa mara ingine kugombea Uenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi wa Disemba 2008 amezidi kujenga maadui kutoka Makao Makuu ya chama hicho.

Hakuna baya mtu kujipigia panda. Angalau tunaweza kuona nini kinafanyika. It is all about election. Ni kuhusu kuchaguliwa tu na kuwa on top!

Hofu ya MBOWE inatokana na ukweli kwamba, hivi sasa WANGWE anaungwa mkono na matawi mengi ya CHADEMA nchini kutokana na msiamamo wake wa kutenda haki na kusimamia ukweli daima.

Hadi leo sijasikia matawi yaliyojitokeza kumuunga mkono Wangwe, maana hata tawi la kwake Tarime wameanza kumgeuka. Natoa wito kwa matawi yanayomuunga Wangwe kujitokeza na kumuunga mkono hadharani. Lakini hili swali la "kutenda haki na kusimamia ukweli" tungewauliza wachagga ambao wanajikuta wanatakiwa kufanya kazi na Wangwe kama wanajisikia kutendewa haki na kufanyiwa mambo kwa ukweli. Sitoshangaa kama Wangwe anaweza kumkataa dereva Mchagga akipatiwa!

Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha. Kwa sababu hiyo, WANGWE anadai kwamba hakuelezwa siri alizovujisha hatua ambayo inakidhi matakwa ya kisheria kwamba MBOWE amemhukumu WANGWE bila hatia. Hatua hii ina lengo la kukwaza ustawi wa demokrasia na utawala bora katika vyama vya siasa.

Katika hili la kuvujisha siri WANGWE anajitetea kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa basi mtu aliyetakiwa kuwajibika ni DR SLAA ambaye mke wake ni diwani wa kuchaguliwa wa CCM wakati mkewe CHACHA WANGWE ni mwanachama mwaminifu wa CHADEMA. Kitendo cha DR SLAA kuwa na mke mkereketwa wa CCM yamkini Nyaraka za siri za CHADEMA zinaweza kuangukia kirahisi kwa mkewe na hatimae CCM na pia wageni wa CHADEMA wanaofika nyumbani kwa DR SLAA ambako kuna tawi la CCM kwa maana ya mkewe DR SLAA ambaye anawajibika kuwakirimu wageni na hivyo kusikia mazungumzo yao. WANGWE anataka kujua ni nani kati yake na DR SLAA anaeweza kuvujisha siri za CHADEMA?

Aidha, imeonekana kwamba, kutokana na nafasi yake ya Ubunge WANGWE na wabunge wengine wa upinzani wanaweza kujipatia marafiki kutoka chama tawala CCM kama ambavyo Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na marafiki kutoka vyama vya upinzani. Urafiki huu unaweza kuwa wa binafsi/kawaida kuliko mambo ya siasa kwa sababu ya uzalendo, hivyo tofauti ya itikadi siyo uadui bali ni suala la kusimamia ukweli kama ambavyo ZITTO KABWE alivyojumuika na wabunge wa CCM katika kamati ya madini ya Bomani.

Pia WANGWE anadai, kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa mbona MBOWE amewahi kuonekana akiwa katika mazungumzo na Rais JAKAYA KIKWETE hata kufikia kumkumbatia mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Halikadhalika MBOWE ameonekana katika mazungumzo na viongozi wengine wa CCM, vivyo hivyo wana CHADEMA wengine?

Kwa ujumla kashfa hizi zinakuja wakati bado baadhi ya Watanzania wanahoji uadilifu wa FREEMAN MBOWE. Kashfa ya kukopa na kushindwa kulipa deni la NSSF kwa muda stahiki ilitia mashaka ya uadilifu wa MBOWE kwa taifa lake. Hakika bila kujibu hoja nzito za WANGWE, Mwenyekiti MBOWE asitarajie kupata kura za Watanzania wenye fikra mbadala katika uchaguzi ujao ndani ya chama chake na asijisumbue kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Natoa mwito kwa MBOWE kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari kujibu tuhuma moja baada ya nyingine. Vinginevyo MBOWE atakuwa ameingia katika kundi la Wenyeviti wa vyama vya siasa wanaoua demokrasia nchini.

Katika hili ni wazi kuwa ni suala binafsi sana kati ya Wangwe na Mbowe at least kwa upande wa Wangwe. Ushauri wangu ni kuwa nyinyi watu wawili tu muitane Ngurdoto yenu na mkae mzungumze, no TV no radio, no newspaper na mkimaliza mje na msimamo wenu, mambo ya kukubaliana mkubaliane ya kupingana mpingane, lakini inaonekana kuna mambo mawili yanayowahusu ninyi watu wawili. It is more personal than professional.

Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee.

WoW shujaa amesimama na kujitangaza kuwa kazi anaifanya peke yake! Well, wakati mwingine mtoto anaweza kuingia chumbani na akaanza kupigana na jinamizi la chini ya uvungu, jinamizi ambalo ni yeye pekee analiona!

Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA? Kamati hiyo ilibaini ubaguzi wa kikabila na kidini katika CHADEMA lakini haikuwekwa wazi kwa Watanzania na wala haijafanyiwa kazi. Je tuwaelewe vipi viongozi hao wa CHADEMA? Ufisadi ni ule unaofanywa na viongozi wa serikali ya CCM tu? Je sio kweli kwamba Hisani siku zote inapasa kuanzia nyumbani???

Kama Wangwe ana ripoti hiyo, basi aitoe, kama Mziray (yeye siyo mtu wa Kilimanjaro?) na yeye aitoe ili kijulikane kilichomo.
 
Hii mbinu imepitwa na wakati; ilifanikiwa katika kuisambaratisha NCCR lakini sasa hivi haitawezekana kwa sababu watanzania wameshashtuka. Sasa ukiibuka na madai ya blabla unajibiwa na unajiabisha. Sasa Mpaka Kieleweke na MKJJ wamejibu hoja moja baada ya ingine, tunasubiri hawa wenzetu watumishi wa Wangwe na aliyejipeleka kanisani waje na uzushi mwingine. The bottom line: watanzania wameshashtuka, wanaweza kuchambua pumba na mchele. Wangwe anavyozidi kupayuka anazidi kuanika udhaifu wake. Yeye ni mjumbe wa kila kikao ndani ya chadema, kama ameshindwa kuwashawishi wajumbe wenzake na madai yake, ataweza kuwashawishi watanzania?
 
Once again... wangeanza kwa kututafsiria wanaposema "Ukabila" wanamaanisha nini kwa sababu kaw muda wote ambao nimekuwa nikisoma jambo hili wanazungumzia kana kwamba tunakubaliana maana ya ukabila ni nini. Naamini kwa kuwasoma vizuri kwao ukabila si hisia za kabila moja kujitukuza dhidi ya mengine, au kujiona bora na wanastahili zaidi kuliko makabila mengine bali kwao ukabila is simply idadi. It has nothing to do with vitendo vya kabila fulani dhidi ya makabila mengine.

Huyo aliyeigawa katika makundi hayo ndiye mwenye lengo la kuonesha kugawanyika? Kwanini isiwe CHADEMA - KATIBA na CHADEMA - MALALAMISHI; Kwanini isiwe CHADEMA - UMOJA na CHADEMA - UTENGANO? n.K NI wazi jibu ni kuwa watu na watu ndio wanajitengenezea agenda.

Malalamiko ya wanachama wa Chadema au mwanachama mmoja. Hadi hivi sasa sijasikia mwanachama mwingine wa Chadema aliyetoa tuhuma au madai hayo ukiondoa mtu mmoja. Basi hao wengine wajitokeze na wenyewe angalau wampe nguvu huyo mwanachama mmoja. Hao "wanachama" wako wapi?

Well, it went back to the two! Hakuna makundi as far as one can see; kuna mtu anayejidhania kundi na kuna chama ambacho kina uongozi ambao uko msimamo mmoja. Halafu Wangwe hakuwa Makamu Mwenyekiti alichaguliwa Kukaimu tu.

Hili ni wazo zuri, lakini unapotakiwa kujibu tuhuma basi utoe ushahidi wa tuhuma hizo kusema namtuhumu fulani hivi halafu uoneshe msingi wa tuhuma hizo ni kejeli. Tunaposema kwa mfano kuna matumizi mabaya ya fedha katika serikali hatusemi hewan, tunachukua ripoti ya Mkaguzi Mkuu na kuiweka hadharani na kusema ripoti hii inasema hivi, namba ni hizi, na authority ya hiyo namba ni hizi. Tuhuma za Wangwe zina msingi huo?

hebu tuziangalie tuhuma hizo na kama zina "msingi"

Vyama vya kisiasa vinatakiwa kutoa ripoti ya matumizi ya fedha za ruzuku kwa Msajili wa vyama vya siasa nchini. Chadema ni mojawapo ya vyama hivyo vya siasa. Katika mwaka wa fedha ulioisha Juni 30, 2007 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali ilionesha kuwa kuna zaidi ya Shilingi Bilioni 13 ambazo vyama vya kisiasa havikutokea maelezo jinsi gani walizitumia. Bilioni hizi 13 zinahusisha fedha siyo za Chadema tu bali CCM, CUF, TLP n.k

Kwa hiyo, Chacha ana hoja hapa na yeye angeweza kutumia ripoti ya mkaguzi mkuu kama msingi wake wa kuhoji matumizi ya ruzuku inayoenda kwenye chama chake.

Chacha amekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama chake na ameushika umakamu. Inaonekana yeye ameona vitu ambavyo watu wengi hawajahi kuviona. Kama yeye ana msingi wa madai basi aseme na kujenga hoja kuwa Chama kilipokea kiasi fulani cha ruzuku, vitabuni imeoneshwa hivi, na matumizi yake yameoneshwa vile na haiingii akilini.

Kama kweli alikuwa ananita ya kutatuta ukweli suala la ruzuku haliendi mbali, angeenda kwa Msajili wa vyama vya siasa, angefungua kesi, n.k ili kuweza kupata taarifa hizo. Akienda kwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa na kuuliza kuhusu Chadema kama kinatoa ripoti ya matumizi ya ruzuku kama inavyotakiwa na kama angeweza kuona ripoti hiyo. Hiyo ndiyo njia rahisi ya kuonesha jinsi ruzuku inavyotumika. Yawezekana Wangwe hajui ilipo ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa na majukumu yake?

Mwanzoni ilikuwa ni "Mbowe" sasa wameamua kuongeza na "Dr. Slaa" na muda si mrefu watamuongeza na "Zitto" na wakiona haviendi wataongeza "Kamati Kuu nzima" n.k Swali ambalo Wangwe angelijibu kwanza kabla ya kuendelea na kauli yake ni lini, wapi, na kwa amri gani ambayo Dr. Slaa na Mbowe walifanya "kitendo" cha kuzuia ruzuku isifike mikoani. Hapa kwa kumsaidia anaweza akatoa barua, email, mazungumzo, kikao, au ushahidi wowote kuwa kuna agizo au uamuzi kama huo uliochukuliwa na watu hao wawili bila kumhusisha yeye kama Kaimu Makamu Mwenyekiti.

Sasa hili la kufungua matawi ya chama halihusiani na fedha moja kwa moja, kwani matawi mangapi ya vyama vingine yanayofunguliwa na fedha toka makao makuu? Ni hoja ya kilaghai kutaka kufanya watu waamini kuwa bila fedha toka Makao Makuu matawi hayafunguliwi. Kosa kubwa la Chadema hadi hivi ni kuwa wameshindwa kuwatia moyo mashabiki wao mikoani na wilani kujianzishia matawi yao wao wenyewe. Matawi yanayoanzishwa kwa misingi ya kupewa fedha mikoani yatakufa fedha hizo zikikoma!

Nadharia hii ya Wangwe siyo tu haina msingi lakini is impractical. Matawi yanaanzishwa na mashabiki, na kwa kadiri yanavyoongezeka hadi pale yanapofikia ngazi fulani ndivyo pesa ya kuendeshea inapoanza kutolewa. Hata CCM na mabilioni yake ya fedha haitoi ruzuku kwenye matawi yake, vinginevyo wangefilisika!

Zaidi ya yote hili wazo kuwa matazi yanaanzishwa kutoka juu halina msingi, matawi ya vyama huanza kuanzia kweny shina ambako wananchi wenyewe wanaamua kuanzisha tawi la chama chao. kwa wale wanakumbuka watakumbuka jinsi gani vyama vya NCCR na CCM vilivyokuwa vinashindana kufungua matawi na hata kule Zanzibar mashindano ya CUF na CCM. NI mara ngapi fedha toka makao makuu zimetumika kufungua matawi vijijini au mitaani? Kwanini Chadema itakiwe kutumia fedha kidogo ya ruzuku kufungua matawi vijijini?

Hoja ya Wangwe ingekuwa ya msingi kama angesema uongozi wa makao makuu haujahamisha wanachama kufungua matawi sehemu mbalimbali nchini na hivyo kukosa wanachama wengi zaidi na mapato yanayotokana na mauzo ya kadi na michango ya wanachama. That is a more valid argument than saying Makao Makuu haijatuma fedha za kuanzisha matawi! this is ab absurdo

Hii nayo ni hoja dhaifu. Kama Kamati Kuu au ile ya uchaguzi (whatever final authority is ) waliacha Mbowe atumie helikopta kufanya kampeni hilo ni kosa lao wao wenyewe. Wangwe mwenyewe ni sehemu ya Kamati hiyo. Njia pekee ya kumbebesha lawama Mbowe ni kuonesha kuwa viongozi wengine wote walikataa na walipiga kura ya kukataa lakini Mbowe AKAWALAZIMISHA aidha kwa ahadi au vitisho. Na kama waliogopa kumsimamia (akiwemo Wangwe) basi Mbowe ana ubavu mkubwa sana na hao wengine hawana ubavu wa kumpinga. Hilo linasema zaidi kuhusu wao kuliko yeye.

Hata hivyo, kama maamuzi yalichukuliwa kwa pamoja na uamuzi wa kutumia helikopta ulipitishwa kwa pamoja basi hapa ndio collective responsibility inapokuja. Hivyo Mbowe, Wangwe, Zitto, Slaa na wengine waliopitisha uamuzi huo wanawajibika moja kwa moja kwa kuwaacha "wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama." Ina maana kile anachomtuhumu Mbowe, na yeye anahusika.

kama wote walihusika na mchakato wa kuruhusu hiyo chopa, the answer is simple uongozi mzima wa Chadema akiwemo Chacha Wangwe.

I

There it is! "Mbowe ni Mchagga wa Kilimanjaro"! Sitaki kujua wachagga wengine wanatoka wapi. Hili la Wabunge wote "kutoka mkoa wa Kilimanjaro" limeshajibiwa mara nyingi sana kiasi kwamba hata sitojaribu kuelezea. Tukumbuke tu kuwa kwa Wangwe madai ya ukabila kwake ni idadi. Period. Kuna Ukabila pale penye idadi ya watu wengi wa kabila moja mahali fulani. Ukifiria sana msimamo huu utashangaa ni sehemu ngapi tanzania kuna ukabila!

Mbowe ndiye aliyefanya maamuzi haya? Au ndiye mwenye kubebeshwa lawama hizo. Kwanini asiseme chombo au watu waliotoa uamuzi huu ili tuweze kuona msingi wake. Maana huyu Mbowe inawezekana ana nguvu kubwa sana kiasi watu kama kina Mbowe wanashindwa kumhoji humo humo ndani.

Hili ni suala la ajira, lakini well bado tatizo ni "Wachagga wa Kilimanjaro" na kama mtu haoni sumu ya ukabila na chuki dhidi ya Wachagga wa "kilimanjaro" sijui iwekwe vipi ili ionekane.

lakini kama nilivyosema hapo juu kuwa kwa Wangwe Ukabilla ni idadi anaonesha namba. Basi si wangetoa na majina ya hao wakurugenzi ili tuweze kuamua kuona ukweli (validit) wa hoja yake? Hao wakurugenzi ni kina nani na je ni kweli ni Wachagga, na kweli wanatoka "Kilimanjaro"?

Once again tatizo siyo ajira ya watanzania bali walioajiriwa ni "wachagga" wa kutoka Kilimanjaro. Hata hivyo hili ni rahisi kwani tunayo majina ya madereva wa makao makuu.

1.Juma waziri- kutoka nachingwea.
2.Pella Ngunagwa-huyu sijui katoka wapi ila ni kusini.
3.Waziri Simba -Mkwere bagamoyo.
4.Baraka Daud -Tanga.
5.Olvary Karia -mchagga.kibosho
6.Kalikisha -Kigoma.

Sasa njia pekee ya dai hili kuwa na nguvu ni kwa Wangwe kutoa majina yake ya madereva wa makao makuu na kuonesha kuwa ni "Wachagga wa Kilimanjaro". Haitoshi tu kusema bali angalau aoneshe chembe ya ushahidi wa madai kama haya kuwa "Madereva wote".

Hili ni swali zuri lakini lina ufundi. Je kuna wanachama ambao waliamua kukikopesha fedha chama fedha ambazo wanatarajia kulipwa? Kama wapo wanachama hao na ni kweli waliingia makubaliano na chama, wakatia sahihi na masharti yapo na wakatoa fedha hizo, swali kwanini wasilipwe? Jambo pekee ambalo Wangwe anaweza kulionesha ni kusema kuwa hakuna makubaliano yoyote ya kukikopesha chama na hivyo malipo wanayojilipa hayana msingi wa kisheria.

In that case kinachofanyika ni wizi na Wangwe ana haki ya kwenda mahakamani siyo kulalamika. Kwa mpambanaji kama yeye anajua wapi pa kukimbilia.

Kuhusu wanachama wengine, swali ni hilo hilo je na wao waliingia mkataba wa kukikopesha chama na hadi sasa hawalipwi? Ni kina nani hao na waliingia mkataba huo lini na kwa makubaliano gani?

kwa mara nyingine tena, anampa nguvu kubwa sana Mbowe. Wanachama wa Chadema Dar wako wapi kutoa malalamiko haya? Kama kuna mtu anataka kuanzisha tawi dar kwanini wasianzishe? Je ni kweli Mbowe ndiye aliyevunja tawi hilo? Hapa tunahitaji habari zaidi maana mtu mwenye nguvu ya kuvunja tawi zima na viongozi wenzie kama kina Wangwe wakawa wanamuangalia basi wamempa nguvu za kidikteta; aidha wanahitaji kubadili Katiba au kumuondoa madarakani!

Hapa inabidi atuoneshe angalau hiyo Katiba inasema nini kuhusu Wakurugenzi wa Chama. Kwa kuisoma kwangu kwa haraka inasema kuwa Kamati Kuu itakuwa ina jukumu la kuwateua "Wakurugenzi wa Idara Kuu za Chama Makao Makuu"

Sasa kama kweli Mbowe ndiye aliyewateua wakurungezi hao (note a fine difference from what the constitution says and what Wangwe alleges) basi tatizo bado liko kwenye uongozi mzima wa Chadema kwa kumuacha Mbowe avunje Katiba na badala ya kumshtaki au kujenga hoja ya kuondolewa madarakani kwa kuvunja Katiba mtu anaamua kulalamika pembeni. Kumbuka hapo juu tayari ameshadai kuwa wakurunzi wanne ni "Wachagga wa Kilimanjaro".

Nimeangalia kwenye Katiba iliyoko kwenye tovuti yao na sijaona kipengele hicho ambacho kinasema Katibu Mkuu anatakiwa kuwajibikwa kwa Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti. Kipengele hicho kinasema hivi:

yawezekana Katiba iliongezwa kipengele kidogo cha (iii). Mwenye nacho naomba akiweke na kusema kinasemaje.

I give up on this one!

Inadaiwa na nani, na yeye au na mtu mwingine.?

very vague.. taja majina au nafasi yoyote au viongozi ambao hawakufika kwa sababu walifichwa habari hizo. Kwa mujibu wa kanuni za Chadema, sasa basi angalau taja hizo kanuni ziko wapi. Kwa mujibu wa hiyo Katiba mahali pekee ambapo suala la siku 21 lipo ni hapa:

Hivyo suala la siku 21 halihusiani na vikao vya kawaida bali suala la kubadilisha Katiba.

Ingekuwa kwenye mpira wa basketball hapa ndipo ile horn ya kumiss basket inapolia.. ng'eeee!

Wow! sasa si ndio uzuri wa demokrasia? Kwani hadi Mwenyekiti akukubali ndio uona uhalali wa wewe kuwepo. As long as umeshinda fair and square si Mbowe wala Slaa ambao wanaweza kufanya lolote nje ya taratibu za kikazi.

Hakuna baya mtu kujipigia panda. Angalau tunaweza kuona nini kinafanyika. It is all about election. Ni kuhusu kuchaguliwa tu na kuwa on top!

Hadi leo sijasikia matawi yaliyojitokeza kumuunga mkono Wangwe, maana hata tawi la kwake Tarime wameanza kumgeuka. Natoa wito kwa matawi yanayomuunga Wangwe kujitokeza na kumuunga mkono hadharani. Lakini hili swali la "kutenda haki na kusimamia ukweli" tungewauliza wachagga ambao wanajikuta wanatakiwa kufanya kazi na Wangwe kama wanajisikia kutendewa haki na kufanyiwa mambo kwa ukweli. Sitoshangaa kama Wangwe anaweza kumkataa dereva Mchagga akipatiwa!

Katika hili ni wazi kuwa ni suala binafsi sana kati ya Wangwe na Mbowe at least kwa upande wa Wangwe. Ushauri wangu ni kuwa nyinyi watu wawili tu muitane Ngurdoto yenu na mkae mzungumze, no TV no radio, no newspaper na mkimaliza mje na msimamo wenu, mambo ya kukubaliana mkubaliane ya kupingana mpingane, lakini inaonekana kuna mambo mawili yanayowahusu ninyi watu wawili. It is more personal than professional.

WoW shujaa amesimama na kujitangaza kuwa kazi anaifanya peke yake! Well, wakati mwingine mtoto anaweza kuingia chumbani na akaanza kupigana na jinamizi la chini ya uvungu, jinamizi ambalo ni yeye pekee analiona!

Kama Wangwe ana ripoti hiyo, basi aitoe, kama Mziray (yeye siyo mtu wa Kilimanjaro?) na yeye aitoe ili kijulikane kilichomo.

Ebwana umenichekesha sana.

Na umenifurahisha ulivyochambua.

Sasa hawa na propaganda zao wanayotoa hayo kama makala kwenye Majira na Mtanzania na Rai. Kwanini na nyinyi wachambuzi huru na makini msichambue mambo haya Tanzania Daima, Mwananchi na Kulikoni? Maana naona mafisadi wamedhamiria kuhamisha mjadala kwa kweli

Asha
 
Kitila Mkumbo Kitila Mkumbo is Thinking independently, deciding collectively!
JF Senior & Premium Member Join Date: Sat Feb 2006

Re: Mpaka Kieleweke Si Mbowe

1. Kwamba Mbowe ndiye Mpaka Kieleweke ni uongo.

2. Kwamba FMES amewahi kusema Mpaka Kieleweke ndiye Mbowe ni uongo vilevile, labda kama alisema nje ya forum hii.

3. Hivyo basi tusipoteze muda kujadili kitu ambacho hakipo. Kwa upendeleo, hii mada inaweza kusogezwa kwenye udaku haraka sana, vinginevyo ni vizuri ikaondolewa.

4. Hakuna ubaya pia kama dada Asha atamtaka radhi FMES, hata kama ni pembeni huko PM, kwa kumzushia kajambo!

Tuendelee na mijadala mingine tafadhali.

Mkuu Kitila heshima mbele na hapa tupo ukurasa mmoja!
 
Nilisema sitachangia tena hapa lakini kwa kuwa nimetakiwa kuomba radhi naomba niseme maneno machache ya mwisho kabisa.

1. FMES amekiri mwenyewe kuwa ni kweli hapa kuna watu wameanzisha maneno kwamba Mpaka Kieleweke ni Mbowe. Na amekiri kwamba ni kweli kwamba alimkataza asifanye spin. Sasa nendeni kwenye mtiririko wa yale maongezi na someni na mchango wangu nilivyoandika hapa.

1. Mimi ndiye Field Marshall Es sauti ya umeme, ni kweli nilimuambia Mpaka Kieleweke kuwa haifai yeye ku-spin awaachie wengine kama katibu mkuu, sasa hii inamfanya Kieleweke awe Mbowe? Inamfanya awe Mwenyekiti wa Chadema? What a logic? Kwa nini asiwe Wangwe makamu? Kwa nini asiwe Zitto? Kwa nini inalizimishwa awe Mbowe?

Mtitiririko wa maongezi unaweza ku-prove kuwa nimesema Kieleweke ni Mbowe?

2. Mimi sikusema na wala sijawahi hapa JF kutaja jina la mtu, unless yeye amenihisi akanisema hisia zake na mimi nikamjibu, hakuna mahali nimewahji kusema kuwa Kieleweke ni Mbowe, huo ni uzushi na sababu yake ninaijua na nitaisema kabla sijamaliza kujibu,

nilimuomba Kieleweke awaaachie wengine ku-spin, akanijibu kuwa amenielewa kwa PM na akashukuru sana kwa ushauri wangu, lakini hakusema kuwa nimemuita Mbowe, sasa haya mashambuilzi kutoka kwako Asha ni ya nini? au kuna kitu kunajaribiwa kufichwa hapa?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom