Bikirembwe,
Heshima mbele mkuu, tunasema tena humu ndani kuna watu wenye tabia ya kukimbilia lines za ID, wanapozidiwa hoja sasa tulichofanya ni kwamba tuna orodha ya hao watu, na tunachosema ni kwamba kwanza tume-extend sasa na tutamlinda anybody tutakayeona anaonewa on those lines kwa kufichua pia ID za wale the aggressors kwa sababu tunazo, kwenye hili hakuna compromise kwa sababu ni suala la self-defense, kwa sababu kwa kawaida watu wa namna hii huwa wana tabia ya kuwa na majina mengi humu, moja hulitumia kwa kujifanya wastaaarabu halafu mengine huyatumiwa kuwatukania watu wengine na hata kugusa hizo lines za ID, and then hugeuka na kujifanya wastaarabu sana na majina mengine, tunawajua vizuri sana hatuna tatizo na hilo, lakini kwa wale wenye jina moja tu kama mimi tutajilinda kwa nguvu zote bila kuogopa wala kujali nani yuko upande wa pili!
Tuliamua haya baada ya pain nyingi sana zilizosababishwa na hawa watu, in fact JF tumepoteza members wengi mashururi kwa tabia hii, na mimi binafsi hii tabia ninaifahmu kwa karibu sana kwa sababu kidogo im-cost kazi mwanamama mmoja ninayemfahamu ambaye mmoja kati ya hawa wajinga alirusha jina lake hapa baada ya mimi kumzidia hoja hapa, ni mpaka nilipomtishia kumpa mkewe habari zake za kuwa na hawara nje ya mkewe na nikamtajia hata jina ndio aka-back off, na yeye kuomba radhi kazini kwa yule dada kwa sababu jamaa aliwahi kufanya kazi pale zamani kabla ya huyu dada,
Sasa kwenye hili I am dead serious, kwamba tuendele kujadiliana kwa misingi ya sheria za JF kwa kuheshimiana na kus-tick kwenye mistari ya hoja za kisiasa hasa kwa viongozi wanaohusika, lakini asiyetaka kuelewa hili ni langu mimi ndiyo nimelivalia njuga ninasema kuwa ni langu personal, otherwise hawezi kutajwa mtu hapa bila sababu huwa sio tabia yetu, na kwa mara ya kwanza ninashukuru kupata nafasi ya kuweza kuliweka wazi hili hapa.
Lakini ujumbe wako umesikika na umefika.