Mpaka Kifo Kitakapo tutenganisha - Mpango wa Dalia Dippolito kumuua mme wake

Mpaka Kifo Kitakapo tutenganisha - Mpango wa Dalia Dippolito kumuua mme wake

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,468
Reaction score
32,167
Hakuna jambo gumu kama kuchagua mwenza wa maisha yako ambaye utaishi naye maisha yako yote mpaka pale kifo kitakapowatengenisha. Kujitolea kuishi na mtu siyo jambo jepesi, ndiyo maana mimi Nafaka mpaka leo sijaamua nasubiri mpaka pale kiongozi wetu Le baharia Lemutuz atakapoanza yeye au atakapotoa mwelekeo kwetu wafuasi wake!

Hivi itakuwaje iwapo mtu unayehisi anakupenda, amejitoa, na kukujali kama wewe unavyomjali kumbe ni maigizo tu, na anatamani ufe tu? Kwangu mimi nitamtanguliza yeye kabla hajanitanguliza mimi.

12.jpg

Huko Florida, Michael Dippolito alikuwa kamuoa binti mrembo Dalia Dippolito ndoa ikiwa changa changa imejaa mahaba ya kila aina. Michael kabla ya kumuoa Dallila alikuwa tayari anamiliki ukwasi wa kutosha. Michael aliweza kuwa na ukwasi wa maana baada ya kuwekeza katika biashara moja ya kitapeli iliyohusisha kubadilisha pesa za kigeni. Katika utapeli huo, Michael alikuwa akipata mamia ya dollar kila siku.

Kwa upande mwingine, Dallila yeye alikuwa akifanya kazi kama kahaba (Kwa lugha ya wenzetu siku hizi wanawaita ma escort hata Tanzania wapo wazuri balaa sema charges zao ni $50 @hr ila ni wazuri kwakweli). Siku moja hawa wawili wanakutana kwenye kiduka cha kuuza kahawa na hapo ndipo mahusiano yao yalianza.

Baada ya muda mfupi wawili hawa walioana, Dallila akaacha kazi yake ya kutoa huduma kwa mijidume iliyo na uhitaji wa kampani. Ndani ya muda mfupi Michael penzi shata shata la mtoto Dallila likamchanganya na kumpindua miguu juu kama mende hadi akabadili umiliki wa nyumba yake ambapo akampa asilimia kubwa ya umiliki Dallila. Haya mapenzi haya yaacheni sijui uwa hawa mabinti wanatupa nini mimi sijawahi kuelewa.

Michael hakuishia hapao, Dallila alitaka apendeze zaidi awe na shape la kuchora kama ile midada ya kwenye majarida ya zamani lile la Bongo, Sani na Tabasamu, basi ikabidi Michael aghalamie bidada afanyiwe plastic surgery yenye thamani ya dollar $200,000 (Kiasi cha milioni 500 za kibongo). Pia alimtunuku zawadi za vito vya thamani vyenye thamani zaidi ya dollar $100,000.

Michael alivyokuwa boya tena lofa, alidhani unaweza kumfuga kunguru kwa kumpa chakula akiwa bandani, kumbe hata umpe nini amezoea kuruka ruka tu. Michael alikuwa akimpa kila kitu anachotaka ili tu kumfanya ampende zaidi. Kumbe hakujua jinsi anavyozidi kutoa na kumhonga ndivyo binti anavyoona hili chimbo lina pesa sana, kwanini nisilimiliki mwenyewe badala ya kusubiri kupewa.

Dallila alianza kutamani sana pesa ya Michael, akawa anawaza njia gani itamfanya awe mmiliki halali na pekee wa mali na pesa ya huyu shababi. Njia ni moja tu na iko wazi kama dish juu ya bati, lazima Michael afe. Akimuua Michael atapata malipo ya Bima, mali zake pamoja na pesa zake na kila kitu. Hapa ndipo alianza kuandaa mpango kabambe wa kumtoa uhai mme wake ili afaidi mema ya nchi akiwa peke yake.

Dallila alihitaji mtu wa kutekeleza mpango wake wa kumuua Michael, hivyo aliamua kuwasiliana na mpenzi wake wa zamani na kumuuliza kama anafahamiana na mtu yeyote anayeweza kumsaidia kumtoa uhai mtu. Huyo mpenzi wake wa zamani, alimuunga kwa mtu ambaye alikuwa anaishi kwenye mji wa West Palm Beach, huko Florida. Huyu mtu alikuwa ndiye alipaswa kumpatia Dallila bunduki itakayotumika kumuua Michael. Jambo ambalo hakulifahamu ni kwamba huyu mtu alikuwa mtoa taarifa wa jeshi la polisi (informant).

Huyu jamaa na Dallila walikutana katika kituo cha kuongeza mafuta kwenye gari kuzungumza jinsi gani watatekeleza mpango wa kumtoa Michael uhai. Lakini kabla ya kukutana kwao, huyo jamaa alikuwa katoa taarifa kwa polisi kuhusu mpango wa Dallila. Polisi hawakuwa wamemuani huyo jamaa kwasababu hii habari ilikuwa ya ajabu sana na waliona haiwezi kuwa kweli. Lakini waliamua kucheza mchezo wa kung'amua ukweli ambapo waliandaa operesheni kabambe, ambapo askari mmoja ilibidi ajifanye yeye ndiye atakaye mpiga Michael risasi (hitman). Hivyo yule jamaa baada ya kukutana na Dallila alimwambia ana mtu wa kufanya kazi hiyo, kwakuwa bunduki iko tayari atamuunga naye. Hivyo akamuunga Dallila kwa huyo askari.

Dallila na huyo askari walikutana kwenye duka la vinywaji nje kwenye maegesho ya magari. Dallila akiwa anadhani huyu ndiye atatekeleza mauaji ya mumewe walianza mazungumzo. Jambo amabalo hakujua ni kwamba kwenye lile gari la huyo askari (dallila hakujua kama ni askari), lilikuwa limefungwa vinasa sauti na kamera ili kumrekodi Dallila. Askari huyo alikuwa akimuuliza Dallila maswali ya kimtego ili akili kabisa apate ushahidi. Askari aimuuliza maswali ambayo yaliwahakikishai kuwa weli Dallila alikuwa kadhamilia kumtoa uhai mume wake. Alimuuliza na uhakika wa asilimia ngapi kama kweli anataka mtu wa kumuua mume wake, na Dallila alijibu kuwa ana uhakika wa asilimia 5000. Kufikia hapa, polisi walikuwa wana uhakika kuwa kweli bi dada anataka kumuua mume wake, na pia walikuwa wana ushahidi wa kutosha wa kumkamata na kumfungulia mashitaka.

Wakati haya yakiendelea, kwa muda huo kulikuwa na kipindi cha Reality TV show kinachojulikana kama COPS. Waendesha kipindi cha COPS walisikia kuhusu tukio hili na wakaanza kuchukua matukio kisiri siri kwa kushirikiana na polisi. COPS na kikosi cha polisi walifanya kazi pamoja kutengeneza mazingira ambapo Dallila ataitwa nyumbani kwake na kuambiwa kuwa mume wake kauawa. Pale kutaonekana kuna waandishi wa habari na makamera na lengo lilikuwa kurekodi mwitikio wake ili wapate kutazama hapo baadae kujua kama mwitikio wake ulikuwa wakushtuka au wa kuigiza. Hii ingewasaidia pia Polisi wakati wa uendeshaji kesi mahakamani kuonyesha kwamba Dallila hakuwa kashtuka.

Tukio lilienda kama ilivyopangwa, Michael aliambiwa kilichokuwa kinaendela, Dallila alikuwa ashaambiwa kuwa Michael atauawa siku hiyo hivyo akajifanya ametoka kamuacha Michael nyumbani kaenda gym ili awe na mashahidi watakao kuwa tayari kusema kuwa walimuona gym. Huku nyuma Michael akaondolewa polis na COPS wakaandaa mazingira halafu akapigiwa simu kuwa kuna shida nyumbani arudi. Akaja na kufika pale anajifanya kapanic kuuliza kuna nini, akaambiwa mumewe kauawa. Kwanza akasita kidogo, baadae akaanza piga mayowe huku akilia na polisi wakimtuliza. Baadae wakamwambie waende naye kituo cha polisi kwa ajili ya kuandika maelezo, akakubali.

Walipofika kituoni, Dallila aliingizwa chumba cha mahojiano na kisha mumewe akiwa mzima wa afya akaletwa mbele yake. Mumewe akabaki amesimama pembeni yake akimtazama, huku Dalllila akiwa akipigwa butwaa kabla ya askari kumfunga pingu na kuondoka naye.

Tarehe 21, mwezi wa 7 mwaka 2017, Dallila alihukumiwa kwenda jela miaka 16 kwa kusa la kushiriki kupanga njama za kumuua aliyekuwa mume wake Michael Dippolito.

Jambo la kustaajabisha zaidi ni kwamba hii haikuwa mara yake ya kwanza kujaribu kumuua mumewe. Miaka kadhaa nyuma aliwahi kumwekea mumewe sumu kwenye chai. Hakuishia hapo aliwahi pia tegesha dawa za kulevya kwenye gari la mumewe kisha akawapigia simu polisi kisiri kama raia mwema ili wamkamate. Jambo lilimsaidia ni kwamba askari walikuta hakuna alama za vidole za michael kwenye yale madawa na pia sehemu yalipokuwa yamewekwa ilikuwa inatia shaka.

Vipi wewe unamuamini mwenza wako asilimia ngapi? Kuna mtu aliniambia eti wanawake uwa wanaamini waume zao watatangulia kufa!

Mbaki salama salmini
 
Nice story nimeipenda kwakweli nashangaa sana kuona baadhi ya wanaume wenzetu wakijimaliza kwakuwaamini wanawake zao mimi ujinga huo sifanyi naishi nae kwa taadhari sana mpk mwenyewe anajua kuwa sina mapenzi nae kiivyooooo
 
Dallila si ndiyo Delila kwa kiswahili sasa maiko alishindwaje kutambua. Maana majina mengine yanaambatana na tabia.
 
Daaaaah! Mtu anapewa kila kitu bado haridhiki
#SIOI
 
Mapenzi ya kweli ni pale K na M zinapokutana na kusigana, bila kusahau denda maridhawa.

Baada ya hapo mnabaki kama dada na kaka anything can happen including cheating.

Mkuu [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]umenifanya nicheke sana kumbe hata wewe unamaneno sana
 
Pamoja na yote mm bado nitaendelea kumuamini mke wangu hata kifo hakiwezi kututenganisha !.hizi stories nimezisikia tangu nikiwa primary tu

Mkuu hatukuzuii lkn tunajaribu kutaadharishana tu ninaushahidi wa kuona na kushuhudia baadhi ya mahusiano ya watu waliokuwa wakiaminiana sana tena mpk mwanaume anajimaliza kabisa kwa mkewe kwa kumwambia siri zake kilichokuja kutokea kumbukumbu anazo mpiga picha
 
Mapenzi hayaigwi
Mkuu hatukuzuii lkn tunajaribu kutaadharishana tu ninaushahidi wa kuona na kushuhudia baadhi ya mahusiano ya watu waliokuwa wakiaminiana sana tena mpk mwanaume anajimaliza kabisa kwa mkewe kwa kumwambia siri zake kilichokuja kutokea kumbukumbu anazo mpiga picha
 
Pamoja na yote mm bado nitaendelea kumuamini mke wangu hata kifo hakiwezi kututenganisha !.hizi stories nimezisikia tangu nikiwa primary tu

Imagine hat maandiko matakatifu waliyaona hayo na kuandika kuwa MWANAMKE MPUMBAVU ATAIVUNJA NDOA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE na pia tuliambiwa TUISHI NAO KWA AKILI sasa aisimuliaye mvua basi imemnyeshea
 
Akaja na kufika pale anajifanya kapanic kuuliza kuna nini, akaambiwa mumewe kauawa. Kwanza akasita kidogo, baadae akaanza piga mayowe huku akilia na polisi wakimtuliza. Baadae wakamwambie waende naye kituo cha polisi kwa ajili ya kuandika maelezo, akakubali.
​
 
Askari huyo alikuwa akimuuliza Dallila maswali ya kimtego ili akili kabisa apate ushahidi. Askari aimuuliza maswali ambayo yaliwahakikishai kuwa weli Dallila alikuwa kadhamilia kumtoa uhai mume wake. Alimuuliza na uhakika wa asilimia ngapi kama kweli anataka mtu wa kumuua mume wake, na Dallila alijibu kuwa ana uhakika wa asilimia 5000. Kufikia hapa, polisi walikuwa wana uhakika kuwa kweli bi dada anataka kumuua mume wake, na pia walikuwa wana ushahidi wa kutosha wa kumkamata na kumfungulia mashitaka.
​
 
Tarehe 21, mwezi wa 7 mwaka 2017, Dallila alihukumiwa kwenda jela miaka 16 kwa kusa la kushiriki kupanga njama za kumuua aliyekuwa mume wake Michael Dippolito.
Nadhani ni 20
​
 
Mapenzi ya kweli ni pale K na M zinapokutana na kusigana, bila kusahau denda maridhawa.

Baada ya hapo mnabaki kama dada na kaka anything can happen including cheating.
Nimependa comment miss kasie
 
Hahaha kuna kitu watu wanasahau, kwamba Mungu alipomfukuza shetani mbinguni alimtupa duniani.

Na huyu hakuwa kiumbe mwingine bali mwanadamu, ila kwa kuuchukia ukweli mwanadamu hataki kukubali yeye ndiye shetani naye anamsingizia ubaya shetani wakati hakuna aliyewahi kumuona kiumbe anaitwa shetani duniani.

Ila ushetani anafanya mwanadamu akihisi kuna invisible being kamu influence kutenda ubaya ule na ndiye huitwa shetani.

Sisi ni yeye tunazidiana ujasiri wa matendo yetu tu.

Huyo alijitahidi kuwa yeye yani shetani kweli.
 
Back
Top Bottom