“Mpaka kifo kitutenge” wanawake sasa wakataa kiapo hicho……….!


Hapa cha kujiuliza ni kutoa kiapo cha uongo na kumdanganya Mungu kuwa mtaishi kwa shida na raha mpaka kifo kiwatenge au kuwa wakweli kwa kufungia ndoa kwa mkuu wa wilaya na kuapa vinginevyo?

Na kwa kutoa kiapo cha kufunga ndoa kwa condition fulani, hatuoni ni bayana kuwa hakutakuwa na ubinadamu wala utu? By the way ndoa itakuwa na faida gani hapo?

Hapa nachanganyikiwa kidogo, na tukiwa na viapo vya kuishi na mpenzi mpaka penzi litakapo-eksipaya, je kutakuwa na maendeleo ya pamoja katika ndoa??? Kuna sababu ya kujenga pamoja kama hakuna uhakika wa kuishi pamoja? Kuna sababu ya kuinvest pamoja kama hakuna uhakika wa Maisha? Na pia kuna sababu gani ya kuwa mwaminifu inhali wakati wowote ndoa yenu itavunjika?? Na kwa nini kuzaa watoto watakopata usumbufu wa kuishi leo kwa mama wa kambo na kesho kwa baba wa kambo kama ndoa yenyewe ni temporari??

Hebu ngoja niendelee kutafakari nitarudi baadaye kidogo, Mtambuzi umenichanganya ...
 
Hiki kiapo kilikuwa katika kipindi cha mama zetu, siku hizi wanaume kwa wanawake wanafata masilahi tu ndani ya ndoa, japo wapo wachache wanatimiza kiapo hiki.
 
Watafiti wengi wameshindwa kubaini kuwa chanzao kikubwa cha kuenea kwa Ukimwi kwa wanandoa wengi hasa Afrika(dini ipo sana) ni kwasababu ya kiapo cha ndoa. Mtu anaona kabisa upendo umeisha lakini kwa vile hawezi kutaliki basi anakuwa na hawara......huku ndani tendo la ndoa linaendelea na nje linaendelea matokeao yake ni ugonjwa. Pia wengine wanagombana muda mrefu baadaye wanarudiana.....kumbe wakatika wa huo ugomvi mwingine tayari alikuwa na nyumba ndogo wanavyorudiana wanaambukizana na ugonjwa pia......mifano ni mingi sana.

Wazungu wenzetu hawawezi kudanganya sana nafsi zao upendo ukiisha basi tunaachana......ni mpaka pale dini zitakaporuhusu/kubali ukweli huu ndo ukimwi utaisha au kuisha......it is just a matter of time maana waliotuletea dini wao kuachana ni kitu cha kawaida....angalia akina Benny Hinn


 
Hivi wale wanaooana kwa ndoa ya kiserikali/kiislamu huwa wanaapa vipi?

Mimi naona tuna tatizo kubwa la kukosa imani. Kwa mfano, watu wanataka kufunga ndoa ya kikristo lakini kiukweli hawana imani thabiti juu ya ukristo. Yaani ni kama vile watu wanataka kufunga ndoa ya kikristo lakini hapohapo wanataka iwe na masharti kama ya ndoa ya kiserikali au wakati mwengine ndoa ya kiislamu (wake wengi)! Kwa bahati mbaya, hiyo "hybrid" kisheria bado haipo!
 
Mmh haya mambo ya ndoa mie sio mtaalamu kwa kweli nyie apeni tu mnavyoweza hata mkisema mpaka pesa itakapo tutenganisha ni sawa tu, sie wengine ni mashabiki!
 
nitang'ang'ana hadi kifo kinitenganishe Mtambuzi na alichokiunganisha Mungu kamwe mwanadamu asikitenganishe
 
Last edited by a moderator:

Thread hii ni dedication kwa MadameX ambaye anatafuta mume wa kumuoa baada ya kuchoshwa na masharobaro

Ni kweli MadameX amekataa tamaa? Mie ninataka nimtafutie kidume cha uhakika ambacho kinajua kulea mwanadada................
 
Last edited by a moderator:
nitang'ang'ana hadi kifo kinitenganishe Mtambuzi na alichokiunganisha Mungu kamwe mwanadamu asikitenganishe
nivea bado huamini tu kwamba wanandoa hufikia mahali wakabwaga manyanga?
Ni vyema kila mwanandoa ausikilize moyo wake akiona hayawezi basi hakuna sababu ya kung'ang'ania, mahakama inayo mamlaka ya kuvunja ndoa na maisha yakaendela kama kawaida.........................
 
Mtambuzi unataka nikauze haka kapete kangu au we mtambuzi weeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Last edited by a moderator:
Mie nitakuwa dalali ili nipate cha juu, we sema tu unataka shing ngapi.......................LOL

we mzee wewe badala ya kumpa mbinu ya kudumisha nanihiii................we unatafuta kubomoa afu uchukue cha juu kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…