Twinawe
JF-Expert Member
- Oct 3, 2016
- 2,431
- 5,336
Huyu binti nimekutana naye mara moja na sikuwahi kumjua kabla ila ananinyima usingizi. Juzi jumapili wakati natoka Makumbusho usiku alipanda gari nililokua nimepanda tukashuka wote Buguruni.
Nilimfata nikamwomba kama hatojali tubadilishane no kwa mawasiliano zaidi haikua rahisi nilihojiwa maswali kama naomba kazi UN.
Kishingo upande akanipa no akasema ila haipatikani akifika atawasha simu nami akasave yangu kwa simu alodai ni ya rafiki yake anatoka kuifata kwa fundi.
Tokea tulivyoachana hajanitafuta na no haipatikani. Naumia sana nawaza sana siko tayari kumpoteza na sijui wapi pa kumpata.