Mpaka leo sijaona beki wa kati kama Victor Costa "Nyumba"

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Kwa miaka 15 iliyopita katika ligi yetu ya VPL nadiriki kusema mpaka sasa sijaona beki wa kati wa kariba ya Victor Costa Nampoka "Nyumba".

Victor Costa alibarikiwa kila kitu ambacho beki wa kisasa anatakiwa kuwa navyo, kuanzia uwezo wa kumsoma adui, ukabaji, utulivu na bila kusahau matumizi makubwa ya akili. Beki pekee ambaye angeweza kuonyesha utulivu wa hali ya juu katika box lake bila kutetereka.

Kitu ambacho sijaona kwa mabeki wetu wa kizazi hiki, ambao wengi wao huwa na papara kubwa wawapo ndani ya 18 yao na huishia kubutua ili kuondoa lawama. Atleast, Pasco Wawa alikaribia kufikia walau robo ya uwezo wa Costa.

Nadiriki kusema kwa miaka 15 iliyopita sijawahi kuona beki wa kati mwenye uwezo mkubwa kama Costa, na laiti kama angepata washauri wazuri walau enzi zake angelikuwa anatamba ulaya maana naamini Victor Costa ni mahiri kuliko Chris Smalling, Per Matesaka, Samuel Umtiti au Kurt Zouma. Bahati mbaya alichezea soka lake lote hapahapa Bongo kutokana na washauri wabovu waliomzunguka.
Tunakukumbuka Victor Costa Nampoka Nyumba!!
 
kweli jamaa alikua fundi sana dimbani enzi zake kwa sasa sijui ni beki gani anakaribia uwezo wake,kuna game kati ya msumbiji alimgeuza tico tico ndani ya box jambo lililomchanganya @Maximo hadi kufumba macho
 
Beki bora Haroub Cannavaro kamuulize Samuel Etoo akiwa Barcelona kwenye ubora wake..aliwafunga All Ahly ya Misri Taifa
 
Beki bora Haroub Cannavaro kamuulize Samuel Etoo akiwa Barcelona kwenye ubora wake..aliwafunga All Ahly ya Misri Taifa
Utakuwa unasikiliza sana radio mbao! Basilika mkuu hizi sio nyakati za kumsikikiza Sued Mwinyi akikudanganya redioni.

Huyo Cannavaro anamzidi nini Costa?
Victor Costa ni wa kumfananisha na Franco Baresi au Franz Backenbeur "the kaiser"
 
Vipi kuhusu George Masatu? Naye naona alifanya vema kwa kipindi kile! Huyo Victor Nyumba kweli alikuwa fundi, alikuwa anauwezo wa kupiga vyenga ndani ya eneo la penati bila papara wala wasiwasi!

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
Kama kumbukumbu zako ziko sawa, kuna mechi moja na Senegal tushalambwa 4-0 ugenini, Victor Costa Nampoka Nyumba katika utulivu wa hali ya juu kabisaa, alimgeuza El Hadji Diouf ndani ya Box letu bila papara yoyote huku Marcio Maximo akifumba macho.

Baada ya mchezo nusu ya wachezajibwa Senegal walimfuata Costa kumpa mkono kwa mchezo wake huku Papa Bouba Diop akiomba jezi ya Costa baada ya kukunwa na uwezo wa jamaa.

Ila wachezaji wale wa Senegal walifadhaika baada ya kusikia Costa anacheza mpira Tanzania na sio Ulaya wala South Africa.
 
Nilimwona sinza nikakumbula miaka yake
 
HABARI BILA PICHA HAINOGI

Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…