mob
JF-Expert Member
- Dec 4, 2009
- 2,262
- 1,356
anafanyaka sana mazoezi pale sinza mapambanoYupoje kwasasa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
anafanyaka sana mazoezi pale sinza mapambanoYupoje kwasasa?
Ngoja waje wataalam wa picha mkuu
Naunga mkono hoja yako mkuu.Kweli Pascoal Wawa anafanana kidogo uchezaji wake na Victor Costa. Mwingine anayemkaribia kwa mbaali ni Deo Njohole (OCD). Wataalamu wengine ndio hao akina Kizota, Gaga, Nico Njohole n.k. vipaji vya hali ya juu lakini walikosa kwenda ulaya on time. Taratibu viwango hivyo vinaweza kurudi kama ufadhili, elimu na uchumi wetu ukipanda. Inafurahisha kuona akina Kaseja, Nyosso hata hao akina Chuji na Haruna Moshi wanaonyesha hamu ya kurudi viwanjani, ni dalili kuwa watu wanaanza kuona umuhimu wa kulala mbele na vipaji vyao maana maisha ya kubabaisha sasa hivi hakuna. Kama wafadhili wasipobughudhiwa na mambo ya fitna na hasa za nje ya viwanja yakidhibitiwa, tutaanza kuona tena mpira wa maana nchini.
You are a living legend!Kwa miaka 15 iliyopita katika ligi yetu ya VPL nadiriki kusema mpaka sasa sijaona beki wa kati wa kariba ya Victor Costa Nampoka "Nyumba".
Victor Costa alibarikiwa kila kitu ambacho beki wa kisasa anatakiwa kuwa navyo, kuanzia uwezo wa kumsoma adui, ukabaji, utulivu na bila kusahau matumizi makubwa ya akili. Beki pekee ambaye angeweza kuonyesha utulivu wa hali ya juu katika box lake bila kutetereka.
Kitu ambacho sijaona kwa mabeki wetu wa kizazi hiki, ambao wengi wao huwa na papara kubwa wawapo ndani ya 18 yao na huishia kubutua ili kuondoa lawama. Atleast, Pasco Wawa alikaribia kufikia walau robo ya uwezo wa Costa.
Nadiriki kusema kwa miaka 15 iliyopita sijawahi kuona beki wa kati mwenye uwezo mkubwa kama Costa, na laiti kama angepata washauri wazuri walau enzi zake angelikuwa anatamba ulaya maana naamini Victor Costa ni mahiri kuliko Chris Smalling, Per Matesaka, Samuel Umtiti au Kurt Zouma. Bahati mbaya alichezea soka lake lote hapahapa Bongo kutokana na washauri wabovu waliomzunguka.
Tunakukumbuka Victor Costa Nampoka Nyumba!!
Mzigo huo, butu butu tu.
mwehu huyo,victor costa ana kitu gani cha ajabu!..kupiga chenga kwenye boksi lake ndo ajabu,hivi kipindi hicho alimuona yule beki wa yanga mtanzania akitokea yanga!?..walimwita waziri wa ulinziUkianza kwenda uwanjani utawaona wengi tu
wewe kweli hujui mpira, Hamisi Yusuph alikuwa na jipya gani?mwehu huyo,victor costa ana kitu gani cha ajabu!..kupiga chenga kwenye boksi lake ndo ajabu,hivi kipindi hicho alimuona yule beki wa yanga mtanzania akitokea yanga!?..walimwita waziri wa ulinzi
Rwanda walitaka kumpa uraiawewe kweli hujui mpira, Hamisi Yusuph alikuwa na jipya gani?
Nadir Haroub Ali "Cannavaro"Taja beki anayemzidi Victor Costa Nampoka! Usikengeuke!