Mpaka leo sijaona beki wa kati kama Victor Costa "Nyumba"

Mpaka leo sijaona beki wa kati kama Victor Costa "Nyumba"

Ngoja waje wataalam wa picha mkuu

Kweli Pascoal Wawa anafanana kidogo uchezaji wake na Victor Costa. Mwingine anayemkaribia kwa mbaali ni Deo Njohole (OCD). Wataalamu wengine ndio hao akina Kizota, Gaga, Nico Njohole n.k. vipaji vya hali ya juu lakini walikosa kwenda ulaya on time. Taratibu viwango hivyo vinaweza kurudi kama ufadhili, elimu na uchumi wetu ukipanda. Inafurahisha kuona akina Kaseja, Nyosso hata hao akina Chuji na Haruna Moshi wanaonyesha hamu ya kurudi viwanjani, ni dalili kuwa watu wanaanza kuona umuhimu wa kulala mbele na vipaji vyao maana maisha ya kubabaisha sasa hivi hakuna. Kama wafadhili wasipobughudhiwa na mambo ya fitna na hasa za nje ya viwanja yakidhibitiwa, tutaanza kuona tena mpira wa maana nchini.
 
Naunga mkono hoja yako mkuu.
 
Kwa miaka 15 iliyopita katika ligi yetu ya VPL nadiriki kusema mpaka sasa sijaona beki wa kati wa kariba ya Victor Costa Nampoka "Nyumba".

Victor Costa alibarikiwa kila kitu ambacho beki wa kisasa anatakiwa kuwa navyo, kuanzia uwezo wa kumsoma adui, ukabaji, utulivu na bila kusahau matumizi makubwa ya akili. Beki pekee ambaye angeweza kuonyesha utulivu wa hali ya juu katika box lake bila kutetereka.

Kitu ambacho sijaona kwa mabeki wetu wa kizazi hiki, ambao wengi wao huwa na papara kubwa wawapo ndani ya 18 yao na huishia kubutua ili kuondoa lawama. Atleast, Pasco Wawa alikaribia kufikia walau robo ya uwezo wa Costa.

Nadiriki kusema kwa miaka 15 iliyopita sijawahi kuona beki wa kati mwenye uwezo mkubwa kama Costa, na laiti kama angepata washauri wazuri walau enzi zake angelikuwa anatamba ulaya maana naamini Victor Costa ni mahiri kuliko Chris Smalling, Per Matesaka, Samuel Umtiti au Kurt Zouma. Bahati mbaya alichezea soka lake lote hapahapa Bongo kutokana na washauri wabovu waliomzunguka.
Tunakukumbuka Victor Costa Nampoka Nyumba!!
You are a living legend!
 
Kuna Method Mwanjali a.k.a Baba Mwenye Nyumba, huyu jamaa ni shughuli nyingine.
 
Beki hasifiwi kwa chenga. Beki Kazi yake ni kuharibu mipango ya washambuliaji.

Victor alikua taratibusana na alikua anapenda kuchezea sana mpira, kituambacho kilimyima sifa ya kucheza nje.
Alikua anapenda mpira waa madoido ambao unachezwa apakwetu ila sio kwenye soka lililo endelea.
Nikama umuonavyo Haruna,Wengiwetu tunapenda Mpira wa majukwaaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yawezekana UKAWA uko sahihi lkn kutompa heshima yake Nadir Haroub Cannavaro ni kuukosea heshima mchezo wa soka kwa kiwango cha Tanzania.

Samwel E'too alitoa heshima yake kwa Nadir licha ya kufunga goli mbili Mpira ulivyoisha Etoo akiwa karibu katikati ya uwanja tulimuona kupitia luninga akienda kwa kasi mpaka kwa Nadir na kuomba jezi yake.

Hata kama humpendi Nadir kaitendea haki no 5 kwa Yanga na T,Stars.
Kwenda kucheza nje si washauri ni kupata nafasi sio ukurupuke utaenda nje wala uwanja hutauona.
 
Ukianza kwenda uwanjani utawaona wengi tu
mwehu huyo,victor costa ana kitu gani cha ajabu!..kupiga chenga kwenye boksi lake ndo ajabu,hivi kipindi hicho alimuona yule beki wa yanga mtanzania akitokea yanga!?..walimwita waziri wa ulinzi
 
mwehu huyo,victor costa ana kitu gani cha ajabu!..kupiga chenga kwenye boksi lake ndo ajabu,hivi kipindi hicho alimuona yule beki wa yanga mtanzania akitokea yanga!?..walimwita waziri wa ulinzi
wewe kweli hujui mpira, Hamisi Yusuph alikuwa na jipya gani?
 
tumpe costa sifa zake mpira wake ni kama rio fedinand stone,beki wa tottenham zanchez,beki chrestensen wa chelsea
 
Back
Top Bottom