Mpaka leo sijaweza kuelewa haya mambo. Nadhani hapa kuna Jambo lifanyike. Inasikitisha Sana

Mpaka leo sijaweza kuelewa haya mambo. Nadhani hapa kuna Jambo lifanyike. Inasikitisha Sana

Bill Lugano

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
1,189
Reaction score
6,450
Pengine ni sababu ya kutumia muda mwingi kuzunguka Duniani. Nchi mbalimbali. Leo nilikuwa naangalia Ramani sijui nchi gani sijafika... Mbinguni tu ndo bado. Nmeshazunguka karibia Dunia nzima.

Hivi pale kwenye lile daraja la kigamboni gari huwa wanacharge kwa kuangalia thamani yake au inakuaje? Mimi nina bahati mbaya sana huwa mara nyingi nikitoa tsh 50,000 nikiwa na Mercedes Benz wanakubali na hata receipt wanashindwa kunipa. Siku nyingine natoa 100,000 nikiwa na GMC ya mwaka 2021 nayo hawanipi receipt.

Mpaka leo sijui hasa kiwango cha kulipa sahihi kwa daraja la Kigamboni. Na ninashangaa Serikali inashindwa hata kuwasaidia wale wafanya kazi pale wawe wanatoa risiti. Maana mara zote kwangu wanakuwa hawana risiti.

Haya ni mambo madogo madogo lakini yanadumaza uchumi. Na hili suala nimeliona hata kwa Traffic mara nyingi wakinisimamisha kwa sababu ya mwendo kasi (huwa najisahau nadhani nipo barabara za nchi za wenzetu) faini zao hazieleweki.

Wakati mwingine natoa 100,000 , wakati mwingine 200,000 kuna kipindi nilitoa 500,000 maana nikiwauliza ni tsh ngapi wanajiuma uma tu sijui wanaona aibu. Hivyo huwa navuta tu draw nawapa. Wanaanza hangaika kutaka kutoa risiti mashine zao mbovu.

Nami kwakuwa nakuwa na haraka naachana nao.sasa sielewi hasa shida nini kukosekana risiti na pia kuwa na malipo au faini ambazo ni constant?

Hili daraja la Tanzanite naona hata wenye tuvitz, subaru, toyota, nissan twao nao wanakuja kupita huku. Sidhani kama ni sawa. Unakuta gari inatoa moshi (mimi gari zangu sijajua shida nini huwa zinadondosha maji kwenye exaust pipe na jamaa wengi huja kukinga wanasema matamu ya baridi) unakuta wengine na usafiri wao una toa milio ya kusumbua samaki baharini. Nadhani pale pangewekwa tu utaratibu wa kulipia tsh 200,000 kuvuka.

Ili tuwe tunatumia sisi wenye magari na mambo ya msingi ya kufanya Mjini
Mfano pale Kigamboni kwa sisi wenye magari tukitozwa tsh 100,000- 200,000 si mbaya. Na wale wenye usafiri wawe wanalipa tu flat tsh 50,000. Maana nikiangalia lile daraja kwa nchi hii maskini walitumia pesa nyingi. Ndio maana huwa naona kuna askari wanalilinda lisije likaibwa. Ni jambo zuri lakini.
 
Kiduku lilo a.k.a Bill Lugano..

Vipi kwako mafuta hayajapanda bei.???
Maana sisi walala hoi tunalia mkuu..
 
Tajiri.... Tunashukuru kwa mchango wako mkubwa katika ujenzi wa Taifa hili Changa. Kuna proposal nataka nikutumie. Je naweza kupata email add yako. Ni proposal nzuri sana kama mtaji upo....
 
Kidogo niamin ila ulipo sema gari lako linatoa maji na watu wanakinga na wanasema ni matamu nikaamin hii ni chai ya mwarobaini
 
Pengine ni sababu ya kutumia muda mwingi kuzunguka Duniani. Nchi mbalimbali. Leo nilikuwa naangalia Ramani sijui nchi gani sijafika... Mbinguni tu ndo bado. Nmeshazunguka karibia Dunia nzima.

Hivi pale kwenye lile daraja la kigamboni gari huwa wanacharge kwa kuangalia thamani yake au inakuaje? Mimi nina bahati mbaya sana huwa mara nyingi nikitoa tsh 50,000 nikiwa na Mercedes Benz wanakubali na hata receipt wanashindwa kunipa. Siku nyingine natoa 100,000 nikiwa na GMC ya mwaka 2021 nayo hawanipi receipt.

Mpaka leo sijui hasa kiwango cha kulipa sahihi kwa daraja la Kigamboni. Na ninashangaa Serikali inashindwa hata kuwasaidia wale wafanya kazi pale wawe wanatoa risiti. Maana mara zote kwangu wanakuwa hawana risiti.

Haya ni mambo madogo madogo lakini yanadumaza uchumi. Na hili suala nimeliona hata kwa Traffic mara nyingi wakinisimamisha kwa sababu ya mwendo kasi (huwa najisahau nadhani nipo barabara za nchi za wenzetu) faini zao hazieleweki.

Wakati mwingine natoa 100,000 ,wakati mwingine 200,000 kuna kipindi nilitoa 500,000 maana nikiwauliza ni tsh ngapi wanajiuma uma tu sijui wanaona aibu. Hivyo huwa navuta tu draw nawapa. Wanaanza hangaika kutaka kutoa risiti mashine zao mbovu.

Nami kwakuwa nakuwa na haraka naachana nao.sasa sielewi hasa shida nini kukosekana risiti na pia kuwa na malipo au faini ambazo ni constant?

Hili daraja la Tanzanite naona hata wenye tuvitz,subaru,toyota,nissan twao nao wanakuja kupita huku. Sidhani kama ni sawa. Unakuta gari inatoa moshi (mimi gari zangu sijajua shida nini huwa zinadondosha maji kwenye exaust pipe na jamaa wengi huja kukinga wanasema matamu ya baridi) unakuta wengine na usafiri wao una toa milio ya kusumbua samaki baharini. Nadhani pale pangewekwa tu utaratibu wa kulipia tsh 200,000 kuvuka.

Ili tuwe tunatumia sisi wenye magari na mambo ya msingi ya kufanya Mjini
Mfano pale Kigamboni kwa sisi wenye magari tukitozwa tsh 100,000- 200,000 si mbaya. Na wale wenye usafiri wawe wanalipa tu flat tsh 50,000. Maana nikiangalia lile daraja kwa nchi hii maskini walitumia pesa nyingi. Ndo maana huwa naona kuna askari wanalilinda lisije likaibwa. Ni jambo zuri lakini.
Huyu Bill Lugano ndio nani jamani mbona anatonesha madonda sana yaani kula tu Mimi napata taabu lakini yeye anazungumzia fine 500000! Duuuh jamani kweli Mungu ametutenga madaraja [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Nachoka kabisaaa.... Huyu mwamba huwa namkubali sana kwa maisha yake. Nami nikipata pesa nitakuwa kama yeye....matajiri wa hivi wachache sana aisee .......
 
Huyu Bill Lugano ndio nani jamani mbona anatonesha madonda sana yaani kula tu Mimi napata taabu lakini yeye anazungumzia fine 500000! Duuuh jamani kweli Mungu ametutenga madaraja [emoji848][emoji848][emoji848]
Watu wanasumbuliwa na Mwigulu na matozo ya kipumbavu yy analeta utani! Kuwa serious basi!
 
Back
Top Bottom