Sote tumekuwa Mashuhuda wa matukio mbalimbali katika soka yanayofanywa na marefaree wetu hapa Bongo. Imefika mahala mechi zinaharibika kutokana na utashi mdogo wa watu hawa katika kuchezesha soka. Watu hawa muhimu kabisa katika soka ndo wamekuwa vinara wa kutuharibia soka letu.
Ukianza kuchambua ni matukio mengi sana ya ajabu yanayofanywa na waamuzi wa soka kote nchini. Swali ni je,hawana uelewa na sheria za mchezo huu? Je ni wageni katika mchezo huu?
Kwa uchunguzi wa haraka haraka ,nimekuja kugundua kuwa wengi wao wanamahaba na timu flani flani hapa Bongo,ndio maana wakipewa dhamana ya kuendesha michezo inayoambatana na timu zao wanaambulia kuharibu mechi, kwa mbeleko za mbao.
Je, hiyo ni sababu tosha kwako mpenda soka? Je, Unahisi nini chanzo cha uhaini huu katika soka letu?
Nini mchango wako (Tuchukue hatua gani kwa vilaza hawa).
#jr