Ndugu zangu Watanzania, kila mmoja wetu ameshuhudia wimbi kubwa la utekaji, utesaji na mauaji hapa Nchini hasa kabla na wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.
Mimi niwaombe wanaotekeleza mambo haya, waangalie zaidi UBINADAMU na UTANZANIA wetu. Tofauti ya vyama vyetu isiwe sababu ya kuuana kwetu. Naomba tusitafute ushindi wa kishindo kwa kumwaga damu za wasio na hatia. Inashangaza sana kuona kila Halmashauri, Wilaya na Mkoa kila mmoja anataka ushindi wa uchaguzi wa 100%. Nadhani hii ndo inayopelekea Madhira haya.
Kuna shida gani kama mtu atapata ushindi angalau kuanzia 75% na kuendelea? Mbona wakati wa J.M. Kikwete iliwezekana? Je, alipungukiwa na nini kwa ushindi wa kiwango kile? Katika hali ya kawaida haiwezekani wapiga kura wote Tanzania nzima wakakipigia kura chama kimoja tu na kukipa ushindi wa 100%.
Naomba sana, watawala wetu wajitathmini. Kupitia tu uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita juzi juzi hapa kumejengeka chuki ya hali ya juu sana baina ya Watanzania kwa Watanzania na Watanzania na watawala.
Hali hii haileti afya kwa Taifa letu.
Nawasilisha.