Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kutoka kwa Muliro, IGP Wambura wala Waziri Masauni juu ya utekwaji wa Sativa, kuna nini?


Suku hizi wote wanajifanya CHURA... Zamani ilikuwa ni maelekezo kutoka juu.
 
ni muhimu akaripoti kituo cha polisi. kuripoti mtandaoni na kwenye vyombo vya habari sidhani inatosha na kama ndio utaratibu 🐒
 
Kuuliza sio Ujinga,
Sisi wakazi wa Ibologelo, Nata, Igogo, malendi, ulemo, iguguno shamba, kizonzo, jojo, sipongwe, chombe, chumvi, chokaa, santilya, Galula, kapunga , isamgawana, mtanila, mafyeko , mbawe, Sakukwa, sangambi, kiwanja, Chalangwa. Kwani huyo Sativa ni nani na anajihusisha na nini?.
Historia yake walau kidogo
 
Jeshi la polisi ni kikundi cha wahuni kinachohitaji mamlala huru kulisimamia, kwa sasa wapo huru kutumika na wanasiasa na wahuni pia, mimi sina imani nao nasitakuja kuwa na imani nao
 

Hao wote uliowataja ni sehemu ya huu ushetani unaosimamiwa na kulindwa na CCM na Serikali nzima ya CCM. Tunaongozwa na mashetani. Bila ya kuondokana na hawa mashetani, watanzania wataendelea kudhulumiwa haki zao za kuishi.

Kumbukeni mkuu wa Serikali aliwahi kutamka kuwa polisi wa serikali ya CCM wakimlenga mtu hawawezi kukosa kumwua.
 
Ni kati ya wakosoaji wakuu wa uozo ndani ya serikali na baadhi ya wakuu wa Serikali kuoitia mtandao wa X.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…