Uchaguzi 2020 Mpaka sasa Halima Mdee ameshashinda Jimbo la Kawe, Dar-es-Salaam

Gwajima mweupe sana kwenye siasa ,CCM wanafikiri waamini wa gwajima ndio wapiga kura bila kutambua waamini wake wengi sio wakazi wa jimbo la kawe.
Hakuna mtu hatari kwenye Siasa kama mtu ambaye ni mgeni kwenye siasa na pia hana hata ule umaarufu wa kisisasa lakini ana strong social ties na jamii ya watu wanaomzunguka! Ogopa sana kwenye Siasa ukikumbana na mtu wa aina hiyo. Hawa ni aina ya watu kana akina Sugu na {Prof. Jay
 
Halima keshaondoka hapo ingawaje nampenda sana yule dada. Haogopi na anajiamini ila kwa huyu mtu aliyeweka, kazi anayo. Pesa , kuongea na ushawishi.
Hapana siyo kwamba anajiamini. Ana over-cinfidence ile yenye nyongeza ambayo huwa anadhani kuwa asipokuwa nayo atadharauliwa kwa sababu yeye ni mwanamke, kumbe hapana. Unajua ile kuongeza kitu kuziba na ua kuficha hofu uliyonayo. Hiki ndicho huwa kinawaharibu baadhi ya watu, especially wanawake. Kama ni mwanaume, kuwa tu katika ile hali ya kawaida mwanaume anavyotakiwa kuwa, vile vile pia kama ni mwanamke. Saa ukitaka kuongeza tena na u-shoka, mwanaume wa shoka, mwanamke wa shoka; lazima tu uharibu
 
Halima keshaondoka hapo ingawaje nampenda sana yule dada. Haogopi na anajiamini ila kwa huyu mtu aliyeweka, kazi anayo. Pesa , kuongea na ushawishi.
Udini umemaliza Gwajima aliahidi kuzigeuza madrasa kuwa Sunday school. Aliwahi kuonesha kwa kauli yake kuchukizwa na ongezeko la waislamu duniani
 
Mjadala umekuwa mkali sana..
kwanza kabisaa Gwajima ana waamini wake wanaotoka nje ya kawe na ndani ya kawe labda, na anaweza kuwa amefanikiwa kuwa na waamini kwa njia anazojua yeye mwenyewe na Mungu wake. Uwezo wa kuongea kwenye makanisa kwa kufoka sidhani au siamini kuwa ndo iwe hoja ya ushindi katika uchaguzi. Kawe ni jimbo ambalo lina watu educated na wanaojielewa sana tena katika kufikiri.

Mdee nae ana mtaji wake kawe maana ana miaka 10 pale kama mbunge toka upinzani au mbunge wa vigogo.

Point yangu ni hii. Kama tatizo la kawe ni HALIMA MDEE basi Gwajima atashinda, lakini kama tatizo la kawe ni CCM basi halima mdee atendelea kuwa mbunge wa kawe ..
 
As long as ameweza kupenya na kuwa mgombea mteule kwa ticketi ya CCM liwake jua au inyeshe mvua Gwajima anaenda kuwa Mbunge kuwakilisha jimbo la Kawe!

Gwajima ni mchapa kazi atawakilisha vyema wananchi.

Ndani ya muda mfupi mtaanza kuona mabadiliko ya maendeleo jimboni.

Nachelea kusema ni bahati na Tunu kumpata mtu mwenye kariba ya Gwajima kuwa mbunge wa jimbo la Kawe .

Wanakawe msichezee shilingi chooni!

Gwajima is the best person to represent wananchi wa Kawe.
 
Tatizo Mdee hana jipya,

Kwa miaka 10 sijui na zaidi amefanya nini? [emoji2369][emoji2369]

Kwanza mimi binafsi ni muumini wa mabadiliko,

Scientific research has proven that changes lead into improvements always.

Kwanini kuendelea kumng’ang’ania Mdee miaka yote hiyo kama hakuna watu wengine wazuri?

Hapana tunataka mabadiliko.

Vinginevyo CDM walipaswa kuleta mtu mwingine kama John heche na siyo Halima ambae kimsingi amechoka kufanya kazi za kibunge jimboni!

Gwajima is the best !
 
Uzuri wa Gwajima ana access hata ya kufika Ikulu iwapo kero imekithiri akaenda kumuona CEO wa nchi kupata ufumbuzi.

Gwajima ni king’ang’anizi wa utendaji atafaa sana.

Ni bahati sana kupata Mbunge kama Gwajima.
 
Nakumbuka mwaka 1995 pale Musoma Nyerere alisema angekuwa yeye ndo anapiga kura angempigia Wandwi wa NCCR,tukajua hapa CCM Chali lakini kilichokuja kutokea acha tu
 
Ila hao wasomi wanapenda wenye tuhuma za kusagana?! Mbona ni yale yale! Tutumie vigezo vingine tu.
 
Ila hao wasomi wanapenda wenye tuhuma za kusagana?! Mbona ni yale yale! Tutumie vigezo vingine tu.
Una ushahidi wa hizo tuhuma za kusagana????

Ukitaka ushahidi wa clip za Gwajima kuhamasisha ukabila utapata, ukitaka ushahidi wa clip ya Gwajima akikata mauno na binti kitandani ipo!!!

Sasa wewe unasema jambo lipi hasa la ajabu????
 
Una ushahidi wa hizo tuhuma za kusagana????

Ukitaka ushahidi wa clip za Gwajima kuhamasisha ukabila utapata, ukitaka ushahidi wa clip ya Gwajima akikata mauno na binti kitandani ipo!!!

Sasa wewe unasema jambo lipi hasa la ajabu????


Wewe unaweza kuthibitisha kuwa yule alikuwa Gwajima?


Vipi kama ilikuwa ya kutengenezwa na wasiomtakia mema kutaka tu kumpaka matope?

Walioitengeneza zile picha za ngono kumchafua Gwajima Mwenyezi Mungu ameanza kuwashughulikia !


Watu wanataka chapakazi na kwa sasa ni Gwajima kwa Kawe!
 
Naunga mkono hoja yako kwa asilimia mia moja ila bado nashanga ccm wakubwa hawalioni hili?
 
Hii ni hoja maarufu sana wanayotumia baba wachungaji karibu wote wakibanwa na ushahidi juu ya maovu wayafanyayo gizani, lakini kwa teknolojia ya sasa hivi ni rahisi sana kujua kama ilikuwa ya kutengenezwa au la
 
Ni ukweli usio semwa kwamba kuna factors nyingi zaidi ya kutoka CCM ama Chadema. Kila jimbo lina mambo yake, kwa CCM kumteua Mchungaji Gwajima, uchaguzi wa Kawe utakuwa wa kidini zaidi kuliko kisiasa. Kuna tofauti kati ya kuwa mkristo na kuwa Kiongozi wa wakristo. Inapokuwa kiongozi wa dini fulani anasimama kugombea nafasi ya kuwa kilisha watu wa dini zote huwa ni ngumu sana upande wa dini nyingine kumkubali. Kwa mtazamo wangu hili la Mch Gwajima halikuangaliwa kwa mapana yake hasa ukizingatia Dar-es-Salaam ni jamii iliyochanganyika sana kidini.
 
Ikitokea Shekhe mwenye uwezo wa kuwakilisha watu mfano Shekhe Issa Ponda watu wa dini zote na wapagani watamuunga mkono sababu atatumikia wananchi wote.

Si vema kutaka kuleta udini.

Ndiyo maana hata Rais wa dini nyingine anakubalka lakini anatumkia wananchi wa dini zote na wapagani na mambo yanaenda vyema!
 
Haya mbashiri wa kisiasa... Naona umeamua kufanya kazi ya sanduku la kura.
 
Naunga mkono hoja yako kwa asilimia mia moja ila bado nashanga ccm wakubwa hawalioni hili?
Vuta picha mtu kama Dr Bashiru au Kate Kamba; watu wenye hadhi zao kwenye jamii wamepanda jukwaani wana mnadi Gwajima ni mtu safi na mwenye maadili yanayofaa CCM si kujishushia heshima zao tu.

Kate Kamba mtoto wake ni mganga Mkuu wa mkoa wa Tabora, kesho apande jukwaani atuambie tapeli aliejitapa anaweza fufua wafu ni mtu mwenye maadili si kujidhalilisha tu mbele ya familia yake.

Makampuni makubwa tu leo awataki kuhusishwa na wasanii waliokosa maadili; iweje taasisi inayoongoza nchi ishindwe kuona hilo ni tatizo kisa kura.
 
Vuta picha mtu kama Dr Bashiru au Kate Kamba wamepanda jukwaani wana mnadi Gwajima ni mtu safi kujishushia hadhi zao tu.
Daaah pengine wanatujua zaidi wanakawe kuliko tunavyojijua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…