GE2025 Mpaka Sasa sijaona hoja za kiuchumi kutoka kwa wagombea urais mwaka huu

GE2025 Mpaka Sasa sijaona hoja za kiuchumi kutoka kwa wagombea urais mwaka huu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
25,522
Reaction score
40,795
Niseme ukweli, ni kwamba mpaka Sasa sijaona au kuridhika na hoja za kiuchumi za wagombea urais wakiichukua fomu INEC mwaka huu. Hakuna mgombea urais aliyeonesha namna atakavyo ikwamua Tanzania kiuchumi.

Wagombea urais wengi wanahoja za kawaida au za kufurahisha hadhira. Wengine wanadai watatumia leseni watu kulewa, wengine wanadai lazima kila mtanzania ale ubwabwa, wengine wanadai lazima mtanzania anywe maziwa glasi moja kila siku na wengine wanadai kila polisi lazima ajenge ghorofa na kumiliki VX. Mwingine anasema utu na kazi wakati watu wanashushwa kwenye basi na kuuawa na yeye kudai kifo ni kifo. Utu upo wapi kama sio uongo?

Cha kusikitisha Kuna mgombea mmoja yeye alidai akipewa urais atakuwa anavaa t-shirt na jeans na kutembea mitaani. Hili ni jambo la kawaida kwa Rais sio priority ya kufanya ugombee urais. Kipaumbele chako Cha kuutaka urais ni nini? Kuna mgombea Urais yeye kasema akipata urais atapiga marufuku vitanda vya SITA kwa SITA.

Nadhani wananchi wanahitaji wagombea ambao watakuja na slogans au sera zenye kuonesha mwelekeo chanya wa Taifa lao kiuchumi. Ni namna gani deni la Taifa litapunguzwa, namna gani tatizo la ajira kwa vijana litashughulikiwa, pensheni kwa wastaafu, masuala ya Kodi na Tozo etc. Mpaka Sasa hakuna mgombea ambaye ameonesha mwelekeo mpya wa kuwafanya wananchi wahamasike kwenda kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais mwaka huu.
 
Screenshot_2025-08-22-16-30-59-1.png
Screenshot_2025-08-22-16-27-32-1.png
 
Back
Top Bottom