Mpaka sasa sijaona wa kumfananisha na Mzee Dossa Aziz Ally Tanzania hii

Mpaka sasa sijaona wa kumfananisha na Mzee Dossa Aziz Ally Tanzania hii

S
Mzee Dossa Aziz Ally wakati wa uhai wake alikuwa mtu mwenye utu, upendo, mkarimu, mwenye subra, mtulivu, mwenye imani,aliyejaa amani, mpenda haki, aliyetetea usawa akaishi salama.

Uzalendo wake mkubwa aliokuwa nao wa kutoa na kujitoa kusuka mikakati ya ukombozi na kutumia mali zake kwaajili ya ukombozi wa Tanganyika ulimfanya Dossa atambulike bila kujitambulisha Dossa alifanikiwa kuondoa dhana ya adui uoga wa kufilisika kwenye akili yake, akabeba mafanikio ya wengi. Alijua kuwa mtu muoga ni mtu aneishi kwaajili yake tu. Kwa kufanya hiyvo alitimiza lengo la uwepo wake hapa duniani la kufanikisha maisha ya wengi, na yeye akavuna umilele. legacy yake kubwa kwa Tanganyika ndiyo inamfanya asisahaulike unapoutafuta ukweli kuhusu historia ya ukombozi wa Tanganyika.

Mzee Dossa pamoja na kutumia mali zake katika kujenga TANU na ukombozi wa Tanganyika, hali iliyomfanya aitwe Bank na badae kufa masikini, hakulalamika, hakusikitika,wala hakujuta kutoa mchango wake huo katika kuiletea nchi yake Uhuru, kwani usipotarijia mengi kutoka kwa watu mfadhaiko wako ni kidogo na ukitarajia mengi kutoka kwa Mungu hautofadhaika kabisa.

Dossa ni nani?Waziri Dossa Aziz Ally ali-maarufu kwa Dossa Aziz alikuwa mwanachama wa TAA na badae TANU akimiliki kadi namba 4 ya TANU, huku kadi namba 1 ikimilikiwa na Mwl Nyerere, Ally Skyes namba 2, kadi namba 3 alimilik Abdulwahid Skyes na John Rupia alimiliki kadi namba 7. Ni mtoto wa kwanza wa Ally kidonyo ali-maarufu kwa Aziz Ally "Aziz" ikibeba maana ya mpenzi yaani aliitwa kipenzi chetu Ally na wakazi wa Mzizima enzi hizo kutokana na wema na ukarimu wake aliokuwa nao, jina ambalo lilipelekea kupotea kwa jina lake la asili la Kidonyo.

Dossa Aziz ni mdigo kutoka Tanga aliyezaliwa na kukulia Mzizima (kwa sasa Dar es salaam) mtaa wa mtoni kwa Aziz miaka ya 1920. Baba yake aliyekuwa askari wa kijerumani aliyepigana vita vya kwanza vya dunia na tajiri mkubwa Dar er salaam enzi hizo alimzuia asiende shule ili apate elimu ya qur'ani hadi alipofikisha umri wa miaka 14.

Asili ya utajiri wake
Utajiri wa kurithi wa Dossa kutoka kwa baba yake na sifa zake mwenyewe zilimtambulisha kwa uzuri sana Dar es salaam. Baba yake mzee Aziz Ally alikuwa miongoni mwa matajiri Waafrika wakubwa na mtu wa kwanza Tanganyika kununua gari, alikuwa mkandarasi wa majengo wakati wa ukoloni hivyo baada ya kifo chake 1951, ukiacha pesa, mzee Azizi Ally aliacha urithi wa nyumba nyingi katika maeneo mengi Dar es salaam, magari ya kutembelea na magari saba ya kubebea kokoto na mchanga. Dossa ndiye aliyerithi mali hizo kwasababu alikuwa mzawa wa kwanza wa mzee Aziz Ally. Rafiki zake wanasema walikuwa wakimuona Dossa ameingia kila mtu anapumua kwani watakula na kunywa kwa furaha hadi wakampa jina la utani, ‘’The Bank.’’

Umuhimu wa Dossa kuelekea Tanganyika huru
Dossa alianza kuingia kwenye harakati ya siasa ya ukombozi wa Tanganyika tangia enzi za Tanganyika African Association (TAA) kipindi hicho chama kiliongozwa na Mwalimu Thomas Plantan kama Rais na mzee Clement Mtamila akiwa katibu, baada ya chama kuzorota na kukosa malengo ya kudai uhuru wa Tanganyika. Dossa na wenzake akina Abdulwahid Skyes, Hamza mwapachu na Dr Vedasto Kyaruzi walifanya mapinduzi ya uongozi wa TAA na kumfanya Abdlwahid skyes kuwa katibu wa TAA na Dr Vedasto kuwa rais.

Mwalimu Nyerere alipofika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza mwaka wa 1952 kama mwalimu wa shule ya St. Francis (kwa sasa Pugu Sekondari) hakuna mtu aliyekuwa anamjua au kupata kusikia habari zake katika ulingo wa siasa. Kassela Bantu ambaye alikuwa akijuana na Nyerere kwa siku nyingi alimtambulisha Nyerere kwa Abdulwahid Sykes. Wakati ule Abdulwahid alikuwa Rais wa TAA. Nyerere mara moja akajiunga na baraza la siasa lililokuwa likifanyika Mtaa wa Mbaruku nyumbani kwa Dossa. Ikawa kila Jumapili Nyerere anakuja kutoka Pugu kumtembelea Dossa. Doss, alikuwa anawapitia viongozi kwenda kwenye mkutano. Akipiga honi ili mtu atoke waende mkutanoni.

Mwaka 1951, Dossa Azizi pamoja na wapigania Uhuru wenzake mashuhuri akiwemo chifu Kidaha makwaia, Liwali Yustino Mponda wa Newala, DrJoseph Mtahangarwa, chifu Abdiel Shangali wa Machame, chifu Thomas Marealle wa marangu, chifu Adam Sapi Mkwawa, chifu Harun Msabila Lugusha, Dr William Mwanjisi, Abdulkarem Karimjee, Dr Vedasto Kyaruzi, Liwali Juma Mwindadi, Stephen Mhando, Ally Skyes na Abdulwahid Skyes, alikataa mpango wa ghiliba uliosukwa na aliyekuwa mjumbe wa baraza la kutunga sheria la kikoloni V.M Nazerali, akimuomba awashawishi wenzake kuunga mkono juhudi za chama kingine tofauti na chama cha TAA kilicholenga kusimamia ukombozi wa Tanganyika.
Baadae 1953 Dossa Aziz, Abdulwahid Skyes, Ally Sykes, John Rupia na Julius Nyerere waliunda kamati ya siri kuifanya TAA chama kamili cha siasa na badae kuundwa kwa TANU julai 7, 1954.

Dossa alitoa pesa mfukoni mwake kulipia bili kila siku" princes hotel Mnazi mmoja" sehemu ambako Nyerere na wenzake walipatumia kuhutubia wanaTANU na badae kupongezana na kufanya tathimini ya chama. Alifanya hivo bila kuchoka kwa miaka yote hadi Tanganyika ilipopata uhuru chini ya uongozi wa Mwl Julius Nyerere. Dossa alikuwa mfadhili mkubwa wa TANU kipesa, kwanza alianza kuwa dereva wa mwl Nyerere akimuendesha sehemu mbalimbali za nchi kuhubiri ukombozi wa Tanganyika mpaka TANU ilipokuja kumwajiri Said kamtawa kuwa dereva wa Mwl Nyerere.
Dossa, ndiye aliyetoa gari yake kuipa TANU na badae ikaja kuwa gari ya mwanzo kumilikiwa na TANU katika shughuli zake za kuikomboa Tanganyika kutoka kwa Waingereza. Nyumbani kwa Dossa ndiko palipokuwa na baraza la TAA mahali ambapo Nyerere pamoja na wanasiasa Waafrika walikutana kila Jumapili kupanga mikakati ya kumng’oa Mwingereza katika ardhi ya Tanganyika. Na hapa ndipo pia mwl Nyerere alijifunzia siasa, na Dossa akamwambia Mwl asivae tena kaptula na sokisi ndefu mpaka magotini mbele za watu, kwani tayari alikuwa mtu mwenye ushawishi na alikutana na watu wa aina tofauti wenye heshima.

Dossa akiwa na Mwl Nyerere ndio walioasisi wazo la kuanzisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Nyerere alimwambia Dossa, “Dossa tukipata uhuru wetu hapa lazima tujenge Chuo Kikuu.” na kweli baada ya uhuru wazo hilo lilifanyiwa kazi na chuo kikuu kikajengwa kwenye kiwanja cha John Rupia alichokitoa kwa TANU. 1955 wakati TANU ilipomtuma mwl Nyerere kupeleka ujumbe wa kudai uhuru wa Tanganyika umoja wa mataifa, Dossa ndiye aliyejitolea kumnunulia Nyerere suti kadhaa maridadi, na baade mwl Nyerere aliporejea nchini kutoka Umoja wa mataifa alikokwenda kudai uhuru wa Tanganyika, alikuta umati mkubwa wa wananchi unamsubiri uwanja wa ndege. Haikuwezekana kwake kutoka nje ya uwanja jinsi umati wa watu ulivyojazana kumlaki. Walinzi wa kikoloni walimruhusu Dossa aingize gari yake hadi chini ya mlango wa ndege. Nyerere akashuka na kupokelewa na swahiba wake Dossa na akaingia ndani ya gari la Dossa.

Mzee Dossa Aziz, ndiye aliyejitolea kumlipa mshahara wa kila mwisho wa mwezi Mwl Nyerere hadi Tanganyika ilipopata uhuru kuanzia 1955 hadi 1960, baada ya Father Walesh mkuu wa shule ya saint Francis kwa sasa Pugu sekondari alipokuwa akifanya kazi Julius Nyerere kama mwalimu kumwambia achague moja kati ya siasa na ualimu.
Ufa Kati Dossa Na Nyerere.

Baada ya Uhuru, urafiki uliodumu kipindi chote cha kudai uhuru wa Tanganyika kati Dossa na Nyerere ulianza kufifia 1962. Pale Mwl Nyerere aliposhauri baraza la wazee wa TANU ambalo wajumbe wake wengi walikuwa waislamu liongozwe na waislamu waafrika, likahisi Nyerere alikuwa akiuhujumu uislamu. jambo hili liliibua mgogoro wa kidini kati ya Waislamu na serikali na kupelekea halmashauri kuu ya TANU kuvunja Baraza la Wazee wa TANU kwa kile kilichodaiwa kuchanganya dini na siasa.

Nyerere taratibu aliwahama marafiki na wahimili wake wa siku za awali na akaanza kujenga nguvu mpya kutoka kwa wasio Waislamu kwa hofu ya kuwa akiwa karibu na waasisi wa TANU ambao wengi wao walikuwa Waislamu akiwemo mzee Dossa Aziz, Ally Mwinyi Tambwe, Iddi Faizi Mafongo, Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Abdalla Iddi Chaurembo, Sheikh Suleiman Takadir, Ibrahim Hamis, Abdulwahid Sykyes, Ally Sykyes na wengineo, kungehatarisha amani na usitawi wa taifa changa la Tanganyika huru. Na huu ndo ulikuwa mwanzo mbaya wa kufutika kwa hisitoria ya wazalendo wengi waliojitolea maisha yao kuupigania uhuru wa Tanganyika ambao wengi wao walikuwa waislamu.

Katika kudhihirisha kufifia kwa urafiki kati ya mwl Nyerere na Dossa Aziz, 29 April 1985 mwl Nyerere alipokuwa anang'atuka na kuwa baba wa taifa, alitoa medali 3979 kuwatambua mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika, kati yao ni Sheikh Abdallah idd chaurembo peke yake alipewa heshima hiyo huku Dossa na rafiki zake akina Abdulwahid skyes hawakupata medali hizo.Lakini baadae mwl alistuka na kumuita Dossa faragha ikulu kumtambua kama miongoni mwa mashujaa wa ukombozi wa nchi.

Dunia Mapito
Waswahili husema, Dunia haikuwa sawa, haiko sawa na haitokuwa sawa, Dossa mtu aliyekuwa na mali katika miaka ya 1950 aliishi katika hali ya ufukara baada ya Uhuru wa Tanganyika, akiishi maisha ya upweke kwenye nyumba ya udongo kijijini kwao Mlandizi.Hali hii ya ufukara ilitaka kumkosesha kuhudhuria Mkutano Mkuu wa CCM mwaka1987 pale Kizota Dodoma, ambapo waasisi wote wa TANU walialikwa. Sababu kubwa ilikuwa ni ukosefu wa nguo na viatu vya kuvaa katika hadhara kama hiyo. Ilikuwa mmoja wa marafiki zake wa zamani Abbas Sykes ndiye aliyemnunulia nguo na viatu vya kumwezesha kwenda Dodoma

Kwaheri Dossa, kwaheri shujaa
Baada ya masumbufu ya miaka mingi ya mateso na maisha mapya ya ufukara aliyopitia akiwa Mlandizi, Mzee Dossa alifariki dunia machi 10 1998 akiwa na umri wa takribani miaka 78 kwa maradhi ya uzee huko Mlandizi Kibaha. Akaiacha Tanganyika na Tanzania huru na yenye amani.

Dossa amliza Nyerere
Maisha ni safari ndefu, maisha ni fumbo la imani, maisha ni mtihani, maisha ni ahadi, na maisha ni mipango maana kuna kuchagua. Mzee Dossa aliishi safari ndefu ya ukombozi wa Tanganyika, akafumbua fumbo la utumwa wa Tanganyika kwa kushiriki harakati za kudai Uhuru akafanikiwa, akafanya mtihani wa kujitoa sadaka kwa hali na mali kuhakikisha Uhuru unapatikana akafaulu,aliahidi kutokata tamaa katika kudai Uhuru wa Tanganyika akashinda, na akachagua kuwa mzalendo kwa nchi yake kwa kutoa mali zake kwa faida ya nchi na Watanganyika kwa ujumla ikawa, leo hii hatunae tena kimwili lakini legacy yake inazungumza nasi kutukumbusha kuwa tulisahau na tumesahau kumpa mwisho mwema shujaa huyu wa harakati za ukombozi wa Tanganyika.

Mwalimu Nyerere mwenyewe siku ya Jumapili tarehe 19 Aprili 1998 katika khitma ya marehemu nyumbani kwa Dossa pale Mlandizi wakati Nyerere aliposimama kusema machache katika hadhara ile kuhusu uhusiano wake na Dossa na mchango mkubwa wa marehemu Dossa Aziz katika kuleta uhuru wa Tanganyika. Nyerere alisema kuwa hata siku moja Dossa hakupata kumuomba kazi au kuonyesha dalili za kutaka ukubwa. Mwalimu Nyerere aliposema maneno haya alibubujikwa na machozi na waliokuwepo nao walilia kwa huzuni. Subira aliyokuwa nayo Dossa ndiyo sababu kubwa iliyomfanya astahamili dhiki kwa miaka yake ya mwisho ya uhai wake na afe masikini katika hospitali ya Tumbi, Kibaha.


Risky 2X
Sema kweli
 
Baba yake alimpeleka madrsa kusoma Quran halafu kuna Mijitu inataka Mwl Nyerere a mpatie ukuu wa mkoa
Na yeye kusoma Quraan wewe imekukera sana au sio?
Ungesikia kasoma Ufunuo na galatia ungeskia raaaha.
Makafiri mna laana ya Mungu. Mnaugua maradhi mabaya kwa roho zenu mbaya.
Haya Corona hio . Nyie si mmesoma? Tuleteeni Tiiba basi sisi watu wa madrasa tunasubiri.
Laanatullahi wahedi.

.
 
Na yeye kusoma Quraan wewe imekukera sana au sio?
Ungesikia kasoma Ufunuo na galatia ungeskia raaaha.
Makafiri mna laana ya Mungu. Mnaugua maradhi mabaya kwa roho zenu mbaya.
Haya Corona hio . Nyie si mmesoma? Tuleteeni Tiiba basi sisi watu wa madrasa tunasubiri.
Laanatullahi wahedi.

.

Laana ipo kwa wasiolijua neno
 
Mkuu sijui niseme hii ni '' shoot oneself in the foot'' au ni ''own goal'' sijui
Nimeweka hizo nukuu ili tuone kazi za pacha, Pacha leo(P-Leo) na Pacha mzoefu sana (P-MS)

1. Wote wanakubaliana Mwalimu alifika Dar mwaka 1952 kwa mara ya kwanza na si Mwaka 1948.
Pacha wanakubaliana kwamba hakuna aliyemjua Mwalimu Nyerere
Halafu wanajichanganya Mwalimu alitambulisha kwa Abdul na Kasela Bantu.

Kasella Bantu aliyekuwa na Mwl katika ujana hakuwahi kumweleza Abdul kuhusu mtu aliyeandika ile barua kutoka Makerere na ambaye ni katibu wa tawi la TANU Tabora.

Lakini pia huyu Abdul Rais wa TAA alikuwa kiongozi wa ajabu, hakumjua katibu wa Tawi la Tabora!

2. Wote wanakubaliana kuundwa kwa TANU kutoka TAA.
Pacha wa leo( P-Leo) anasema kamati ya Siri iliundwa na Mwalimu alikuwepo.
Pacha mzooefu sana(P-MS) anasema TANU iliundwa Bama na Abdul Mwal hakujua lolote!

3. P-Leo sijui kama ni mdogo au la , anasema Mikutano ya TAA ilifanyika barazani kwa Dossa.

P-MS anasema, la hasha ilifanyika barazani kwa Abdul Syke, kijana wa Bi Mluguru.

4. Kuna ufanano wa Kaptula. P-Leo katutajia aliyemfundisha Mwalimu kuvaa suruali
P-MS amelikana kana hili lakini ukifukua maandishi amelitumia kwa Mwalimu, kuonyesha jinsi alivyokuja na ushamba. Mzoefu hasemi wazi kama pacha mgeni

Sisi kule Muheza tukisema ''ukiwa muongo basi uwe na kumbukumbu''

Masalaam.

Pascal Mayalla JokaKuu
Nguruvi3,
Hata wale ambao wananichukia kwa ajili ya hasad hawajapata kusema kuwa Mohamed Said anaandika ''ngano'' mfano labda wa Irving Wallace au James Clavell.

Naweza nikakuwekea hapa vitabu nilivyoandika pamoja na papers kisha nikakupa changamoto uoneshe ''ngano,'' nina hakika hutaweza la kama unabisha sema ''su,'' nikuwekee.

Naamini unataarifa kuwa kitabu cha Wasifu wa Julius Nyerere kimetoka siku chache zilizopita.
Soma hapo chini ujumbe nilioandikiwa na waaandishi wake:

''Ndugu Mohamed,
Salaam kutoka Dar es Salaam. Tunatumai uko mzima. Tuna furaha kukujulisha kuwa kile kitabu cha wasifu wa Mwalimu Nyerere tulokuwa tunakiandika sasa kimeshachapishwa. Ndugu Mohamed, ulitoa mchango muhimu kwenye mchakato wa utafiti, na hivyo tuna furaha kubwa kukutunukia nakala ya kitabu. Ikiwa utapenda kukifuata kitabu kupitia kijana wako hapo TPH mtaa wa Samora, unaweza kufanya hivyo. La sivyo, tunaomba anuani ya kukutumia nakala yako. Tunatoa shukrani zetu tena na kukutakia kila la kheri.
Prof Issa Shivji
Prof Saida Yahya-Othman
Dr Ng’wanza Kamata''

Bwana Nguruvi3,
Bado unaamini naandika ''ngano?"?

Kuhusu historia ya TANU sina sababu ya kubishana na mtu yeyote kwani mimi nimeandika historia ya wazee wangu jinsi walivyounda chama cha TANU wewe kinakukasirisha nini?

Vipi utataka kuniingiza katika ubishi usio na tija wa Nyerere aliishi kwa Abdul au aliishi nyumbani kwa Ally?
Hivi kweli Abdul Sykes kadi yake ya TANU no. 3?

Kweli Denis Phombeah Mnyasa wa Nyasaland kadi yake ya TANU no. 5 na Dome Budohi Mluya kutoka Kenya kadi yake ya TANU ni no. 6?
Sasa ilikuwaje hawa wakawa wanachama wa TANU na wengine kuwa viongozi?

Kweli Chief Kidaha Abdul ndiye alimtaka awe Rais wa TAA kisha waunde TANU.

Hivi kweli African Association iliasisiwa na baba yake Abdul Sykes?
Hivi ni kweli Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa anauza kadi za TANU misikitini wakati anadarsisha?

Waliotaka kujua historia ya wazee wangu wamesoma kitabu na wakaja nyumbani kwangu kwa heshima na ustaarabu wote kuja kunihoji kuhusu uhusiano wa Julius Nyerere na wazee wangu.

Kama wewe una historia nyingine andika tusome.

Hawa waliaondika wasifu wa Nyerere waliona athari ya kuiacha historia yangu ibaki peke yake haina jibu nami nimemtaja sana Mwalimu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Angalia picha ya mimi kwa heshima ya hawa walimu wangu walionisomesha mimi nimekaa chini ya miguu yao.
Waliponiuliza kwa nini nakaa chini nikawaambia hii ndiyo adabu ya ilm.

Ndugu yangu unakuja hapa na kejeli na lugha za maudhi...
Mimi si mtu wa hayo tafuta mfano wako mshambuliane kifu yenu.
 

Attachments

  • PROF. SHIVJI, PROF. SAIDA NA DR. KAMATHA.JPG
    PROF. SHIVJI, PROF. SAIDA NA DR. KAMATHA.JPG
    12.6 KB · Views: 8
  • PROF. ISSA SHVJI NA PROF. SAIDA YAHYA-OTHMAN.jpeg
    PROF. ISSA SHVJI NA PROF. SAIDA YAHYA-OTHMAN.jpeg
    34.5 KB · Views: 8
  • WASIFU WA JULIUS NYERERE.jpg
    WASIFU WA JULIUS NYERERE.jpg
    6.4 KB · Views: 8
Mohamed Said
Heee! sheikh imekuwaje tena na swaumu hii, mbona umetufikia kwa taharuki, hamaki na jazba?
Katika uzi huu sijataja neno 'ngano'' iweje unilishe maneno yako!

Hata hivyo huhitaji vitabu na paper, kuamini Nyerere alikuja Dar mwaka 1952 kwa mara ya kwanza si ngano?

Kuamini mwenyekiti wa TAA Bw Abdul hakumjua katibu wa tawi la Tabora Mh Nyerere si ngano hiyo?

MS, mbona tupo jamvini muongo mmoja tukionyesha mchele, chuya na Mashudu seuse ngano!

MS au ulitaka mahala pa kueleza umeletewa nakala ya kitabu cha Mwl Nyerere, eleza tu usinitumbukize huko

Badala ya kunishambulia mjibu mleta mada, kwamba, mikutano ilifanyika barazani kwa Dossa na si kwa mwana wa Bi Mluguru, Bw Abdulwahidi Kleist Sykes Mbuwane(mamluki).

Maslaam

Mag3
 
Mohamed Said
Heee! sheikh imekuwaje tena na swaumu hii, mbona umetufikia kwa taharuki, hamaki na jazba?
Katika uzi huu sijataja neno 'ngano'' iweje unilishe maneno yako!

Hata hivyo huhitaji vitabu na paper, kuamini Nyerere alikuja Dar mwaka 1952 kwa mara ya kwanza si ngano?

Kuamini mwenyekiti wa TAA Bw Abdul hakumjua katibu wa tawi la Tabora Mh Nyerere si ngano hiyo?

MS, mbona tupo jamvini muongo mmoja tukionyesha mchele, chuya na Mashudu seuse ngano!

MS au ulitaka mahala pa kueleza umeletewa nakala ya kitabu cha Mwl Nyerere, eleza tu usinitumbukize huko

Badala ya kunishambulia mjibu mleta mada, kwamba, mikutano ilifanyika barazani kwa Dossa na si kwa mwana wa Bi Mluguru, Bw Abdulwahidi Kleist Sykes Mbuwane(mamluki).

Maslaam

Mag3
Nguruvi3,
Unapenda shari na naona unajisikia raha kutafuta kushambuliana.

Kwanza mimi si sheikh kama wewe ulivyokuwa si mchungaji.

Mimi ni sawasawa na mtu yeyote yule.

Wala hakuna taharuki wala hamaki.

Mimi natafakhari kuwa wazee wangu wana historia na katika historia hii yao ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika ndipo wanapokutana na Nyerere.

Vinginevyo labda ungesoma kitabu changu na ungekisahau kama kitabu kingine chochote kwani sijakusoma ukiishambulia historia ya Chuo Cha CCM Kivukoni.

Haikukukera kwa kuwa ndani yake hukumkuta Abdul Sykes na historia yake ya kuwa ndiye aliyempokea Mwalimu Dar es Salaam.

Haikukera kwa kuwa hukumsoma Sheikh Suleiman Takadir wala Iddi Faiz Mafungo wala Bi. Tatu bint Mzee.

Wewe na wengine wengi mfano wako wazalendo hawa hamkuwajua na kamwe msingewajua majina yao wala nafasi zao katika maisha ya Nyerere kama nisingenyanyua kalamu kuandika.

Umeghadhibika kwa nini Waswahili hawa wameunganishwa na Nyerere?

Labda umefunzwa kudharau watu na ulipotambua kuwa umedanganywa ndipo ulipojenga chuki.

Lakini nimewaeleza hawa wazee wangu kama inavyostahili kuelezwa na heshima yao leo imerejea.

Ulitaka historia hii ipotee ibaki historia ya Nyerere peke yake?

Ndiyo maana katika kuandika historia ya Julius Nyerere nikawekwa katika orodha ya watu wanaomjua Nyerere lau kama mimi na yeye hatukupata kukutana hata siku moja.

Mimi nijifarague kwa kitabu cha Nyerere?

Nimemtafiti Nyerere na kuandika historia yake na kitabu chake kuchapwa Uingereza zaidi ya miaka 20 iliyopita na sababu ya kitabu kuchapwa nje ni kuwa publishers wote nchini pamoja na Oxford University Press Nairobi walikiogopa kitabu changu.

Kipi kiliwatia hofu?

Hiki kinachokughadhibisha wewe ndicho kilichowatisha.

Lakini baada ya kitabu kutoka Oxford Nairobi (2007)na Oxford New York (2011)na wachapaji wengine wamechapa kazi zangu na cha kustaajabisha zote Nyerere nimetaja kwa sifa zake anazostahili.

Kama kujifaragua ningejifaragua na hawa si kwa kupewa kitabu kitabu cha Nyerere.

Ningejifaragua kwa kumzungumza Abdul Sykes Northwestern University, Evanston, Illinois, Ukumbi wa Eduardo Mondlane.

Nahitimisha kwa kukufahamisha kuwa nimeombwa nifanye "book review," ya kitabu cha Mwalimu.







Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kafanya yote Mazuri kwa ajiliya Nchi lkn Leo kasahaulika kabsaa anakumbukwa Piere au Kingwendu..
Mungu amrehem Mzee Dossa Aziz..
Mungu awalipe ubaya wale wote walozulumu haki yake huyu Mzee

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati mwingine watu kawa hawa wanasahaulika kwa sababu ya kutokuwepo na kumbukumbu zozote zinazo wahusu. wengi tunaujua mtaa wa Dosa pale Magomeni lakini hatukua tunajua mwenye jina alikuwa ni nani. Tujifunze kuweka kumbukumbu za mambo/watu mbalimbali kwa ajili ya vizazi vijavyo
 
Wakati mwingine watu kawa hawa wanasahaulika kwa sababu ya kutokuwepo na kumbukumbu zozote zinazo wahusu. wengi tunaujua mtaa wa Dosa pale Magomeni lakini hatukua tunajua mwenye jina alikuwa ni nani. Tujifunze kuweka kumbukumbu za mambo/watu mbalimbali kwa ajili ya vizazi vijavyo
Kitumaki,
Huu ni Mtaa wa Dosi siyo Dossa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Mohamed Said, post: 35310156, member: 12431"]
Nguruvi3,Unapenda shari na naona unajisikia raha kutafuta kushambuliana.
Mzee Said, Hakikha katika kaumu ya waungwana sikosi kiti. Chembelecho punguza jazba mwezi 15 tunashuka
Kwanza mimi si sheikh kama wewe ulivyokuwa si mchungaji.
Kuna mtu alinigutia sheikh si msalishaji, ni neno la kiarabu la 'mzee''. Kama unaukana uzee hair inshallah, wakati ukifika ni majaaliwa tu
Mimi ni sawasawa na mtu yeyote yule.
Wewe ni sawa na mimi na sijui uchungaji unanipa kutoka wapi Yarabi.
Vinginevyo labda ungesoma kitabu changu na ungekisahau kama kitabu kingine chochote kwani sijakusoma ukiishambulia historia ya Chuo Cha CCM Kivukoni.
Kuna sababu sishambulii kitabu cha Kivukoni.
Nilishakisoma mara moja na sitakirudia tena, sasa upige Bomu mochuari halafu utambe umeua
Haikukera kwa kuwa hukumsoma Sheikh Suleiman Takadir wala Iddi Faiz Mafungo wala Bi. Tatu bint Mzee.
Bi Mluguru pia. Inikere nini wewe kutaja wazee wako!
Umeghadhibika kwa nini Waswahili hawa wameunganishwa na Nyerere?
Lahaula! mimi mwenyewe Mswahili, leo uswahili unikere! Hakika akutukane hakuchagulii tusi.
Nanynyua nyuso kukuombea kwa maulana akujaze palipopungua, na palipojaa ajazie pomoni! akusamehe unapoghafilika, kaupe subra penye hamaki na upendo kwa Nyerere
Labda umefunzwa kudharau watu na ulipotambua kuwa umedanganywa ndipo ulipojenga chuki.
Hii wanaita inferiority complex, yaani mtu anahisi kuchukiwa bila kuwepo chuki.
Lakini nimewaeleza hawa wazee wangu kama inavyostahili kuelezwa na heshima yao leo imerejea.
Waliowavunjia heshima ni Wazee wako wa Dar es salaam,

Yusuph Makamba ana alama Dar lakini ya Idd Faiz Mafungo hatuioni, ya Bi mluguru hatuioni, Bi Selengia, au Mnonji, na hata basi mamluki Mbuwane aliyetuletea ''uzao maalumu'' kama unavyoamini hatuoni.

Hawa wazee wako walikuwa madiwani na mameya miaka mingi tu baada ya uhuru ndio walianza kukosa adabu sisi wengine tunafuata tu.Sikumoja natamani nikusikie ukiwasota madole ya macho, ukimaliza ndipo urejee kwetu!
Mimi nijifarague kwa kitabu cha Nyerere?
Huyu bwana humpendi weweee!

Yaani ukimsikia Nyerere roho inapaa.Hata hivyo ukweli unabaki pale pale ndiye aliyepokea uhuru si Abdul Sykes! Ni ukweli si mimi wala adabu zangu.
Hiki kinachokughadhibisha wewe ndicho kilichowatisha.
Yaani nilisoma vitabu vyote, kiingereza na kiswahili , matoleo yote magazetini, sijawahi kughadhabika.

Kinachotia ghadhabu si kitabu ni maudhui, unaponyunyuzia hamira, ukaumua tukabaki na shudu na ngano.
Hili linatia ghadhabu sana. Halafu hutaki kubadilika hata ukiambiwa 1 na 1 ni 2.

Nyerere hakufika Dar mwaka 1952 wala hakuingizwa siasa na Abdul na kwamba Abdul alimjua akiwa Tabora na walikutana mkutano mkuu Dar es salaa.Sasa tunasikia katika uzi huu kuwa vikao viilikuwa kwa Dossa si kwa mwana wa Bi Mluguru , karani wa soko Abdul.
Lakini baada ya kitabu kutoka Oxford Nairobi (2007)na Oxford New York (2011)na wachapaji wengine wamechapa kazi zangu na cha kustaajabisha zote Nyerere nimetaja kwa sifa zake anazostahili.
Tafadhali bwana, wewe umuheshimu Nyerere mvaa Kaptula!

MS umeheshimu Nyerere! real? Unavyomchukia mzee wa watu!
Yaani wewe unayekaa kimya watu wakisema Nyerere laanatullah leo unampenda !
Mzee Said, una swaumu kumbuka. Lahaula kapate Iftar kama si daku kisha funda la maji!
 
Mzee Said, Hakikha katika kaumu ya waungwana sikosi kiti. Chembelecho punguza jazba mwezi 15 tunashukaKuna mtu alinigutia sheikh si msalishaji, ni neno la kiarabu la 'mzee''. Kama unaukana uzee hair inshallah, wakati ukifika ni majaaliwa tu Wewe ni sawa na mimi na sijui uchungaji unanipa kutoka wapi Yarabi. Kuna sababu sishambulii kitabu cha Kivukoni.
Nilishakisoma mara moja na sitakirudia tena, sasa upige Bomu mochuari halafu utambe umeua Bi Mluguru pia. Inikere nini wewe kutaja wazee wako!
Lahaula! mimi mwenyewe Mswahili, leo uswahili unikere! Hakika akutukane hakuchagulii tusi.
Nanynyua nyuso kukuombea kwa maulana akujaze palipopungua, na palipojaa ajazie pomoni! akusamehe unapoghafilika, kaupe subra penye hamaki na upendo kwa Nyerere Hii wanaita inferiority complex, yaani mtu anahisi kuchukiwa bila kuwepo chuki. Waliowavunjia heshima ni Wazee wako wa Dar es salaam,

Yusuph Makamba ana alama Dar lakini ya Idd Faiz Mafungo hatuioni, ya Bi mluguru hatuioni, Bi Selengia, au Mnonji, na hata basi mamluki Mbuwane aliyetuletea ''uzao maalumu'' kama unavyoamini hatuoni.

Hawa wazee wako walikuwa madiwani na mameya miaka mingi tu baada ya uhuru ndio walianza kukosa adabu sisi wengine tunafuata tu.Sikumoja natamani nikusikie ukiwasota madole ya macho, ukimaliza ndipo urejee kwetu! Huyu bwana humpendi weweee!

Yaani ukimsikia Nyerere roho inapaa.Hata hivyo ukweli unabaki pale pale ndiye aliyepokea uhuru si Abdul Sykes! Ni ukweli si mimi wala adabu zangu. Yaani nilisoma vitabu vyote, kiingereza na kiswahili , matoleo yote magazetini, sijawahi kughadhabika.

Kinachotia ghadhabu si kitabu ni maudhui, unaponyunyuzia hamira, ukaumua tukabaki na shudu na ngano.
Hili linatia ghadhabu sana. Halafu hutaki kubadilika hata ukiambiwa 1 na 1 ni 2.

Nyerere hakufika Dar mwaka 1952 wala hakuingizwa siasa na Abdul na kwamba Abdul alimjua akiwa Tabora na walikutana mkutano mkuu Dar es salaa.Sasa tunasikia katika uzi huu kuwa vikao viilikuwa kwa Dossa si kwa mwana wa Bi Mluguru , karani wa soko Abdul. Tafadhali bwana, wewe umuheshimu Nyerere mvaa Kaptula!

MS umeheshimu Nyerere! real? Unavyomchukia mzee wa watu!
Yaani wewe unayekaa kimya watu wakisema Nyerere laanatullah leo unampenda !
Mzee Said, una swaumu kumbuka. Lahaula kapate Iftar kama si daku kisha funda la maji!
Nguruvi3,
Launcelot Gobbo...
Soliloquy!

Umenichekesha kidogo.
Ahsante sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom