Mhhh somo zuri sana na picha zako Lizzy zimeendana na uhalisia wake.
Swali kubwa hapo kweli je wale ambao wako kwenye ndoa zao au ndo wanaingia au wanatafuta namna ya kuingia kwenye hizo ndoa are they ready to be there till kifo kiwatenganishe. Wako radhi kupambana na milima na mabonde mpaka wafikie umri wa huyo babu na bibi hapo.
Swali kwa wengi ni gumu maana kuna watu wako kwenye ndoa hawana uhakika wa kesho yake kitatokea nini. Wapo kwa sababu kuna mmoja anaogopa kuachika au anaogopa financial difficulties atakazokutana nazo akiachana na mwenzake, atakosa mali walizochuma pamoja, atakosa gari analotumia kuringia mjini, atasemwa vibaya na jamii na mambo kama hayo. Ila ile ndoa halisi na maana yake haipo ndani ya moyo wa mtu kama huyo.
Tatizo ni nini
Je wakati unaingia kwenye ndoa uliingia kwa kuwa ulimpenda mwenzako au ulivutiwa na status yake kwenye jamii au mshahara wake au mali zake
Je ulikuwa na uhakika kuwa huyu ndie atakayekuwa mwezangu mpaka kifo kiwatenganishe
Je ulimpenda kweli au ulimtamani tuu the way alivyo ukaona anafaa kuwa mke/mume
Je wakati unachukua kiapo cha kuwa mke na mume ulikuwa unamaanisha au ulikuwa unatamani padri, shekhe, mchungaji au DC amalize haraka uendelee na mambo yako au ufunue makucha uliyoyaficha
Je ulikuwa na uhakika kabisa kuwa huyu ndie nitakayekuwa nae kwa maisha yangu yote kwenye shida na raha, ugonjwa na taabu, akifilisika, akikosa kazi, mali ikipotea,akipata kilema cha maisha, au ulikuwa unatamani mguu wake wa bia au macho yakle mazuri, au umbo lake la no nane. Je akiwa kilema ile miguu mizuri ikiondoka will u still love her, au akiwa kipofu yale macho yake uliyoyatamani yakikosekana will be her partner till death separate you?
Sasa ukiweza jibu hayo maswali na changamoto nyingine mbalimbali ingia kwenye ndoa ukiwa na uhakika kuwa yule uliye nae mtafikia umri wa huyo babu hapo juu.
Ila hizi ndoa za kufuata mkumbo kuwa Lizzy kaolewa na mimi ngoja nimlazimishe yule jamaa yangu tuoane mwisho wake ni majuto. Unakuja kukumbuka kuwa ulikuwa humpendi na wala hauko tayari kuwa nae hata kwa usiku mmoja zaidi.
Au kwa kuwa fulani ameoa ngoja na mimi nioe au wacha nimuoe fulani nifaidike na mali zake au wacha fulani anioe nikafaidi utajiri wake hapo jua kuwa hakuna ndoa.
Mambo haya na mengine yanapunguza thamani ya ile taasisi ya ndoa na kufanya kuongezeka sana kwa talaka zisizotarajiwa hasa kwa watu kuoana na baadae wanakuja kujikuta kwambva hawakuwa wanawapenda au hakuna ile dhamiri ya ndoa ndani mwao. Walisukumwa zaidi na tamaa au mambo ya dunia zaidi ya institution ya marriage yenyewe.
Kwangu mimi am sure and absolutely sure and God yupo kushuhudia haya I will be in that shoes of that grandpa and grandma above with my marriage. Nilimpenda na nampenda na nitampenda till death do us part.