Mpaka wa Namanga wafungwa kwa muda baada ya Kenya kuwazuia madereva malori kutoka Tanzania kwa kutokuamini vipimo vyao vya #Corona

Mpaka wa Namanga wafungwa kwa muda baada ya Kenya kuwazuia madereva malori kutoka Tanzania kwa kutokuamini vipimo vyao vya #Corona

Wewe una virusi vya corona au hauna , kama hauna unapenda nani awe nayo na kama unayo ,wewe kuwa nayo inatosha
Tanzanian President John Magufuli has said the number of coronavirus patients in hospitals is declining, although the government has not released data on infection rates for many weeks.

The president has repeatedly downplayed the risk of the pandemic, causing alarm among neighbouring African countries and international organisations.

The government has even urged Tanzanians to dedicate three days for thanksgiving this weekend as they say they're beating the virus.

So what do we know about the situation in Tanzania?

Where is the data?

The main issue is that there's been no official data on the coronavirus for weeks, and there are concerns that the authorities are trying to downplay the extent of the outbreak.

Doctors and healthcare professionals are afraid to speak out about coronavirus because of a climate of fear.

"Tanzania has always had very repressive laws against freedom of expression and the press," says Roland Ebole, a regional researcher at Amnesty International.

"We are now seeing these laws being used in a more intensive way to target those who are speaking out, especially about Covid-19," says Mr Ebole.

The government stopped releasing daily updates on the number of positive cases in April, with the president saying they were creating panic.

The Africa Centres for Disease Control and Prevention has "strongly" called on Tanzania to release its latest data on the outbreak.

The last figures, published on 29 April, reported 480 cases and 21 deaths (its island territory Zanzibar has since added 29 more cases in May).
 
Kenya haawaamini Tanzania kwa Sababu tz unasema Corona umeisha kwa maombi, hii haingii akilini kwa mtu yoyote
Sasa hata kama corona ipo utafanyaje sasa kwani kenya wana dawa unapima alafu ili iweje wakati dawa hakuna
 
Mnasema kwenu wagonjwa wamebaki wanne, balozi wa Marekani anatoa taarifa yake anaonesha hali bado mbaya, nani atawaamini nyie?

Hamuwezi kuchakachua hivyo vipimo kuwalinda madereva wenu?

A second thought also is a thought, huwezi kumdharau mtu simply bcoz kabadilisha msimamo wake, kama una akili timamu jiulize why?

There is nothing clear over there, unless you are myopic.
Basi waende marekani
 
Hapa kwenye hii video sioni wale wazee wa kushabikia kenya wakitoa neno
Sijui wamelala?
Yani natamani mods waiweke ile video kule mwanzo ili wale wapumbavu watanzania wenzetu wanaotusaliti waione yani natamani niwatie shaba manake ni useless kabisa. Safari hii magu funga mpaka tu then weka bandari kavu hakuna kucheka na kima
 
Tatizo kubwa ni uelewa na mambo ya "Copy and Paste" kisa mzungu anafanya:
Mtu akipimwa na kuwa +ve, haimaanishi kuwa tayari ni mgonjwa wa covid. Asilimia 85 hadi 95% ya waliopimwa na kuwa +ve, hawaonyeshi dalili zozote za ugonjwa wa covid (asymptomatic) au mild symptoms na hupona baada ya siku 3-14. Ni kama silimia 5% tu ndiyo huwa severe cases ambazo kwa Tanzania ndiyo wanakuwa admitted for further management, hasa wenye magonjwa mengine kama kisukari au pressure n.k lakini wale wengine huwa wanaruhusiwa na kurudi nyumnbani. Na ndiyo hiyo idadi Mhe. Ummy nadhani anayoiongelea. Sasa unapofanya mass screening ili ujue kama wangapi wamekuwa infected, HAISAIDII CHOCHOTE, hasa kama ugonjwa tayari uko kwa jamii (community transmission). Ndiyo maana Tz tunafanya "targeted screening", na hata hao madereva, ni kwa sababu ya hayo makubaliano, otherwise, its wastage of tax payers money, na kuleta Public panic unnecessarily. Kama mass screening ingesaidia, tungeona deaths huko US zikipungua, lakini hakuna.
Cha msingi nchi zingeongeza juhudi kwenye elimu ya kujikinga badala ya kila siku kutoa takwimu za waliokufa na walioambukizwa, ambazo hazisaidii chochote. On the other side, hizo lockdown zimeathiri uchumi sana, ngoja majirani zetu waendelee hiyvo hivyo mpaka Oktoba au December, na baadaye tuone nani ameathirika zaidi kiuchumi.
Sasa tz ilishindwaje kuelezea Kenya wao haawaamini Kama vipimo vinasaidia ili iwr hakuna kupima kabisa? Huu ndio uduwaanzi
 
Tumieni akili acheni hasira, matendo yenu yanaleta aibu kwa taifa, mjifunze kusikiliza wengine.

Hapa ndio mtajua ule uongo wenu wa wagonjwa kupungua huwa mnajidanganya wenyewe.
Nyie Wakenya mtakalia kushikilia mambo ya Corona hadi lini? Tatizo ni misaada mnatoipata kutoka ulaya na Marekani. Corona sio ugonjwa wa kutishia Afrika hasa chini ya jangwa la sahara. Nyie Wakenya mnajibaruguza tu.
 
Hao jamaa ni wajinga sana!

Wanakimbizana kutoa takwimu sijui ili wamfikie USA?

Wanaumia sana kuona tz maisha yanaemdelea huku wao wamejifungia ndani kama mwali
Wapuuzi kweli hao wakenya hasa viongozi wao ambao ni wafisadi wa kutupwa. Kibaya zaidi wanawatesa wananchi wao ambao ni masikini wa kutupwa mfano wale raia wa Kibera ambao hata Corona kwao sio ishu.
 
Tanzanian President John Magufuli has said the number of coronavirus patients in hospitals is declining, although the government has not released data on infection rates for many weeks.

The president has repeatedly downplayed the risk of the pandemic, causing alarm among neighbouring African countries and international organisations.

The government has even urged Tanzanians to dedicate three days for thanksgiving this weekend as they say they're beating the virus.

So what do we know about the situation in Tanzania?

Where is the data?

The main issue is that there's been no official data on the coronavirus for weeks, and there are concerns that the authorities are trying to downplay the extent of the outbreak.

Doctors and healthcare professionals are afraid to speak out about coronavirus because of a climate of fear.

"Tanzania has always had very repressive laws against freedom of expression and the press," says Roland Ebole, a regional researcher at Amnesty International.

"We are now seeing these laws being used in a more intensive way to target those who are speaking out, especially about Covid-19," says Mr Ebole.

The government stopped releasing daily updates on the number of positive cases in April, with the president saying they were creating panic.

The Africa Centres for Disease Control and Prevention has "strongly" called on Tanzania to release its latest data on the outbreak.

The last figures, published on 29 April, reported 480 cases and 21 deaths (its island territory Zanzibar has since added 29 more cases in May).
Habari hii inahusiana vipi na thread hii
 
MPAKA wa Namanga upande wa Tanzania umesitisha shughuli zote za kibiashara na nchi jirani ya Kenya kwa muda kutokana na nchi hiyo kutoamini vyeti vya ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na virusi vya corona vya madereva wa malori wa Tanzania vinavyoonyesha kuwa hawajaambukizwa.

boda.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe, ameiambia Nipashe jana kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa Kenya kukiuka makubaliano ya pande hizo mbili, waliyotiliana saini Mei, mwaka huu kwa kuzuia madereva wa Tanzania, kukataa vyeti ili wawaruhusu kuingia Kenya.

“Nadhani wenzetu wana ajenda ya siri kutuhujumu kiuchumi, tumeshakubaliana dereva anapopimwa upande wa Tanzania aruhusiwe upande wa Kenya kwa cheti, sasa wamekiuka makubaliano, wakifika upande ule wanataka wawapime tena sijui wana maana ipi nashindwa kuwaelewa kabisa, tumeamua kuchukua hatua na haturudi nyuma,” alisema.

Katika makubaliano hayo waliamua katika lori itaruhusiwa dereva na wasaidizi wawili kuingia katika nchi husika wote wakiwa wamepimwa kama wana maambukizo ya corona.
Hata hivyo, alisema upande wa Kenya wamebadilika juzi (Jumatatu) kwa kuzuia na kutaka kuwapima tena.

“Pamoja na juhudi za mimi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, kuwasiliana na viongozi wenzetu wa Kenya, lakini zimegonga mwamba na ndipo tukaamua kuzuia vyeti vyote na magari ya mizigo kutoka Kenya pamoja bidhaa zote zinazoingia kutoka nchini humo hadi hapo tutakapokaa tena na kufikia muafaka maana sote tunategemeana, Kenya wanatuhitaji kama soko na sisi wanatuhitaji pia ili kuuza bidhaa,” alisema Mwaisumbe.

Alisema mwezi Mei makubaliano ya kuruhusu kuaminiana pande mbili yalikaliwa kikao na mawaziri wa mambo ya nje za nchi, makatibu wakuu, wataalamu na viongozi wengine wa mikoa na wilaya wa kutoka nchi mbili katika mpaka wa Namanga, kufuatia mazungumzo ya Rais John Magufuli na Rais Uhuru Kenyata ambao waliwaagiza viongozi wanaohusika kukaa na kufanya vikao na makubaliano, huku wakichukua tahadhari za ugonjwa huo na kuona namna ya kuendelea na biashara kwa nchi hizo.

Alisema kama hali ya kutoaminiana itaendelea, itawalazimu kutoa uamuzi wa kuigeuza Namanga kuwa bandari kavu na majirani Wakenya watashusha mizigo au bidhaa upande wake na Tanzania kuichukua na pia hata Tanzania itapeleka wa Tanzania ili Kenya waifuate.

“Nchi yetu ni huru inayojitegemea haihitaji kubembeleza nchi nyingine kufanya biashara kwa sababu sisi tunategemeana, haiwezekani mambo ambayo yameagizwa na marais viongozi wa chini hawatekelezi…linaashiria dharau na ajenda ambayo wanadhani ni siri iliyofichika kumbe sisi tunaifahamu, hatutaweza kuivumilia hata kidogo,” alisema.

Alisema, nia ya Rais Magufuli ni kuwasaidia watu wa hali ya chini kwa kuwa uamuzi huo unapofanyika wanao umia ni watu wa chini.

“Nataka nikuhakikishie ndugu kupima kipimo cha Covid-19 sio lelemama kinaumiza sana, sasa haiwezekani siku mbili mtu amechokonolewa pua, halafu anatoka upande wa Tanzania anaenda upande wa Kenya anafanyiwa kitu kile kile, sasa hali hii kwa kweli sio sahihi, tunataka hiyo agenda yao ya siri ijitokeze hadharani tushughulike nayo kuliko kutumia ugonjwa wa Covid-19, sisi hatutakuwa tayari,” alisema Mwaisumbe.
Miss hongera kwa kutuhabarisha. Ila hayo macho...punguza kulembua utafanya tuuze ng'ombe zetu.
 
Sasa tz ilishindwaje kuelezea Kenya wao haawaamini Kama vipimo vinasaidia ili iwr hakuna kupima kabisa? Huu ndio uduwaanzi
Kenya ni nchi huru wana haki ya kuamini kila mzungu anachofanya, Tz pia tuko huru kufanya tunachotaka sasa na si kwa masharti au maelekezo ya mzungu. By the way, nchi nyingi zitakuja kufahamu kuwa, wameharibu uchumi wao na corona bado wako nayo, mpaka pale watakapokubali kuishi nayo. Corona itaondoka baada ya chanjo kupatikana....endeleeni na lockdown, sisi ni full shangwe....
 
Kama Kenya wanahofu kuhusu corona tz kwanini wanaruhusu madereva wao kuleta bidahaa zao huku tz.

Wakenya waache ujinga wawe na msimamo kama hawatuamini they should stop their people to visit our Tz.
 
Kinachowasumbua hawa jamaa ni wivu,wamejaribu lockdown, curfew,wamefanya mauaji kwa raia wako,wamekopa lMF,WB na bado Corona imekuwa ya kwao. Jana nilipata habari kwamba Hospital ya Kenyatta na Mbagathi imelemewa na wagonjwa.hayo yote yanawauma sana.ukizingatia TZ hatujafanya lolote kuumiza raia watu,na watalii wameanza kuja kwa wingi sana TZ,lazima iwaume.
 
Mkuu New Zealand hawakutangaza hivyo baada ya maombi. Ni kwamba wanapima watu wao kwa kiwango cha juu, barabarani, majumbani nk. Wakipima watu 100 wakakuta labda ni mmoja tu au 0 katika waliowapima hawana Corona basi wana haki ya kutangaza Corona imeisha na dunia ikawaamini.

Sasa je, sisi Tanzania tulitangaza Corona imeisha baada ya kufanya kama walivyofanya New Zealand?

Kwa nini hata unashangaa kuaminika wa New Zealand iliyopima watu wake na kutoaminika kwa Tanzania iliyofanya maombi?

Kama unataka tuamini Tanzania Corona imeisha, waambie watu wa Maabara wapime watu angalau 50 kila siku kwa wiki moja Soko Kuu Kariakoo, Manzenze, Temeke Yombo, Arusha mjini, Dodoma mjini, Mbeya mjini na Mwanza.

Kisha watutangazie matokeo ndio tutajua Corona imeisha au la.

Kama katika kila 50 tutakaowapima tukikuta ni watu 10 wana Corona, basi mie nitaunga mkono Tanzania tutangaze Corona imeisha
Kama ingekuwepo kama ayo madai yenu, tungekuwa tunashuhudia vifo vingi sana na serikali isingeweza kuficha hata wafanye nini.

Hapa Zanzibar, watu ni careless kushinda maelezo kwenye suala zima la kupigana na covid19, na hakujatokea vifo kama vinavotokea nchi nyengine, na Zanzibar ni kisiwa kidogo tu, ndio kabisaaaa huwezi kuficha kitu. Wake up! Sio kila kitu akifanya mzungu ndio mnaona sawa au ni kweli! Wewe unaushahidi gani kama JMT ilikuwa ikiwapima hao "wagonjwa wa corona"? Au new Zealand? Au tunakaa na tunasikia kwenye media tu?

Wewe unataka kila siku serikali ikwambia kuwa tumepata wagonjwa wapya? kwamba haiwezekani watu kupona? haiwezekani ugonjwa ukaisha eneo fulani?

And by the way serikali haijasema hamna corona, inakubali uwepo wa corona, lakini hakuna kesi mpya hadi sasa.

Maradhi ya mripuko hayafichiki, utaumbuka tu!
 
Back
Top Bottom