saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Nimetafakari sana juu ya uamuzi wa wananchi wa Tanga kuandaa kisomo maalum kwa ajili ya viongozi na watendaji serikalini walioguswa kwenye ripoti ya CAG. Mbali na watu wa Tanga kuamua kufanya dua maalum kwa kina Mwigulu, Makame Mbarawa, Januari na wakubwa wengine waliotajwa na CAG. Pia yuko mtanzania mwingine ameamua kwenda mahakamani kuwashtaki watu hao hao waliotajwa na CAG.
Maamuzi haya ya wananchi kwa kumbukumbu zangu ndogo sina hakika kama matukio haya yamewahi kutokea hapa nchini tangu nchi yetu ipate Uhuru.
Swali je ni watanzania wangapi wanapaza sauti juu ya watu hao ila hazisikiki kwa sababu ya umasikini wao, kutokuwa na simu janja ya kufika mitandaoni na kukosa bando la kuweza kuwasilisha hisia zake kwenye umma.