stickvibration
JF-Expert Member
- Feb 7, 2017
- 3,226
- 5,147
Mpambano huu uwe na nia ya kuburudika lakini pia kujifunza na kuongeza ufahamu kuhusu jamii ya kaliba moja lakini mazingira tofauti wanavyoweza kutofautiana makubwa
Ni mpambano wa wanawake wa Dar vs wa mikoani, ni vema uwe tofauti kabisa na ule wa wanaume wa Dar vs wa mikoani ambao umegeuka kuwa dhihaka na kutambiana sometimes na matusi juu.....
Wanawake ni walezi wetu, ndio wanaotuzaa na mengine mengi... Bila wao maisha hayana maana sasa usikandie hapa halafu usiku ukalielie huko chumbani
Labda niseme tu kwamba kila upande una mazuri na mabaya yake. Wanaume wa dar wakiwa wamechoshwa na wanawake wa mjini ambao wanaenda na wakati mpaka wanasahau majukumu yao muhimu na wengi wakiwa jeuri na wajuaji hukimbilia mikoani vijijini kwenye mabinti ambao hawana shobo za kwenda na wakati...
Tatizo linakuja huyo wa kijijini unapofika bei na kumleta mjini... Ulimbukeni na ushamba huku akitaka kuiga ili aende na wakati hugeuka janga namba moja.....!!!
Mwisho maamuzi huwa magumu uchukue yupi? Mjuaji wa mjini au wife material wa kijijini!? Je akibadilika!?
Kuna mengi kati ya hawa ndugu wa jinsia moja wanaotenganishwa na mazingira... Twende kazi.
View attachment 701861
View attachment 701862
KUTOKANA NA HUU UZI KUWAVUTIA BARAZA LA WAZEE
KUANZIA LEO WAMEKUTEUA WEWE KUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA FITNA[emoji1321]