Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😂😂 anajikaza nje tu bana. Ndani anawaka motooWamenitisha sana
Sema bwana harusi kauzu na mziki ameuchakata vilivyo kama vile hamna kilichotokea🤣🤣
Nampongeza jamaa aachane na hicho kituko aoe mwingineMy Take:
Huu ndio Ubaya Ubwela wenyewe Sasa.😁😁😁👇👇
---
View attachment 3061901
Katika hali isiyo ya kawaida katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Edward Futakamba Mkazi wa Kata ya Nsemulwa amewashangaza wengi baada ya kufanya sherehe ya harusi licha ya Bibi harusi kugoma kufunga ndoa hiyo.
Edward aliyekuwa akiishi na Mwanamke aitwaye Marry na kufanikiwa kupata Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu ambapo baadae waliamua kwa pamoja kufunga ndoa na taratibu zikaendelea ikiwemo kutoa mahari ya shilingi 1,200,000/- na maandalizi ya harusi kufanyika ili ndoa ifungwe July 26 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya harusi hiyo Simon Moshi amesema siku nne kabla ya tarehe hiyo walipata taarifa kuwa upande wa Bibi harusi wameweka pingamizi kanisani la kuzuia ndoa hiyo “Tulijaribu kuwatafuta kuongea nao ili angalau hili suala liende kama lilivyokuwa lakini ikashindikana, tukaona haiwezekani Watu wametoa mchango yao alafu hili suala likatishwe”
“Sababu ambayo sisi tuliambiwa kama kamati walisema kwamba kwanza bwanaharusi alikuja amechangamka kwenye send off na wakasema kwamba kuna laki mbili haijamalizwa ya mahari”amesema Katibu wa Kamati ya harusi.
“Kupata na kukosa yote ni sehemu ya maisha, cha msingi sana ikiwa kama Mtu unaweza kusherehekea na kufurahia ukipata basi ni vizuri pia hata ukikosa pia usherehekee na kufurahia kwa sababu mpango wa Mungu yeye ndio anayejua” amesema Edward Futakamba.
Mwisho
Unataka utaolewa ,hutaki utaolewa Kwa lazima 😂😂😂
•Nampongeza bibi Harusi kumkataa huyo jamaa anaelazimisha ndoa.😂😂
🤣🤣🤣 Daah maskini😂😂 anajikaza nje tu bana. Ndani anawaka motoo
Hapo kuna maswala makubwa sana ya kisheria ambayo nchi zingine mfungisha ndoa na huyo aliyezuia wangeweza buruzwa mahakamani walipe fidia na gharama za usumbufu na udhalilishaji kwa bwana Harusi kama vigezo vilivyotumika kutofunga hiyo ndoa haviko kisheriaYani unataka hii iwe habari kubwa...Mzee hata ww haupo siriaz kichwani