Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Hii ni true story ya mpangaji wa bibi yangu pale ilala kota,naandika uzi huu kama hamasa kwa wapambanaji wote kwamba ukiweka malengo na kuishi nayo hakika utafika pale unapotaka kufika
Mpangaji huyu na mume wake walikuwa ni miongoni mwa wapangaji kadhaa pale kwa bibi yangu,pamoja na kwamba nyumba ya bibi ilikuwa na umeme,lakini baadhi ya vyumba vilivyo ongezwa havikuwa na umeme
Hivyo ilikuwa ni jukumu la mpangaji mpya kujionganishia yeye umeme kutoka katika vyumba vingine,lakini miongoni wa wapangaji wengi ambao wote wana umeme,ni mama huyu na mume wake pekee hawakutaka kuonganisha umeme,lakini nyuma ya pazia waliwakuwa na malengo yao
Ni kawaida sana kuamka saa kumi usiku kumkuta bibi huyu akichoma maandazi,na hiyo ilikuwa ni daily au kila siku,lakini nyuma ya mapambano haya wanafamilia hawa walikuwa na malengo mazito sana ya kuwa na mji wao
Hatimaye baada ya miaka nane ya upangaji walihamia katika nyumba yao wenyewe,hapa ndio ikajulikana ile siri ya kujinyima kujionganishia umeme,kwao wao hela hiyo ilikuwa na thamani kubwa sana,kikubwa ilikuwa kufikia malengo yao
Sikwambii wewe ukae chumba cha giza laa,nakwambia kwa kila malengo unayotaka kufikia basi lazima ujitoe sadaka kwa baadhi ya mambo fulani katika maisha ili ufikie pale unapopataka,huna budi kujinyima baadhi ya mambo ili ufikie katika lengo husika
Kuna mtu mmoja alikuwa anapenda kula ovyo ovyo,nadhani tunawajua watu ambao akikuta sambusa lete,keki lete,karanga lete na kadhalika,basi kuna bwana mmoja baada ya kutambua udhaifu wake wa kula kula akaona hivi hawezi akabadilisha hii tabia na kuzalisha kitu kikubwa zaidi
Badala ya kula kula ovyo alihifadhi hela zake na kujenga msikiti mkubwa unaitwa NIMESHAKULA,kwa maana kila alipopata hamu ya kununua hiki ama kile alijiambia nimeshakula
Mwisho wa siku alifikia malengo,hata sisi tunaweza kufikia malengo yetu kwa kujikagua na baadhi ya mambo ambayo hayana umuhimu na mwisho wake tukayaepuka na kutumia hizo fedha kufikia malengo fulani maishani
Anza sasa na sio baadae
Ni hayo tu!