BonventureSr
JF-Expert Member
- Nov 16, 2023
- 879
- 1,432
Baba wacha pombe,Niwafurahishe watu wapi wewee tena ile tar1 ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa asee.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Baba wacha pombe,Niwafurahishe watu wapi wewee tena ile tar1 ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa asee.
Hii kauli inafanya watu wengi wasipambane eti unakufa unaviacha.Daah mimi kuishi Giza ili nihamie kwangu hapana...kuna kufa halafu uliwoacha wanauza tu...let me enjoy the moment..
Ngoja nipunguze niwe napiga tu kamzinga kadogo na safari mbili tu baasii.Baba wacha pombe,
Hii ni slowlane way ambayo hadi ufike unapopataka utachukua muda sana... Suluhisho hapo ni kutafuta njia ya kumuongezea kipato tu.Ni sahihi kabisa unavyosema,mtu kama hana budi kuongeza njia nyingine ya kuongeza kipato ili walau mambo yaende sawa
Lakini doktori Janabi anasema hivi hakuna anayeamka asubuhi na njaa,hivyo tunakunywa chai kwa mazoea tu,acha breakfast kwa kipindi flani uweke akiba,kama unatumia breakfast 2000 asubuhi,ukiacha chai ambayo sio ya lazima mwisho wa mwezi una 60,000 je miezi mitatu hujapata kamtaji ka kufanya chochot?
Naamini kabisa kwa kila kitu kuna njia
Kuishi bila umeme ni gharama zaidi kuliko mwenye umeme.View attachment 3200775
Hii ni true story ya mpangaji wa bibi yangu pale ilala kota,naandika uzi huu kama hamasa kwa wapambanaji wote kwamba ukiweka malengo na kuishi nayo hakika utafika pale unapotaka kufika
Mpangaji huyu na mume wake walikuwa ni miongoni mwa wapangaji kadhaa pale kwa bibi yangu,pamoja na kwamba nyumba ya bibi ilikuwa na umeme,lakini baadhi ya vyumba vilivyo ongezwa havikuwa na umeme
Hivyo ilikuwa ni jukumu la mpangaji mpya kujionganishia yeye umeme kutoka katika vyumba vingine,lakini miongoni wa wapangaji wengi ambao wote wana umeme,ni mama huyu na mume wake pekee hawakutaka kuonganisha umeme,lakini nyuma ya pazia waliwakuwa na malengo yao
Ni kawaida sana kuamka saa kumi usiku kumkuta bibi huyu akichoma maandazi,na hiyo ilikuwa ni daily au kila siku,lakini nyuma ya mapambano haya wanafamilia hawa walikuwa na malengo mazito sana ya kuwa na mji wao
View attachment 3200848
Hatimaye baada ya miaka nane ya upangaji walihamia katika nyumba yao wenyewe,hapa ndio ikajulikana ile siri ya kujinyima kujionganishia umeme,kwao wao hela hiyo ilikuwa na thamani kubwa sana,kikubwa ilikuwa kufikia malengo yao
Sikwambii wewe ukae chumba cha giza laa,nakwambia kwa kila malengo unayotaka kufikia basi lazima ujitoe sadaka kwa baadhi ya mambo fulani katika maisha ili ufikie pale unapopataka,huna budi kujinyima baadhi ya mambo ili ufikie katika lengo husika
Kuna mtu mmoja alikuwa anapenda kula ovyo ovyo,nadhani tunawajua watu ambao akikuta sambusa lete,keki lete,karanga lete na kadhalika,basi kuna bwana mmoja baada ya kutambua udhaifu wake wa kula kula akaona hivi hawezi akabadilisha hii tabia na kuzalisha kitu kikubwa zaidi
Badala ya kula kula ovyo alihifadhi hela zake na kujenga msikiti mkubwa unaitwa NIMESHAKULA,kwa maana kila alipopata hamu ya kununua hiki ama kile alijiambia nimeshakula
Mwisho wa siku alifikia malengo,hata sisi tunaweza kufikia malengo yetu kwa kujikagua na baadhi ya mambo ambayo hayana umuhimu na mwisho wake tukayaepuka na kutumia hizo fedha kufikia malengo fulani maishani
Anza sasa na sio baadae
Ni hayo tu!
Unachosema kuhusu wiring ni sahihi lkn nadhan walikwepa ile donation ambayo huwaumiza baadhi ya watu katika nyumba za kupangaKuishi bila umeme ni gharama zaidi kuliko mwenye umeme.
miaka 8 unanunua mishumaa ama unakuwa na kibatari au tochi? biga gharama na za kuchaji simu mbili
piga gharama ya bulb 2 chumbani na sebereni basi luku ya buku kwa mwezi ama buku mbili inatosha kabisa kwa matumizi yao ukiunganisha na wiring hapo haizidi 100k kwenye chumba chake kama alikuwa na single room ni bulb moja tu buku ni mwezi na ushee.
Huyu mtu hakuwa na malengo kabla ya kupata hela...Kuna kipato mtu anapata hawezi weka malengo yoyote kinaisha chote huyu mnamsaidiaje?
Ni sahihi ishu inakuja utapataje kipato cha ziada,ndio hapo pa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili upate mtajiHii ni slowlane way ambayo hadi ufike unapopataka utachukua muda sana... Suluhisho hapo ni kutafuta njia ya kumuongezea kipato tu.
Yawezekana hata mimi niliwahi wagomea bulb moja tu wanadai 5000 kwa mwezi nikawaambia wanaumwaUnachosema kuhusu wiring ni sahihi lkn nadhan walikwepa ile donation ambayo huwaumiza baadhi ya watu katika nyumba za kupanga
Wewe unawasha taa tu ukirudi geto lakini wenzio wana pasi,sijui brenda,friji na mambo kama hayo
Lau wangekuwa na luku yao walau ingekuwa poa,na wakati ule kulikuwa hakuna vile vimita kama ambavyo tunavyo siku hizi ambapo kila mtu analipa kutokana na matumizi yake
Na huwashi siku nzima 😂😂Yawezekana hata mimi niliwahi wagomea bulb moja tu wanadai 5000 kwa mwezi nikawaambia wanaumwa
Wewe ni mtu wa pili unasema hili expert,je hatuwezi kuwaingiza katika mfumo wetu kwa kipindi fulani ili mambo yaende sawaInategemeana una mke wa dizaini gani
Wanawake wengine hata kama una pesa we mdanganye umezikopwa na mtu ili apunguze matumizi ya roughWewe ni mtu wa pili unasema hili expert,je hatuwezi kuwaingiza katika mfumo wetu kwa kipindi fulani ili mambo yaende sawa
Kuna baba wa familia moja wakati anataka kumaliza nyumba yake,aliwaambia familia yake pamoja na watoto kwamba,sasa hivi tutajibana kidogo hatuta kula vizur kwa wakati fulani ili tumalize nyumba yetu,na ikawa hivyo
Uje kwenye kozi au 😂😂Huyo bibi Hana chumba Cha wageni nije miezi hata mitatu 🥺