Mpangaji amekwenda kushitaki kisa kaibiwa

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!

Kuna mpangaji wangu amechukua hatua ya kwenda kushitaki na kuomba muafaka ili arudishiwe kodi yake baada ya wezi kuingia chumbani kwake na kumuibia baada ya kusahau kufunga mlango.

Sasa ameomba nimrudishie kodi yake kitu ambacho nilikiweka wazi kwenye mkataba kwamba hakuna pesa itakayorudishwa iwapo mpangaji ataamua kuvunja mkataba na kuhama kwa hiyali yake.

Hii imekaaje wadau,je mkataba kama huu unambana mpangaji?
 
Fanya fair, kubaliana naye kwamba utamlipa ila hela unayotegemea ni ya mpangaji atakayeingia kwenye hicho chumba atakachotoka.

Na unamlipa kuanzia mpangaji mpya alipoingia mpaka tar aliyotakiwa kuondoka.
haiwezi kuwa fair sababu ni biashara boss ina taratibu zake,pia kuhama hama kwa wapangaji kiholela kunachafua jina la nyumba.

Pia si rahisi kupata mteja kwa kipindi hiki mpk mwaka mpya wa masomo utapoanza maana wateja ni wanafunzi wa vyuo hii imaweza nifanya nikae mwaka mzima bila kutengeneza faida from that house.

Nahisi ana frastuation coz hajawai ibiwa anavyodai nilimpeleka mpk polisi kuchukua RB na nimeanza kufatilia waliomuibia naamini watapatikana lakini yy analilia kuhama .
 
Nimekuelewa Mkuu, sikuwaza katika angle hiyo.
 
Hebu reverse situation, fanya wewe ni mpangaji unaibiwa kwa style hiyo, utafanyaje? Utaendelea kujenga imani ya mahali hapo...!? Kulilia kuhama ni haki yake, hujui alisota vipi kununua hivyo alivyoibiwa pamoja na kupata hiyo kodi. Tumia busara angalia amebakiza muda gani ili kodi iishe, hata usipomrudishia yote angalau fanya kitu kimpunguzie maumivu! Unaweza kumkata asilimia kadhaa...

Kuhusu kupata wapangaji, wapo tu! Biashara si kupata faida kila wakati, huwa upo wakati wa kupoteza pia!
 
Kama wewe ni capitalist unafata mkataba unasemaje. Kila abiria achunge mzigo wake, au huwa analipia hela ya ulinzi kwako?

Wewe hujatuma wezi wala haulazimiki kisheria kumrudishia fedha. Ningeibiwa mimi nisingekudai kodi, angeibiwa mpangaji wangu nisingemrudishia kodi. Mkataba haupo kama mapambo
 
Ukileta huruma zisizo na faida Kwenye biashara ndio mwanzo wa kufiilisika nankuchekwa na wanaokuzunguka.

As long as mkataba upo na uheshimiwe hivi unadhani hawa wapangaji ikitokea jengo lina tatizo watakuvumilia sana sana watongea shit kuhusu nyumba yako ili usipate wapangaji wengine.

Hivyo cha msingi hapa vipengele vya Kwenye mkataba viheshimiwe.
 
Rudia kusoma nilichoandika, sijazungumzia kuwa na huruma! Soma vizuri!
Na wewe kama unaheshimu biashara especial ya kupangisha ni kwa nini jengo lako uliache liwe na kasoro angali wanakulipa?
In fact kama hutaheshimu wateja kwa kuwatengenezea mazingira mazuri wataongea shit tu, na wateja hutopata!
Cha muhimu ni kuwatengenezea mazingira mazuri ya kuziba mianya ya wao kuongea hizo shit!

Kwa bahati nzuri ni kwamba binafsi mimi nina mwaka wa sita hivi sasa kwenye hii sector!
Sitaki kueleza mengi juu ya ninavyofanya lakini wapo wateja waliowahi kunilipa kodi ya hadi mwaka na wakadumu kwa miezi kama minne au mitano kisha kuondoka kwa sababu mbalimbali na nikamalizana nao kwa busara japokuwa mikataba haikuwa na vipengele vya yale niliyowanyia na wala sijawahi kujutia nilivyofanya zaidi wengine wanatamani kurudi ila ndio hivyo nafasi hamna!
Wengi wanaofanya biashara elimu ya kuwahudumia wateja hawana, hata kama mteja ni mkorofi kiasi gani hata akikutusi, hupaswi kujibishana nae kwa jazba, ukifilisika utasingizia mengine kumbe tatizo ni lako wewe!
 
Kama wewe ni capitalist unafata mkataba unasemaje. Kila abiria achunge mzigo wake, au huwa analipia hela ya ulinzi kwako?

Wewe hujatuma wezi wala haulazimiki kisheria kumrudishia fedha. Ningeibiwa mimi nisingekudai kodi, angeibiwa mpangaji wangu nisingemrudishia kodi. Mkataba haupo kama mapambo
Unachoongea upo sahihi kiongozi katika capitalism economy mambo ndio yapo hivyo.
 
Ukileta huruma zisizo na faida Kwenye biashara ndio mwanzo wa kufiilisika nankuchekwa na wanaokuzunguka.

As long as mkataba upo na uheshimiwe hivi unadhani hawa wapangaji ikitokea jengo lina tatizo watakuvumilia sana sana watongea shit kuhusu nyumba yako ili usipate wapangaji wengine.

Hivyo cha msingi hapa vipengele vya Kwenye mkataba viheshimiwe.
Ukitaka ujue wapangaji hawana huruma jaribu siku moja zima main switch harafu waambie kuna short ya umeme kwny nyumba hvyo tuchange hata jero jero ili tumuite fundi kishoka aweke mambo sawa utaona majibu utakayopokea kama haujatukanwa wakati giza ni la wote nilifanya hvyo siku moja wapangaji nane watatu tu ndio walilipa jero jero wengine wakasema haiwahusu.

Kuna mtu mmoja alishawai nambia kwamba wapangaji wa siku hizi sio sawa na wazamani hawana ujamaa kabisa😂😂😂😂
 
Fanya fair, kubaliana naye kwamba utamlipa ila hela unayotegemea ni ya mpangaji atakayeingia kwenye hicho chumba atakachotoka.

Na unamlipa kuanzia mpangaji mpya alipoingia mpaka tar aliyotakiwa kuondoka.
Upo sahihi kiongozi wewe ni mwelevu lakini huyu kijana ni mshindani huwa mm nafanyaga hvyo mara nyingi lakini yy ni mtu mwenye chuki na wivu na mshindani sana anataka kushindana welevu wa sheria badala ya yeye ku join nguvu ili tumkamate mualifu na akiondoka hatofanikiwa kumpata mwizi wake inabdi hawe mwanamme na wala sio wa kiume maana mwanamme akimbii matatizo.

Hata mm nilishawai panga chumba Ubungo Kibo usiku wangu wa kwanza tu nikaibiwa ila sikumwambia mtu niliona aibu mtoto wa mjini Sinza kuibiwa na watoto wadogo wa Ubungo Kibo.😂😂😂😂
 
Mkataba unasema mpangaji akiibiwa unamlipa au unarudisha kodi?
Haujaeleza ila inabdi tuweke vipengere kama hivyo kwenye mikataba yetu pia tusisahau kipengere cha usuluhishi yaani je ni nani atahusika na kutatua migogoro pindi inapotokea.😂😂😂
 
Wee jamaa Mwenye nyumba kaa kama Miaka Kumi ivi kuanzia leo then utaona kama ulistahili kuomba ushauri kwa Swala dogo kama hili
 
Sijaja kuomba ushauri hapa ,nimeanzisha thread tu kama thread nyingine zinavyoanzishwa ndio maana kwenye thread hakuna neno ushauri.

Thread zinaanzishwa kwa minajiri mbalimbali kama kuburudisha,kuelimisha n.k
Wee jamaa Mwenye nyumba kaa kama Miaka Kumi ivi kuanzia leo then utaona kama ulistahili kuomba ushauri kwa Swala dogo kama hili
 
Habari wadau!

Kuna mpangaji wangu amechukua hatua ya kwenda kushitaki na kuomba muafaka ili arudishiwe kodi yake baada ya wezi kuingia chumbani kwake na kumuibia baada ya kusahau kufunga mlango.

Sasa ameomba nimrudishie kodi yake kitu ambacho nilikiweka wazi kwenye mkataba kwamba hakuna pesa itakayorudishwa iwapo mpangaji ataamua kuvunja mkataba na kuhama kwa hiyali yake.

Hii imekaaje wadau,je mkataba kama huu unambana mpangaji?
Wezi kuingia kwenye chumba chake,wewe unakuwa liable kivipi?
 
Back
Top Bottom