Mpangaji mtata kulipa kodi na kuhama

Bingili

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
310
Reaction score
799
Wadau nina mpangaji kwenye nyumba yangu namdai kodi ya mwaka mzima 2019 na na huu sasa ni mwezi wa 3 2020.

Ana familia na watoto 4 wadogo wadogo
Nimeisha mpa notisi ya kuhama toka mwaka jana mwezi wa 8 alipe deni na kuhama lakini halipi na ahami.

Nimempeleka kwa balozi mara kadhaa lakini jamaa ahami na hela halipi.

Anapotea sijui hata huwa narudi saa ngapi kulala kila siku anajifanya kasafiri wakati yupo mjini.

Je nitumie taratibu gani kumtoa na notisi ya kuhama anayo na nakala ipo kwa balozi
Nikaninginizi kufuli au?

Naogopa nisije kuambiwa nanyanyasa watoto wakalala nje

Naombeni muongozo wa kisheria
 
Mbadilishie kufuri
 
Mkuu, mwambie ahame bila kulipa kwa sasa lakini muandikiane na conditions pia tena polisi. Kumbuka anawatoto huyo, ukimfunga watahangaika. Tenda wema nenda zako,haimanishi usipopata hiyo fedha utakufa au kuwa masikini forever. Namaanisha hivi bora upate mpangaji mpya kuliko uendelee kukosa kodi
 
Wema usikuzidi tafuta baunsa wamtoe kwa nguvu.

Siyo Kila Kiuzwacho Sokoni Chafaa Kununuliwa
 
Nilifanya hivi nilimpeleka kwa mtendaji hata hapo ulipo yupo, nikamwambia nampa notice ya masaa 24 na ninamlipa Kodi yake miezi mitatu. Sasa jiandae tafuta hiyo Kodi ya miezi mitatu haijalishi ni shilingi ngapi mpeleke Kwa mtenda samehe yote, andikishiani mpe Kodi yake. Pale pale na muda huo huo Mwambie mtendaji akupe watu uongozane nao wakatoe vyombo nje, hana la kubisha kama ni hela tayari umempa achukue familia yake akawaweke nyumba ya kulala wageni (Guest house) wakati anatafuta nyumba nyingine. Suluhisho la mwisho la mpangaji mkorofi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole kwa mkasa huo mkuu:-

USHAURI:
1. Njia ulokuwa unatumia wewe ni njia ya amani/diplomasia, ambayo tyr imeshindwa kuleta matunda.

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 103 (1) cha sheria ya Ardhi Na. 4/1999 utaratibu unaotakiwa kuufanya ni wa kimahakama, yaani kwa kufungua shauri la madai Mahakamani la kuiomba Mahakama itoe amri ya huyo mpangaji kuondoka (VACANT POSSESSION OF THE DEMISED PROPERTY).

3. Kifungu cha 167 cha sheria hiyo kinatamka Mahakama ni a). Baraza la Ardhi la kijiji, b). Baraza la kata, c). Baraza la Ardhi na nyumba la Wilaya, d). Mahakama kuu, na e). Mahakama ya Rufani (kwa rufaa pekee).

4. Hujatuambia kama upo mjini, ama Wilayani (vijijini) NA/AU Ardhi yako imepimwa ama laa. Mi natumai upo mjini, basi piga hesabu ya kodi yote unayodai kama haitazidi Milioni 300 (yaan 300,000,000/=) KAFUNGUE KESI YA KUMWONDOSHA katika Baraza la Ardhi na nyumba wilaya, ambalo lina mamlaka na eneo ulipo. (KUMBUKA: Mabaraza haya huwa ni ya kikanda sio kila wilaya). Kwa nini sijasema baraza la kata? Kwa sababu katika shauri la Ardhi Misc. Land Appeal No. 129 of 2009 Mahakama kuu ilitamka kuwa Mabaraza ya kata yaliyopo mijini hayana mamlaka na mashauri ya Ardhi.

HIVYO BASI KAFUNGUE KESI MAHAKAMA YA ARDHI ILI UKISHINDA UPEWE DALALI WA KUMWONDOSHA MPANGAJI KWA AMRI YA MAHAKAMA. KUNA POSITI NIMESOMA INASEMA MKAANDIKISHANE POLISI, IPO HIVI KWA MUJIBU WA SHERIA YA POLISI (SURA 322) PAMOJA NA POLICE GENERAL ORDER (PGO) POLISI HAIHUSIKI NA MASUALA YA MADAI BALI NI KWA JINAI PEKEE.

N.B Balozi wa nini karne hii ya 21?? Hata kwa sheria ya serikali za mitaa (Na. 7/1982) hayumo. ungeenda kwa M/Kitongoji ndo maana limekudharau.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni njia ya mazoea (tunaishi kwa mazoea) njia za mazoea ni za bahati na sibu (yaan jambo likiisha salama basi umefaulu).

Lakini WEO kufanya hivyo ni kukiuka wajibu wake ambao umewekwa katika marekebisho ya sheria Na. 13/2006 ambayo nilirekebisha Majukumu ya WEO kwny sheria mama ya Serikali za mitaa (Mamlaka ya Wilaya) sura 287 na pia ni kosa chini ya Sheria ya kupambana na rushwa Na. 11/2007.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna dingi hapa mitaa ya sombetini alikua anamdai mkaradi mmoja msaga gomba deni lilitoboa kama miezi 8 na ushee hivi!jamaa kaigwa sana notisi na pamene kasamehewa na yule dingi lakn chalii akaendeleza zarau yule dingi kumbe alikua bandidu kitambo vua siku hiyo likwa linanyesha akaja na fundi akamwambia toa bati ktk hichi chumba kinavuja sana mvua ikikata tutaweka bati mpya.fundi akatoa bati akapewa chake mkaradi akarudi kufungua mlango anakutana na mvua zaidi ya njee alicheka sana akahama mwenyewe.sasa wewe hicho chumba kibadirishe matumizi weka bafu tu
 
Unashaurije Kwa hili mkuu, mtu hataki kulipa Kodi, halipi maji wala umeme na hataki kuondoka hizo nyumba zimepangishwa zitusaidie sasa ili waondoke kwa haraka tufanye nini? Mimi nilifanya hivyo maana tulifikia kupelekana polisi, tena yeye ndiye aliyekuwa anakimbilia kushitaki kwamba ananyanyaswa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana Ila alitakiwa ang'oe bati na mwenye chumba yupo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi sheria ndio za kubadilisha aisee
Ndio maana jamaa anakiburi
Sasa hivi kakimbia familia naona anawatumia hela kwa mpesa au atakua anakuja usiku wa manane na kuondoka

Sasa hii mahakamani sijui kwa mabaraza ya wilaya si tutamaliza mwaka mzima naendesha kesi jamani

Yaani sipangishi tena huyu mwanaizaya akiondoka

Nashukuru kwa ushauri wa kisheria mkuu
 
Hii inataka moyo sana mkuu
Yaani namdai zaidi ya m3 halafu nimtafutie na kodi ya miezi 3 nimpe?

Shida nyingine hapatikani kila nikienda nakuta familia yake tu yeye labda anarudi usiku wa manane anasalimia na kusepa
Simu kabadili na no, mkewe muongo muongo kampa shule namna ya kunijubu eti kasafiri kwenye kazi zake
 
Nadhani hii njia inaweza kumkurupua huko aliko aje atoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…