Usijaribu kuweka kofuli lako kwenye mlango wa huyo mpangaji,kuna mzee alimeekea mpangaji wake kofuli juu ya kofuli lake ili kumshinikiza alipe kodi,mpangaji akaja usiku na kukuta kofuli la mwenye nyumba limefungwa mlangoni,alichofanya mpangaji ni kutafuta sehemu ya kulala usiku huo,kisha kesho yake akaenda kwa mtaalam mmoja wa kuchonga funguo,mtaalam akaenda kulicheki kofuli na kwenda kuchonga funguo,mpangaji akarudi usiku akiwa na funguo zote mbili akafungua chumba na kusomba kila kitu,baada ya hapo akarudisha kofuli zote mbili,kesho yake akarudi kwa mwenye nyumba akiwa na pesa taslim za kodi anayodaiwa,akajifanya kushangaa kukuta kofuli zaidi ya lile lake,akamwita mwenye nyumba na kumuuliza kama kofuli hilo ni lake,mwenye nyumba akamweleza kuwa kofuli ni lake na hatolitoa hadi alipwe kodi yake,basi mpangaji akaomba sana msamaha kwa kuchelewesha kodi na kumuomba muda kidogo akatafute hela amlipe,akatoka akazunguka kidogo kisha akarudi na pesa yote,mwenye nyumba akafungua kofuli lake na mpangaji akafungua lake,juingia ndani hakuna kitu!! Mpangaji akaita viongozi wa serikali ya mtaa akimtaka mwenye nyumba arudishe vyombo vyake,ilikuwa shughuli haswa,ila mwisho ilibidi mwenye nyumba amlipe mpangaji hela sawa na za kujengea hicho chumba na zaidi.
Sent using
Jamii Forums mobile app