Tupo wapangaji wanne tunaoishi hapa. Hatuishi na mwenye nyumba tuko wapangaji tuu wenyewe. Mwenye nyumba yeye anaishi mkoa mwingine.
Sasa kuna mpangaji ambaye tulimteua awe in charge wa kukusanya bill za maji, taka, umeme etc. hapa tunapokaa.
Hivyo jamaa ana access ya mawasiliano ya wapangaji wote hapa tunapoishi, kiufupi ana namba yangu na ya wife pia.
Sasa juzi niko na simu ya wife meseji ikaingia " nimekukosea nini mbona hujibu meseji zangu " Ikiwa imeseviwa jina la jamaa.
Kufatilia meseji za nyuma naona jamaa ni karibu miezi miwili sasa anajaribu kumtongoza wife, japo wife ameonekana kumkazia na kumsisitiza kuwa anaiheshimu ndoa yetu. Nimeona kupitia meseji. Ingiwa wife hajaniambia mimi hiki kinachoendelea.
Ushauri wadau. Vipi nimchane huyu jamaa kuwa aachane na wife, au nimpotezee kwanza kama sijui kinachoendelea.