DOKEZO Mpangaji wangu kageuza Nyumba yangu kuwa kiwanda bubu cha kutengeneza vinywaji vikali feki kama Konyagi, K Vant nk

DOKEZO Mpangaji wangu kageuza Nyumba yangu kuwa kiwanda bubu cha kutengeneza vinywaji vikali feki kama Konyagi, K Vant nk

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

dadamlamayao

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2022
Posts
243
Reaction score
841
Wapendwa habarini.Mimi ni Mtumishi wa Umma nipo Dodoma.Nina nyumba yangu nimeijenga Boko. Nilimaliza kuijenga Mei mwaka huu na Juni nikapata Mpangaji(Mme na Mkewe).

Nilishukuru maana Mpangaji huyu alijitambulisha kwamba ni Mfanyabiashara anayefuata mizigo China hivyo yupo busy sana, alinilipa Kodi ya miaka miwili(nilifurahi sana). Mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba jirani yangu ambaye tumetengana ukuta(fensi) alinipigia na kuniuliza kama nimeigeuza nyumba yangu kuwa godown au kiwanda cha kutengeneza vinywaji maana alidai kunakuwa na kelele za chupa kugongana usiku, nilimjibu hapana lakini nitafanya uchunguzi.

Juzi Jumapili nilikuwa Dar, hivyo mchana nilienda hapo Boko nyumbani kwangu bila kuwapa taarifa. Cha kushangaza nikakuta kafunga CCTV Camera kwenye pembe zote za fensi pamoja na kuweka Mlinzi getini. Nilivyojitambulisha getini Mlinzi hakufungua geti alinizuia kuingia(imagine nyumba yangu lakini nazuiliwa kuingia).

Nikiwa pale getini nahojiana na Mlinzi, ilikuja gari la Polisi ikasimama kwa mbali, kijana mmoja akatoka ndani ya nyumba yangu na kwenda kwenye ile gari na kuwapa naamini pesa na gari ya Polisi ikaondoka, kijana akarudi akaingia ndani, akafunga mlango, hapo mimi nimezuiwa getini. Kwa kifupi ni kwamba Mpangaji wangu huyu anazalisha bidhaa feki(vinywaji feki) na kuziingiza sokoni.

Msiri wangu ameniambia Konyagi, K-Vant, Gin na vinywaji vingine vikali vinazalishwa ndani ya nyumba yangu na kuingizaa sokoni. Naogopa asije akakamatwa mwisho wa siku Serikali ikataifisha nyumba yangu maana nimeambiwa hilo ni Kosa la Uhujumu Uchumi.

Naomba msaada taarifa hii nikaitoe wapi maana msiri wangu kaniambia Polisi wanajua na huwa wanaenda kuchukua posho kama nilivyoshuhudia mimi mwenyewe hivyo hata nikiripoti kwao itakuwa ni kazi bure.

Naomba mwenye mawasiliano na Viwanda vinavyotengeneza Konyagi, K Vant na hizi Pombe Kali za chupa anisaidie tafadhali Ili niwajulishe tushauriane cha kufanya

Nitashukuru sana wapendwa, siku njema
 
Wewe ni mtumishi wa umma na hujui pa kuripoti? Hiyo nyumba ni yako ama ulupewa zawadi siku ya send off yako?
Wapendwa habarini.Mimi ni Mtumishi wa Umma nipo Dodoma.Nina nyumba yangu nimeijenga Boko.Nilimaliza kuijenga Mei mwaka huu na Juni nikapata Mpangaji(Mme na Mkewe).Nilishukuru maana Mpangaji huyu alijitambulisha kwamba ni

Nitashukuru sana wapendwa,siku njema
 
Wapendwa habarini.Mimi ni Mtumishi wa Umma nipo Dodoma.Nina nyumba yangu nimeijenga Boko.Nilimaliza kuijenga Mei mwaka huu na Juni nikapata Mpangaji(Mme na Mkewe).Nilishukuru maana Mpangaji huyu alijitambulisha kwamba ni
Je mkataba wako wa nyumba una sharti kuwa hiyo ni nyumba ya makazi tu? Mkataba utakulinda kwenye hili, ilapopote utakapotoa taarifa.. ukiondoa viwanda vya hizo pombe kali, wataenda kuchukua rushwa na wewe utaonekana mbaya kwani watakuchoma.
 
Back
Top Bottom