DOKEZO Mpangaji wangu kageuza Nyumba yangu kuwa kiwanda bubu cha kutengeneza vinywaji vikali feki kama Konyagi, K Vant nk

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ukipangisha nyumba hata kama ni room moja,hiyo nyumba inakuwa ya huyo mpangaji Kwa sababu amekulipa fedha ya Kodi,Sasa unapotaka kuingia Tena kwenye hiyo nyumba jinsi unavyotaka unakosea,Kwa sababu anaishi mtu mwingine hapo,nampongeza huyo mpangaji Kwa kuweka ulinzi wa kamera na askari getini,maana wenye nyumba wengine Hawana staha.
 
Ilibidi nicheke tu, Watanzania wengi ni waropokaji na ujuaji feki nakumbuka miaka hiyo radio free walikuwa na kipindi cha nani mkali sasa ukipiga simu lazima utaje nani anaepbaniswha nae.

Ndio kimejirudia ulichomuuliza jamaa amesema hata kidogo??
Kwamba hujasoma chochote alichoandika ukaamua ku comment tu?
 
Amesha kuwa kodi ya miaka miwili / tulizana!, Tunza mkataba wako na yeye, dunia haipo fair!, (usije tengeneza mazingira ya ukaishi huku unawindwa, waone jamaa wa double kick wata respond quickly, na huyo jamaa anaweza kupewa 30yrs To jail. / maisha haya!
 
Wapendwa habarini.Mimi ni Mtumishi wa Umma nipo Dodoma.Nina nyumba yangu nimeijenga Boko.Nilimaliza kuijenga Mei mwaka huu na Juni nikapata Mpangaji(Mme na Mkewe).Nilishukuru maana Mpangaji huyu alijitambulisha kwamba ni Mfanyabiashara anayefuata mizigo China hivyo yupo busy sana,alinilipa Kodi ya miaka miwili(nilifurahi sana).Mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba jirani yangu ambaye tumetengana ukuta(fensi)alinipigia na kuniuliza kama nimeigeuza nyumba yangu kuwa godown au kiwanda cha kutengeneza vinywaji maana alidai kunakuwa na kelele za chupa kugongana usiku,nilimjibu hapana lakini nitafanya uchunguzi.

Juzi Jumapili nilikuwa Dar, hivyo mchana nilienda hapo Boko nyumbani kwangu bila kuwapa taarifa. Cha kushangaza nikakuta kafunga CCTV Camera kwenye pembe zote za fensi pamoja na kuweka Mlinzi getini.Nilivyojitambulisha getini Mlinzi hakufungua geti alinizuia kuingia(imagine nyumba yangu lakini nazuiliwa kuingia).

Nikiwa pale getini nahojiana na Mlinzi ,ilikuja gari la Polisi ikasimama kwa mbali, kijana mmoja akatoka ndani ya nyumba yangu na kwenda kwenye ile gari na kuwapa naamini pesa na gari ya Polisi ikaondoka, kijana akarudi akaingia ndani,akafunga mlango, hapo mimi nimezuiwa getini. Kwa kifupi ni kwamba Mpangaji wangu huyu anazalisha bidhaa feki(vinywaji feki) na kuziingiza sokoni.

Msiri wangu ameniambia Konyagi, KVant, Gin na vinywaji vingine vikali vinazalishwa ndani ya nyumba yangu na kuingizaa sokoni. Naogopa asije akakamatwa mwisho wa siku Serikali ikatahifisha nyumba yangu maana nimeambiwa hilo ni Kosa la Uhujumu Uchumi.

Naomba msaada taarifa hii nikaitoe wapi maana msiri wangu kaniambia Polisi wanajua na huwa wanaenda kuchukua posho kama nilivyoshuhudia mimi mwenyewe hivyo hata nikiripoti kwao itakuwa ni kazi bure.

Naomba mwenye mawasiliano na Viwanda vinavyotengeneza Konyagi,K Vant na hizi Pombe Kali za chupa anisaidie tafadhali Ili niwajulishe tushauriane cha kufanya

Nitashukuru sana wapendwa,siku njema
pambana ukomboe nyumba yako mkuu!!
 
Mwambie awe anakupa asilimia 30 ya faida
 
Back
Top Bottom