DOKEZO Mpangaji wangu kageuza Nyumba yangu kuwa kiwanda bubu cha kutengeneza vinywaji vikali feki kama Konyagi, K Vant nk

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kama polisi Wanavuta ni ngumu kwake kukamatwa na sijui kama uhujumu uchumi wa hivyo nyumba hutaifishwaa

Mpangaji wa kunilipa kodi miaka miwili ningeimba Halleluya
Kwakweli,mi nikipata mpangaji wa hivyo akae tu, kwwnye mkataba ndio naweka vipengele vigumu kwamba hata ikitokea nyumba yangu haiingii hatiani
 
Wapendwa habarini.Mimi ni Mtumishi wa Umma nipo Dodoma.Nina nyumba yangu nimeijenga Boko.Nilimaliza kuijenga Mei mwaka huu na Juni nikapata Mpangaji(Mme na Mkewe).Nilishukuru maana Mpangaji huyu alijitambulisha kwamba ni Mfanyabiashara anayefuata mizigo China hivyo yupo busy sana,alinilipa Kodi ya miaka miwili(nilifurahi sana).Mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba jirani yangu ambaye tumetengana ukuta(fensi)alinipigia na kuniuliza kama nimeigeuza nyumba yangu kuwa godown au kiwanda cha kutengeneza vinywaji maana alidai kunakuwa na kelele za chupa kugongana usiku,nilimjibu hapana lakini nitafanya uchunguzi.

Juzi Jumapili nilikuwa Dar, hivyo mchana nilienda hapo Boko nyumbani kwangu bila kuwapa taarifa. Cha kushangaza nikakuta kafunga CCTV Camera kwenye pembe zote za fensi pamoja na kuweka Mlinzi getini.Nilivyojitambulisha getini Mlinzi hakufungua geti alinizuia kuingia(imagine nyumba yangu lakini nazuiliwa kuingia).

Nikiwa pale getini nahojiana na Mlinzi ,ilikuja gari la Polisi ikasimama kwa mbali, kijana mmoja akatoka ndani ya nyumba yangu na kwenda kwenye ile gari na kuwapa naamini pesa na gari ya Polisi ikaondoka, kijana akarudi akaingia ndani,akafunga mlango, hapo mimi nimezuiwa getini. Kwa kifupi ni kwamba Mpangaji wangu huyu anazalisha bidhaa feki(vinywaji feki) na kuziingiza sokoni.

Msiri wangu ameniambia Konyagi, KVant, Gin na vinywaji vingine vikali vinazalishwa ndani ya nyumba yangu na kuingizaa sokoni. Naogopa asije akakamatwa mwisho wa siku Serikali ikatahifisha nyumba yangu maana nimeambiwa hilo ni Kosa la Uhujumu Uchumi.

Naomba msaada taarifa hii nikaitoe wapi maana msiri wangu kaniambia Polisi wanajua na huwa wanaenda kuchukua posho kama nilivyoshuhudia mimi mwenyewe hivyo hata nikiripoti kwao itakuwa ni kazi bure.

Naomba mwenye mawasiliano na Viwanda vinavyotengeneza Konyagi,K Vant na hizi Pombe Kali za chupa anisaidie tafadhali Ili niwajulishe tushauriane cha kufanya

Nitashukuru sana wapendwa,siku njema
Yani hapo ni kutulia na kuchukua maamuzi sahihi. Kama itafaa Mpe miezi mitatu ya kuhama. Umwambie unarudi kuishi Dar.
Miezi iliyobaki umrudishie Pesa zake.

Halafu pia angalia upya Mkataba wako.

Mlikubaliana nini wakati anakuja kupanga Hadi kufikia hatua ya kuweka Camera.
 
Njoo pm mkuu
 
Atakimbiliaje polisi bila kuanza kureport kwa mjumbe na ofisi ya serikali yake kwanza kutoa taarifa
Hao watu wa mtaa ndiyo wanajukumu la kumuita/kuwaita wote wawili na kuwasikiliza
Polisi hiyo kwenda ni hatua nyingine kama wakishindwanda

We mleta uzi mtumishi wa umma gani hata procedure huzijui

Ova
 
Si ndo wale wale 😅

Yani hapo ni kutulia na kuchukua maamuzi sahihi. Kama itafaa Mpe miezi mitatu ya kuhama. Umwambie unarudi kuishi Dar.
Miezi iliyobaki umrudishie Pesa zake.

Halafu pia angalia upya Mkataba wako.

Mlikubaliana nini wakati anakuja kupanga Hadi kufikia hatua ya kuweka Camera.
Notes ni kupoteza muda na pesa. Aende pm kuna ujumbe wa kumfaa hauhitaji gharama
 
Atakimbiliaje polisi bila kuanza kureport kwa mjumbe na ofisi ya serikali yake kwanza kutoa taarifa
Hao watu wa mtaa ndiyo wanajukumu la kumuita/kuwaita wote wawili na kuwasikiliza
Polisi hiyo kwenda ni hatua nyingine kama wakishindwanda

We mleta uzi mtumishi wa umma gani hata procedure huzijui

Ova
Mjumbe ata haribu asiende polisi wala kw mtendaji mpangaji ata mfanyia visa
 
Wapendwa habarini.Mimi ni Mtumishi wa Umma nipo Dodoma.Nina nyumba yangu nimeijenga Boko.Nilimaliza kuijenga Mei mwaka huu na Juni nikapata Mpangaji(Mme na Mkewe).Nilishukuru maana Mpangaji huyu alijitambulisha kwamba ni Mfanyabiashara anayefuata mizigo China hivyo yupo busy sana,alinilipa Kodi ya miaka miwili(nilifurahi sana).Mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba jirani yangu ambaye tumetengana ukuta(fensi)alinipigia na kuniuliza kama nimeigeuza nyumba yangu kuwa godown au kiwanda cha kutengeneza vinywaji maana alidai kunakuwa na kelele za chupa kugongana usiku,nilimjibu hapana lakini nitafanya uchunguzi.

Juzi Jumapili nilikuwa Dar, hivyo mchana nilienda hapo Boko nyumbani kwangu bila kuwapa taarifa. Cha kushangaza nikakuta kafunga CCTV Camera kwenye pembe zote za fensi pamoja na kuweka Mlinzi getini.Nilivyojitambulisha getini Mlinzi hakufungua geti alinizuia kuingia(imagine nyumba yangu lakini nazuiliwa kuingia).

Nikiwa pale getini nahojiana na Mlinzi ,ilikuja gari la Polisi ikasimama kwa mbali, kijana mmoja akatoka ndani ya nyumba yangu na kwenda kwenye ile gari na kuwapa naamini pesa na gari ya Polisi ikaondoka, kijana akarudi akaingia ndani,akafunga mlango, hapo mimi nimezuiwa getini. Kwa kifupi ni kwamba Mpangaji wangu huyu anazalisha bidhaa feki(vinywaji feki) na kuziingiza sokoni.

Msiri wangu ameniambia Konyagi, KVant, Gin na vinywaji vingine vikali vinazalishwa ndani ya nyumba yangu na kuingizaa sokoni. Naogopa asije akakamatwa mwisho wa siku Serikali ikatahifisha nyumba yangu maana nimeambiwa hilo ni Kosa la Uhujumu Uchumi.

Naomba msaada taarifa hii nikaitoe wapi maana msiri wangu kaniambia Polisi wanajua na huwa wanaenda kuchukua posho kama nilivyoshuhudia mimi mwenyewe hivyo hata nikiripoti kwao itakuwa ni kazi bure.

Naomba mwenye mawasiliano na Viwanda vinavyotengeneza Konyagi,K Vant na hizi Pombe Kali za chupa anisaidie tafadhali Ili niwajulishe tushauriane cha kufanya

Nitashukuru sana wapendwa,siku njema
Kufanya hivyo utaokoa maisha ya wengi kwa kuponya figo zao na macho.
 
Mwite ongea naye kiume. Mrudishie pesa iliyobaki ahame. Kwenda polisi au kwa mjumbe utajizulia mengine. Zaidi, hata kama nyumba ni yako siyo ukurupuke tu na uruhusiwe kuingia. Kuwa mstaarabu.
 
Back
Top Bottom