Mpango: Kiongozi usifikiri nafasi yako haiwezi kuzibwa

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Akiongea mbele ya Rais Samia Ikulu leo July 26, 2024 wakati wa uapisho wa viongozi walioteuliwa Makamu wa Rais Philip Mpango amesema;

Pia soma: Rais Samia: Cheo ni sawa na nguo ya kuazima ambayo siku yoyote mmiliki wa nguo anaweza kuichukua!

“Niwapongeze wote walioteuliwa mmepewa dhamana kubwa ni matumaini ya Mh. Rais na Watanzania kwamba mtakwenda kucheza vizuri katika nafasi hizo niwaombe moja tu asije akafikiria yoyote yule nikiwemo Mimi Makamo wako Mheshimiwa Rais kwamba nafasi yangu haiwezi kuzibwa.”

“Ni muhimu sana kuzingatia kama Viongozi kwamba Amiri Jeshi Mkuu wakati wowote anaweza kutengeneza Timu yake ili kupata ushindi, kuwaletea ushindi Watanzania.”

Naona vijembe kwa Nape na January bado vinaendelea, ni humu tu!


Your browser is not able to display this video.

 
Unakuta mtu anasema "utanikumbuka" so what? Unakaa pembeni anaingia mtu mwingine maisha yanaendelea.
 
Je, Rais anaweza kumbadilisha makamu wake??
 
kwahiyo samia asufikiri hata kidogo kwamba wapinzani hawawezi ongoza nchi.....kisa yeye amepata nafasi basi asidharau ambao bado hawajaipata hiyo nafasi akidhania yeye tu ndio anaiwezea. Mpango mtu makini sana...tunamshukuru kwa uelewa wake mpana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…