Mpango mkakati na dunia isiyotabirika (Strategic planning process in unpredictable world)

Mpango mkakati na dunia isiyotabirika (Strategic planning process in unpredictable world)

Joined
Jul 3, 2016
Posts
19
Reaction score
13
Habari za majukumu wapendwa.
Ni matumaini yetu kwamba nyote mu-wazima na mnaendelea vyema na majukumu ya ujenzi wa Taifa letu tukufu la Tanzania.

Leo tungelipenda ku-share nanyi juu ya mada tajwa hapo juu.

Mafanikio halisi ya biashara au kampuni yoyote ile kwa kiasi kikubwa hutegemea uwepo wa Mpango Mkakati madhubuti (Effective Strategic Plan).
Tukianza na neno MKAKATI, neno hili hutafsiriwa kama tendo (action) )au mkusanyiko wa matendo (actions) ambayo hufanywa na mameneja wa makampuni kwa lengo la kuongeza ufanisi wa kampuni husika (Company's performance).
Kupitia utekelezaji wa mipango mikakati ndipo kampuni husika huweza kupata kile kinachoitwa " Faida ya kiushindani" au Competitive Advantage.
Pindi mpango mkakati unapoiwezesha kampuni kufanya vyema sokoni dhidi ya washindani wake, tunasema kampuni ina " Faida ya kiushindani" au Competitive Advantage.

Utayarishaji wa mpango mkakati hujumuisha hatua mbalimbali ambazo ni :
  1. Uchaguzi wa kauli ya utume wa kampuni (Mission statement) na malengo ya kampuni (Corporate goals)
  2. Uchambuzi juu ya hali ya nje ya kiushindani, ambayo hujumuisha fursa (opportunities) na changamoto (challenges/threats)
  3. Uchambuzi juu ya hali ya ndani ya kiutendaji wa kampuni, hii hujuimuisha uimara/uthabiti (strength) na udhaifu (weakness)
  4. Kuchagua mikakati ambayo itaimarisha uimara wa kampuni (strengths) na kuweza kusahihisha madhaifu ya kampuni (weaknesses) ili kuiwezesha kampuni kuziendea fursa za nje (opportunities) na kukabiliana na changamoto za nje pia (challenges/threats)
  5. Utekelezaji wa mkakati (Strategy implementation)

Uandaaji wa mikakati ya kiushindani katika biashara huweza kufanyika katika njia mbili ambazo ni:
  1. Njia rasmi (Formal strategic planning process), njia hii huja na mkakati kusudiwa (intended strategy)
  2. Njia isiyo rasmi (Informal strategic planning process), njia hii huja na mkakati wa dharura (emergent strategy)
Njia hizi mbili hutokana na aina ya dunia ya kibiashara tunayoishi sasa. Mazingira ya kibiashara katika dunia ya leo hayatabiriki (unpredictable). Kumekuwa na ukosoaji katika uandaaji wa mipango mikakati ya ushindani katika biashara kwa kufuata njia rasmi, na hii hutokana na kutokutabirika kwa dunia ya kibiashara. Ni mara nyingi na kwa makampuni mengi mipango mikakati waliyoiandaa mwanzo ilishindwa kuwaletea kile walichotaraji hivyo kwa mameneja wepesi wa kukabiliana na mazingira waliweza kubadili mikakati na kuja na mikakati mipya tofauti na iliyoandaliwa hapo mwanzo (emergent strategy) na kuweza kuendelea na biashara, kwa mameneja walioshindwa kukabiliana na mabadiliko walitolewa katilka ushindani.

Japo kumekuwepo na ukosoaji katika utumiaji wa njia rasmi za uandaaji wa mipango mikakati ya kiushindani (Formal strategic planning process), tafiti nyingi zinaonyesha kwamba njia hii imekuwa ikiwasaidia mameneja wa makampuni mbalimbali katika kufanya maamuzi ya kimkakati na hatimaye kuleta ufanisi katika kampuni zao.

Japo haiondoi ukweli kwamba tupo katika ulimwengu usiotabirika kibiashara (unpredictable business world), ni vyema mfanyabiashara anaposuka mikakati ya kiushindani katika biashara akazingatia kipengele cha " What-If" hii njia ambayo humuwezeshaa mfanyabiashara, kuzingatia hali zote mbili, kwa maana: hali aitarajiayo (Optimistic scenario) na hali asiyoitarajia (Pessimistic scenario), ili pale mabadiliko yanapokuja mbeleni aweze kukabiliana nayo.
Hii ni njia ambayo hutumiwa sana na makampuni makubwa katika mikakati yao ya kiushindani, kitaalamu huitwa SCENARIO-PLANNING METHOD

Shukrani nyote

Kwa mahitaji ya huduma zifuatazo
  • Uandishi wa michanganuo ya miradi (Project Proposals).
  • Uandishi wa mipango ya kibiashara na mipango mikakati (Business Plans & Business Strategic Plans)
  • Utoaji wa ushauri wa kitaalamu katika maeneo ya Project Planning and Management, Business Development and Management and Operations Management.
  • Utoaji wa semina na warsha katika maeneo tutoleayo ushauri wa kitaalamu.
Usisite kututafuta kwa namba 0719 518 367, 0783 695 639
E-mail platinumconsultancy74@gmail.com

Nyote mnakaribishwa
 
Back
Top Bottom