Mpango wa Bakery 2026 na Ombi la Mawasiliano ya Wauzaji wa Mashine za Kukanda Unga

Mpango wa Bakery 2026 na Ombi la Mawasiliano ya Wauzaji wa Mashine za Kukanda Unga

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
563
Reaction score
1,567
Ndugu na mdau wa jukwaa hili ninatumia nafasi hii kuwasilisha wazo langu la biashara kwa mwaka huu wa 2026, nikiwa na matumaini ya kupata mrejesho, ushauri wa moja kwa moja, na hasa mawasiliano ya wadau wanaohusika na uuzaji wa mashine za kuoka na kukanda unga.

Nina mpango wa kuanzisha biashara ndogo ya bakery itakayojikita katika uzalishaji wa bidhaa za msingi zenye mahitaji ya kila siku, ikiwemo mandazi, mikate na skonzi. Mkakati wangu ni kuanza kwa kiwango kidogo kulingana na uwezo uliopo, kisha kupanua huduma taratibu kulingana na mahitaji ya wateja na mzunguko wa soko.

Chanzo cha wazo hili ni ujasiri wa kuanza na kile kilichopo. Kwa sasa ninakusanya nguvu kwa sababu mwaka ndiyo umeanza naimani mtaji nitapata ninachokosa kwa sasa ni mashine, lakini rasilimali zingine muhimu ninazo kama mtaji wa awali: nina pikipiki ni mpya na baiskeli. Kwa watu wa masoko wanaelewa Vifaa hivi vina umhimu gani mimi naviona kama nyenzo za kimkakati za usambazaji, utafutaji wa masoko, na kuwafikia wateja moja kwa moja, kwa kutumia usafiri huu unaweza kuwafikia wateja wengi.

Kwa upande wa mitambo, ningependa kujua kwa usahihi kuhusu bei na upatikanaji wa mashine za kukanda unga wa ngano kuanzia uwezo wa kilo 25 (25kg dough mixer). Ningeomba msaada kwa yeyote anayefahamu:

Kampuni au wauzaji wanaoaminika ndani ya Tanzania,

Mashine imara zinazofaa kwa biashara ndogo inayoanza,

Mashine zinazoweza kuhimili changamoto za kukatika kwa umeme mara kwa mara, jambo ambalo ni la kawaida kwenye maeneo mengi yanayohudumiwa na TANESCO.


Nasisitiza kuwa kwa sasa silengi mijadala ya jumla kuhusu changamoto za biashara hii. Nafahamu changamoto ni sehemu ya safari ya ujasiriamali, na naamini nikianza nitajifunza kwa vitendo. Kipaumbele changu kwa sasa ni kupata taarifa za vitendo kuhusu mashine na wadau husika.

Kwa yeyote: Anayeuza mashine za kukanda unga, Anayefahamu wauzaji au kampuni zinazohusika, Au mwenye uzoefu wa moja kwa moja na mashine hizi na anaweza kupendekeza kwa uaminifu, tafadhali naomba mchango wako hapa au kupitia ujumbe binafsi.

Naamini mwaka ndiyo unaanza tunaanza nao kwa kuambatana na malengo, nidhamu na maamuzi sahihi, hata kuanzia sifuri kunawezekana. Nipo tayari kujifunza, kushirikiana na kuchukua hatua.

Asanteni naomba ushirikiano wako.

Mawasiliano yangu; 0768 966 075 WhatsApp
 
Formula ya mikate bomba

Ngano 1kg
Yeast 30g
Salt 23g
Sugar 125g
Oil 450
Water

Moto 120
 
Back
Top Bottom