Blessed Tajiri
Member
- Dec 16, 2023
- 57
- 82
Utangulizi
Serikali hufanya maamuzi mbalimbali kwa niaba ya wananchi, baadhi ya mambo huhitaji maoni ya wananchi na wakati mwingine wadau katika sekta husika (ambao huwakilisha wananchi) ili kuhakikisha mipango mizuri na huduma bora zinazaliwa kutokana na maoni hayo. Imekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wadau kulalamika maoni yao kupuuzwa, ama kufanywa ulaghai wa maoni kupokelewa lakini mwisho wa siku Sheria na Sera zikiletwa mazani zinakuwa na maoni ya “Wahuni” badala ya Wadau, mfano wa karibu ni jinsi wadau walivyolalamika maoni yao kupuuzwa kwenye Sheria za Uchaguzi za mwaka 2024. Wakati mwingine serikali huita wadau kwa mazungumzo ya kawaida, baada ya kumaliza mazungumzo hayo unashangaa serikali inatoa taarifa kuwa imekutana na wadau na wametoa maoni yao, wakati kiuhalisia hilo halikuwa dhumuni.
Ni yapi madhara ya kupuuza maoni ya wananachi na wadau;
Nini kifanyike;
Serikali kwa kushirikiana na Wadau iweke Sheria na kanuni zitakazoonesha namna ushiriki wa wadau na wananchi unavyotakiwa kufanyika pamoja ukomo ambao usipofikiwa basi maamuzi hayatakiwi kupelekwa hatua nyingine (Bungeni). Sheria na Kanuni hizo zinatakiwa kuanisha vigezo hivi;

- Kupata Sheria na Sera ambazo haziendani na majitaji ya wananchi – Hii ni kwasababu maoni yaliyofanyiwa kazi siyo ya wananchi wanaopitia changamoto husika, mwisho wa siku Sheria na Sera hizo zinaenda kunufaisha watu wachache na siyo walengwa.
- Wananchi na Wadau kuwavunja moyo wasitoe mapendekezo yao pale wanapohitajika kufanya hivyo wakati mwingine – Wananchi na wadau wakishaona wanapuuzwa mara zote wanapotoa maoni ni dhahiri wataona jambo hilo halina maana tena kwao, na kuiachia serikali ifanye inavyotaka bila kujali ubora wa huduma watakazopatiwa.
- Kuendeleza vitendo vya rushwa, ubadhirifu wa fedha na uvunjivu wa Kanuni na Sheria za Utumishi wa Umma – Kutojumuisha maoni ya wananchi na wadau kwanza inamaanisha gharama zilizotengwa kutumika kupata maoni hayo zimeenda bure, kurusu maoni ya ‘wahuni’ badala ya wananchi ni kwenda kinyume cha utaratibu na Sheria zinavyotaka, lakini pia mpaka maoni ya wahuni wanapita inamaana hayajapita bure, lazima kuna bahasha ilipita kurahisisha mchakato huo kufanyika na hivyo kufanya vitendo hivyo kuonekana kawaida na kuwa mfano mbaya kwa wananchi na wadau wanaotakiwa kujifunza kutoka kwa aliye bora na anayetenda anavyovihimiza (Serikali).
- Upatikanaji wa Sheria mbovu na kandamizi kwa wananchi – Hii ni kwasababu maslahi yanayoangaliwa hapa siyo ya wananchi bali ya kikundi kidogo kinachotaka kuwanyonya na kuwaonea wananchi. Jambo linalochekesha na kusikitisha ni kuwa viongozi hawa wanaopitisha maoni ya wahuni hudhani kuwa watabaki kuwa viongozi milele, huwa wanasahau uongozi huisha na kesho atakuwa mwananchi wa kawaida ambaye Sheria hizi zitamkata pia, lakini pia mambo hubadilika, leo anaweza kuwa na kinga kesho kinga hiyo ikatolewa na wao wakataabika vile, mara nyingi huwa wananshituka pale yakiwakuta! Tuna Sheria mbovu nyingi sana nchini, na hizi kwa kiasi kikubwa zinatokana na kutofanyia kazi maoni ya wananchi na wadau.
- Kudhoofisha Demokrasia – Demokrasia ni mfumo unaounga mkono ushirikishwaji wa wananchi kwenye maamuzi. Kama wananchi hawashirikishwi inamaana serikali haipo kwa maslahi ya wananchi, na wala maoni ya wananchi hawasikilizwi, yanapuuzwa!
- Kukosa uaminifu kwa serikali pamoja na taasisi zake – Wananchi wana matarajio makubwa kwa serikali yao wakiamini watatendewa kwa haki, kupewa kipaombele pamoja na kuthaminiwa. Kama maoni yao hayafanyiwi kazi na kupuuzwa, Imani kwa serikali yao pia hufa, na hapa ndio hutokea masuala ya kujichukulia Sheria mkononi, kwasababu serikali inakuwa imewaangusha.
Nini kifanyike;
Serikali kwa kushirikiana na Wadau iweke Sheria na kanuni zitakazoonesha namna ushiriki wa wadau na wananchi unavyotakiwa kufanyika pamoja ukomo ambao usipofikiwa basi maamuzi hayatakiwi kupelekwa hatua nyingine (Bungeni). Sheria na Kanuni hizo zinatakiwa kuanisha vigezo hivi;
- Kuainisha mambo yote yanayotakiwa kutolewa maoni ya wananchi pamoja na wadau. Ikitokea mchakato huo unahitaji wananchi kutoa maoni, basi iwe lazima kwa serikali kuelimisha umma juu ya Sera au muswada huo kabla ya mchakato wa kutoa maoni sababu wengi huwa hawana uelewa wa kutosha na hivyo kuhitaji msaada wa kuwaelewesha ili waweze kushiriki inavyostahili.
- Baada ya maoni kupokelewa, serikali inatakiwa kuyaweka vizuri na kusambaza nakala kwa wadau (ikiwa suala hilo lilishirikisha na wananchi pia kwa ujumla wao, wadau watasimama kama wawakikilishi wao) amapo itaeleza mchakato wote uliofanyika mpaka kufanikiwa kubakiwa na maoni machache waliyoona yanafaa kwenda hatua nyingine. Hapa utatolewa muda usiopungua siku tatu kwa wadau kupitia na kuhakikisha kuwa maoni yaliyowasilishwa ndiyo yaliyofanyiwa kazi. Wakiridhishwa na hilo watatakiwa kusaini kukubali maoni yao yawasilishwe bungeni kwa mjadala zaidi. Kama kuna maboresho, watatakiwa kuyaainisha, ambapo Serikali itatakiwa kuboresha nakala hizo na kuyarudisha tena kwa wadau kwaajili ya kupitishwa.
- Sheria na Kanuni zitatakiwa kusema kiwango cha asilimia ya wadau ambapo isipotimia basi Sera au muswada huo hautaweza kuendelea hatua nyingine. Hapa wadau watatakiwa kutoa sababu iliyofanya wagome kukubaliana na nakala hizo. Serikali itatakiwa kupokea maoni hayo na kufanya maboresho yanayohitajika na kisha kuirudisha tena kwa wadau ili waipitie upya kuhakikisha kila kitu kipo sawa. Ikiwa wadau hawatakubaliana na maboresho hayo kwa mara ya pili, serikali itatakiwa kufanya zoezi la kupokea maoni upya, sababu hii itamaanisha maoni ya wadau na wananchi hayakufanyiwa kazi, yaani yamepuuzwa.
- Endapo Sera au Sheria iliyopitishwa haitakuwa na maoni ya wadau; hapa inamaanisha wahuni (kama wale aliowaita Balozi Polepole) wamewanyima haki Watanzania. Kanuni ziweke kipengele cha wadau kupinga Sheria/Sera hizo Mahakamani, ambapo baada ya Mahakama kujiridhisha kuwa ni kweli itaagiza mchakato huo kufanyika upya.
Upvote
9