Bwana yesu asifiwe......
Nianze Kwa kushukuru MUNGU muumba mbingu na nchi na vyote viijazavyo Kwa, kutujalia amani, upendo na mshikamano.
SULUHISHO LA UKOSEFU WA AJIRA
-Ukosefu wa ajira ni janga linaloitafuna nchi yetu ya Tanzania, hivyo ili Kuondoa au kupunguza tatizo hili yafuatayo lazima yazingatiwe na serikali;-
1.Udahili wa wanafunzi vyuoni
-Udahili wa wanafunzi vyuoni uzingatie, asilimia 20 shahada, asilimia 30 stashahada, asilimia 50 ufundi Kwa Kila mwaka wa masomo.
-Hii ni kutokana na serikali imekuwa ikizalisha wahitimu wengi wa vyuo vikuu ambao ni wasimamizi na sio wazalishaji, wanasomeshwa Kwa fedha nyingi za serikali Kisha wanatelekezwa bila kazi na kuambiwa wajiajili ili hali wanatoka katika familia masikini. Je serikali imeshindwa kuwapa mtaji ili wajiajili?
-Wanafunzi watakaochaguliwa kwenda vyuo vikuu wawe na division one tu na wapewe mikopo 100% na kuhakishiwa kupewa ajira.
-wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga na stashahada wawe na division 1,2 na serikali itoe ruzuku ya kuwasomesha.
-Wanafunzi watakaochaguliwa vyuo vya ufundi wawe na division 1,2,3 na serikali itoe ruzuku.
-Kulingana na makala ya B.B.C News 2023, waziri wa nchi, tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) wa serikali ya jamhuli ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Angelina kairuki alizungumza na vyombo vya habari na kueleza kuwa , waombaji 419 walidanganya ni walemavu kati ya waombaji 171,916 walioomba katika kada ya ualimu na afya kupitia wizara hiyo. Katika kada hizo mbili waliopata ajira ya ualimu ni 13,130, upande wa afya ni 5,319. Jumla Yao waliopata ni 18,449, walioachwa ni 153,512 hii inatoa picha Pana ya tatizo la ukubwa wa ajira.
-Serikali ipunguze idadi ya kudahili walimu na kufuta astashahada, pia serikali ielekeze nguvu kubwa kwenye vyuo vya ufundi Kwa sababu wanaajilika na kujiajiri kirahisi.
2. Wahitimu wote wa vyuo baada ya kuhitimu chuo waende internship kupata leseni na uzoefu wa kazi.
-Wahitimu wengi wanapokuwa wamehitimu masomo Yao wanakuja na elimu ile ya kwenye madesa , inasikitisha kwamba kinachofundishwa chuoni ni tofauti na unachokikuta mtaani, ndio maana mtaani wanasema fundi mzuri ni wa mtaani na sio aliehitimu chuo na kutunukiwa cheti.
- Inanisikitisha kuwa toka chekecheo hadi chuo kikuu mtu anafundishwa mawazo (theory) ya wazungu vitu ambavyo mtaani huvikuti mfano colonial education, colonial economy, pan Africanism......, ivi huyu mtu ni lini atatawala mazingira yake ili aweze kujiajiri? Ndio maana ambao hawakwenda shule wanaona fursa sana Kwa sababu hawajawa brainwashed kama wasomi.
-Elimu iwe ya kumsaidia mwanafunzi kutawala mazingira yake zaidi kuliko kusoma kuhusu ulaya for what?
-Hivyo basi vyuo vitakapozalisha wasomi wenye weledi na uwezo mzuri wa ufanyaji kazi naamini wataajirika hata nje ya nchi.
3. Tanzania ipige marufuku kusafirisha malighafi isiyochakatwa kwenda nje ya nchi.
-Kama ilivyo kuwa enzi za ukoloni malighafi zisizochakatwa zilipelekwa Kwa wingi kwenda kulisha viwanda huko ulaya, na ndivyo ilivyo Hadi leo Kwa Tanzania yetu.
-Serikali ikaribishe wawekezaji wa kuweza kuchakata malighafi na kuuza bidhaa au malighafi safi.
-Mfano maeneo ya Tarime, Bunda, Butiama, baadhi ya wakenya wanapenya na kukusanya mazao na kuyapeleka Kenya, ombi langu Kwa serikali watu hawa wapigwe marufuku kuingia nchini bila kibali, na wakitaka mazao wachukulie masokoni na si vinginevyo na yawe yamechakatwa, Kwa kufanya hivyo unaongeza ajira.
4. Vijana wote ambao hawana ajira na hawana biashara Kwa sababu ya wimbi la umasikini kwenye familia zao yafanyike yafuatayo;-
I) wahitimu wote wenye umri wa miaka 18-35 wenye elimu ya chuo wapelekwe JKT watumike miaka 10 Kwa mkataba, kama ilivyo Suma JKT inasimamia miradi Kwa weledi hadi raha, watoe Kwa hawa wahitimu Kila wilaya kulingana na alichosomea, mfano kilimo , ufugaji, ujenzi, umeme, uvuvi, na walipwe mishahara Kila mwezi kulingana na uzalishaji katika wilaya husika.
-Baada ya miaka 10 walipwe pension yao
-Suma JKT isimamie shughuli hii na serikali itoe sapoti Kwa kipindi Cha mwanzo kabla ya uzalishaji , baada ya uzalishaji wajisimamie, tractor zipo mashamba yapo, watu wapo , Je nani alaumiwe Kwa ukosefu wa ajira mhitimu au serikali?
II) Serikali ianzishe miradi itakayoweza kuajiri vijana wengi.
-Tatizo la viongozi wanaopewa kusimamia miradi ya uzalishaji wanaua na hapa ndo chimbuko la jobless, Kila mradi wanaua, Kila mradi wanaua, serikali kuweni wakali katika hili kama hakuna mradi unaweza simama je tutaajiriwa wapi?
-Itungwe sheria Kali juu ya usimamizi wa miradi ya uzalishaji, mtu akibainika amehujumu mradi afukuzwe kazi, afilisiwe, utupwe jela......very sad, hata UDART TUMESHINDWA KUSIMAMIA ! .....Je tunaajirika?
-miradi kama, kilimo Cha umuagiliaji, usindikaji wa mazao, ufungashaji wa bidhaa, viwanda vilivyokufa vifufuliwe.
5. Sekta binafsi zitoe mikataba na Kwa kuzingatia salary scale.
-Kuna baadhi ya tasisi binafsi zinanyanyasa sana wafanya kazi, malipo duni, dhuluma, hawawekewi fedha zao Kwenye NSSF
* Serikali imekuwa ikichangia kuwakandamiza wafanya kazi wa sekta binafsi hasa wenye degree, mfano mtu anapewa laki na thelathini kama mshahara Bado serikali inadai mtu huyu alipe loan board jamani huu sio utu ,ombi langu SERIKALI IFUTE MADENI YA LOAN BOARD KWA AMBAO HAWANA AJIRA ZA KUWELEWEKA KWA SABABU WAAJIRI WENGI WANAKWEPA MTU WA DEGREE ETI KISA WANATISHIWA KUFIRISIWA ASIPO LIPA FEDHA KWA MTUMISHI ANAEDAIWA LOAN BOARD.
-Serikali muwe karibu na watumishi wa sekta binafsi huu ni mwiba ........
6.Tasaf ifungwe
- mradi wa kunusuru kaya masikini ufungwe , badala yake hizo fedha zitumike kujenga vituo vya kulelea wazee wasiojiweza na watoto yatima, hii ni Kwa sababu fedha nyingi za Tasaf haziwafikii walengwa.
7. Shughuli za kitaalam zifanywe na wataalam pekee sio Kila mtu ilimradi anapesa.
-Nimeshuhudia maduka mengi ya madawa baridi ya binadamu na wanyama wauzaji hata form one hawajafika, Je serikali hii ni sawa?
-Pembejeo za kilimo zinauzwa kiholela hii ni hatari Kwa afya ya jamii na soko la ajira, mwenye mtaji amwajili mtaalam ndivyo theory of x and y inatuambia.
8. Serikali ndio yenye jukumu la kuwatafutia wananchi wake fursa na ajira.
-Serikali ilipe wahitimu mishahara mpaka wapate ajira.
-Katika kipindi Cha 2021 hadi Sasa nimeshuhudia ajira nyingi sana zikitolewa na serikali yetu pendwa .
-Katika kipindi Cha 2021-hadi Sasa nimeshuhudia madarasa yenye vigae karibu nchi nzima kwenye shule za serikali, zahanati na hospital nyingi zimejengwa.
-Hii inanipa matumaini makubwa sana Kwa mheshimiwa Rais SAMIA SULUHU HASSAN, YAKWAMBA 2025-2030 ATATENGENEZA AJIRA NYINGI SANA NA FURSA KWA KILA MTANZANIA, KAMA JINA LAKE LILIVYO SULUHU.
-MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI VIONGOZI, WAPIGA KURA NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA.
Naomba kura Yako ahsante.

Upvote
5